Google Pixel 8 Pro iko vizuri kuliko nilivyodhania

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,847
5,352
SECTION A: FEW POINTS ABOUT GOOGLE PIXEL 8 PRO

Screenshot_2023-12-28-19-52-40-638_com.android.chrome.jpg

Hapo juu ni Google Pixel 8 (kushoto) na Google Pixel 8 Pro kulia.
Screenshot_2023-12-28-19-57-31-888_com.android.chrome.jpg

Kampuni ya Kimarekani ya Google wametoa Google Pixel 8 series juzijuzi tu na tayari zimeshafanyiwa reviews nyingi tu. Kama mnavyojua Google Pixel silaha yake ni kamera.
Screenshot_2023-12-28-19-54-41-001_com.android.chrome.jpg

Hiyo picha hapo juu inaonesha kamera 3 za Google Pixel 8 Pro, 50MP (wide), 48MP (ultra wide) na 48MP (telephoto).
Kwenye kamera Google Pixel haijawahi kufanya vibaya na mwaka huu kwenye Google Pixel 8 Pro wamefanya improvement kwenye kamera, kasome review ya gsmarena wameelezea jinsi Google Pixel 8 Pro ilivyo na kamera matata
Screenshot_2023-12-28-19-56-12-018_com.android.chrome.jpg

Mbele kuna 10.5MP selfie camera. Kamera za mbele na nyuma zote zinarekodi hadi 4K@60fps videos
Inatumia USB Type C 3.2 kwa hiyo inasupport video out.
Ina uzito wa gram 213, ni nyepesi kuliko flagship nyingi za sasahivi.
Screenshot_2023-12-28-19-56-47-959_com.android.chrome.jpg

Google Pixel 8 Pro inatumia processor ya Google wenyewe, "Google Tensor G3 (4nm)". Actually kwenye performance imepitwa na Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3, haifikii hata Snapdragon 8 Gen 2. Gsmarena pia wamethibitisha hata Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 1 ina performance kubwa kuliko Google Tensor G3.
Lakini wote tunajua, Google chipset zake hazijabase kwenye performance kubwa, yenyewe imebase kwenye software optimization na kuwezesha AI features nyingi kwenye simu zao
Screenshot_2023-12-28-19-57-05-410_com.android.chrome.jpg

Ila bado Google Tensor G3 imepata score ya 924853 kwenye AnTuTu v9 na 1151243 kwenye AnTuTu v10 benchmark.
Kusema ukweli hii ni performance kubwa sana ambayo itawatosha watu wengi sana kimatumizi. Sidhani kama kuna haja ya kulaumu Pixel 8 Pro kutofikia uwezo wa simu zenye Snapdragon 8 Gen 3 kwa sababu hata Tensor G3 tayari ni powerful
Sioni ulazima wa kutumia 8 Gen 3, labda kama wewe ni very heavy gamer, ndio itakufaa utafute iPhone 15 Pro Max au simu zenye Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3 kama Xiaomi 14 Pro
Screenshot_2023-12-28-19-53-14-489_com.android.chrome.jpg

Battery lake ni 5050mAh na ina average battery life. Angalia comparison hapa chini
Screenshot_2023-12-28-20-01-05-458_com.android.chrome.jpg

Google Pixel 8 Pro zote zina 12GB RAM, storage zipo 128GB/256GB/512GB/1TB
Display yake iko vizuri sana. Google wenyewe wanadai inafikia 2400nits ila gsmarena wameitest wamepata 1600nits ambayo bado ni kubwa sana. Mfano, angalia hapa chini utaona kuwa kwenye brightness anapitwa na iPhone tu
IMG_20231228_200038.jpg

Inasupport NanoSIM na eSIM, pia tunajua Google haiko vizuri kwenye fast charging technology kama Xiaomi, Oppo, Vivo na Wachina wengine ila haiko vibaya sana. Kwa kutumia charger official ya 30W kutoka kwa Google mwenyewe unaweza kuchaji Pixel 8 Pro kutoka asilimia 0 hadi 100 kwa saa 1 na dakika 23. Sio mbaya


SECTION B: SOFTWARE FEATURES OF GOOGLE PIXEL 8 PRO
Screenshot_2023-12-28-19-56-56-628_com.android.chrome.jpg

OK, nije kwenye main point sasa iliyonifanya nianzishe huu uzi.
Screenshot_2023-12-28-19-53-46-773_com.android.chrome.jpg
Kwanza Google Pixel 8 Pro inakuja na Android 14 na itapokea software updates kwa miaka 7 mfululizo, Just imagine miaka yote hiyo. Hamna kampuni yoyote ile itakayokupa software support kwa muda mrefu hivi, hata Samsung hafanyi hivi.
Ukinunua Google Pixel 8 Pro sasahivi na Android 14 yake maana yake utapokea updates mpaka Android 21.
Screenshot_2023-12-28-19-53-54-491_com.android.chrome.jpg

Pili nilisema hapo awali kuwa Google Tensor G3 imebase kwenye kuimprove na ku-optimise AI features kwenye Google Pixel 8 Pro, hapa chini nitaonesha jinsi Google anavyojitahidi kwenye hii sekta.
Screenshot_2023-12-28-19-53-21-228_com.android.chrome.jpg


Kwenye Google Pixel 8 Pro kuna features zifuatazo.
View attachment 2856114
1. AI SUMMARIES
*Kwenye Google Pixel 8 Pro kuna feature inayokuwezesha ku-summmarize article uliyoiona mahali popote mtandaoni, iwe Wikipedia, iwe gsmarena, au hata Jamiiforums. Hii feature inafanya kazi kwenye Chrome browser.
Ukiingia Chrome, ukasearch kitu mtandaoni labda habari kwenye website ya The Guardian kuhusu Samia kuuza bandari, halafu habari yenyewe ina maneno mengi unaona uvivu kuisoma, kwenye Google Pixel 8 Pro unaenda kwenye hiyo habari, unahold power button utaona option imeandikwa "Summarize" ukiitap hiyo Summarize, AI itasummarize habari hiyo katika maneno machache tu na itakuambia key points kwenye hiyo article ni nini.
Screenshot_2023-12-28-19-06-48-659_com.google.android.youtube.jpg

Feature nyingine inaitwa "Read aloud". Kama uko gsmarena unasoma review ya Xiaomi 13 Pro halafu unaona review ni ndefu na ina maneno mengi, unaenable hii feature ya Read aloud, then simu itakusomea kilichoandikwa kwenye article hiyo. Wewe kazi yako inakuwa kusikiliza tu. Pia unaweza kupunguza speed, iwe inasoma haraka, taratibu au kawaida.
Screenshot_2023-12-28-19-07-57-299_com.google.android.youtube.jpg

Feature hizi zinapatikana kwa watumiaji wa Google Pixel 8 Pro waishio Marekani tu ila hata kama unaishi Nachingwea unaweza kuzipata kwa kutumia VPN na kuchagua server za USA.

2. WALLPAPER CUSTOMISATION
Kwenye Google Pixel 8 Pro unaweza kutumia AI kutengeneza wallpaper. Kwa mfano unaweza kuiambia AI ikutengenezee wallpaper ya jengo la kifalme lililoezekwa na manyoya kwa juu na madirisha yake yawe yanatoa mwanga wa njano, then AI inakutengenezea wallpaper tatu tofauti za hicho ulichomwambia. Iko vizuri sana
View attachment 2856105
Pia kuna feature inaitwa "Emoji Workshop". Hii inakuwezesha kutengeneza wallpaper yako mwenyewe kwa kupangilia emoji kwa ubunifu unaoujua wewe then unacustomise hiyo wallpaper kupitia style mbalimbali ambazo Google amekuwekea. Mwisho wa siku unapata wallpaper unyama sana, iliyoundwa na emoji mbalimbali
View attachment 2856106



3. LOCK SCREEN CUSTOMISATION
Kwenye Pixel 8 Pro, Google wameextend uwezo wa ku-customize Lock screen

Unaweza kuchagua clock styles tofauti tofauti, pia unaweza kuongeza au kupunguza size yani kufanya namba kuwa kubwa au ndogo, ukitaka saa ijae kwenye screen yote ni wewe tu.View attachment 2856107

Jambo jema ni kwamba kila style ya saa utakayoiweka, Google wameshaitengenezea mwonekano wake unique utakaoonekana unapotumia Always on Display. Mwonekano wa simu unakuwa bomba sana

Pia kuna feature ambayo inakuwezesha kuweka statement mbalimbali kama misemo, methali, nk kwenye lock screen, kama hivi hapaView attachment 2856108

4. PRO CAMERA
Kamera ya Google Pixel 8 Pro ni kali sana, pia wakati wa kupiga picha unaweza kucontrol settings kwa kuongeza au kupunguza brightness, shadows, focus, white balance nk.

5. AI PHOTO EDITING
Kuna feature kwenye Google Pixel 8 Pro inaitwa "Best take" hii inakuwezesha kubadili mambo mbalimbali kwenye picha kwa kutumia akili bandia kuzifanya ziwe unavyotaka wewe
Kwa mfano unataka upige picha na watoto wako wawili lakini kwa bahati mbaya watoto wako wawili wanalia na hawataki kunyamaza muda wa kupiga picha, we piga picha hivyohivyo tu. Baadae kupitia "Best Take" unaweza kutumia AI kubadili sura za watoto wako wanaolia na kuzifanya ziwe sura za kutabasamu, au waonekane wanacheka, ushindwe wewe tu. Google wameweka option nyingi sana kwa hiyo unaweza kuedit sura iwe kwenye emotion state yoyote ile View attachment 2856110

Feature nyingine ni "Magic Editor". Hii inakuwezesha kufuta vivuli kwenye picha, kuremove object kwenye picha au kumove object kutoka position moja au nyingine kwenye hiyohiyo picha.
Kwa mfano mnapiga picha ya kifamilia pale Posta halafu nyuma watu wanapitapita. Unaweza kutumia Magic Editor kufuta wale watu ambao hawaitajiki kuonekana kwa kutumia AIView attachment 2856111

6. AI VIDEO EDITING
*Audio Eraser: Hii ni feature inayokuruhusu kufuta sauti zisizohitajika kwenye video. Kwa mfano unajirekodi ukiwa unaongea kuhusu Simba kufungwa goli 5 na Yanga, then kwenye mazingira uliopo kuna kelele za ndege wanaoimba, au mbwa anabweka, au kelele za magari na pikipiki, upepo au maporomoko ya maji, nk unaweza kutumia AI kufuta hizo sauti nyingine na isikike sauti yako tu sio ya maporomoko ya maji. Feature hii inaitwa Audio Eraser

*Speech enhancement: Feature hii inakuwezesha kupunguza background noise ukiwa unarekodi video. Mfano unajirekodi unaongea ila pembeni kuna mtu anakata mti na chainsaw, unaweza kupunguza sauti ya chainsaw ili kwenye video sauti yako ndio isikike vizuri zaidi

7. TEXTING
Google Messages ya kwenye Pixel 8 Pro ina feature mpya nzuri sana iliyonivutia. Unaweza kumwandikia mtu message halafu kwenye kusend hiyo message unachagua hiyo message imfikie huyo mtu saa ngapi, au Juma ngapi pia unaweza kuset imfikie tarehe 29/December saa 9:51 alasiri. Kwa hiyo unasend message na haimfikii mpaka ufike muda au tarehe uliyoiset wewe
View attachment 2856112

Flash Notification; Kuna feature moja ambayo unachagua rangi ambayo unataka display yako ioneshe pale message inapoingia. Mfano ukichagua rangi ya blue, message ikiingia kioo cha simu yako kitakuwa kinawaka rangi ya blue na kuacha mara chache ili ujue kuna ujumbe umekufikia

8. AI FACE LOCK
Kwenye Google Pixel 8 Pro unaweza kutumia Face Lock kulock hadi application zako. Kwa hiyo mtu mwingine hawezi kufungua hizo apps mpaka wewe mwenyewe uiangalie simu yako

Pia kuna feature ya "Skip lock screen" Yani ukiishika simu yako kama umeweka Face Lock ukiiangalia tu inawaka na kufunguka hapohapo bila kukuonesha Lock screen

9. PRO BATTERY
Kwenye simu zetu sometimes tunawasha Battery saver, au hata ile Ultra battery saver. Hii Ultra-battery saver kwenye Google Pixel 8 Pro inaitwa "Extreme battery saving mode" Unaweza kuset kwamba ukiwasha battery saver, automatically simu inajiweka kwenye "Extreme mode" badala ya ile Battery saver ya kawaida

Jambo lingine zuri ni kwamba unaweza kuset asilimia ambazo betri ikifikia tu, battery saver inajiwasha automatically. Mfano unaweza kuset battery ikifikia asilimia 35 tu, battery saver inajiwasha
View attachment 2856113
Halafu kuna feature nyingine kwenye Google Pixel 8 Pro inaitwa "Battery diagnostics". Kwa mfano simu yako inaisha chaji haraka kuliko kawaida au inapata joto kuliko kawaida unaenda kwenye battery diagnostics, unaelezea shida ya battery yako labda "My phone is overheating" then feature hii itakuonesha possible reasons za simu yako ku-overheat then itakushauri cha kufanya kupitia maneno, labda uzime mobile data au turn off Location services, nk

10. QUICK SETTINGS
Share Link as a QR Code: Feature hii inakuwezesha ku-share link kwa njia ya QR code, mfano upo gsmarena.com unataka kumtumia rafiki yako aliye karibu link ya hiyo site, simu yako itakutengenezea QR code chap tu then rafiki yako anatumia simu yake ku-scan hiyo code then link inafunguka kwenye simu yake pia

Pia sasahivi unaweza ku-share picha kwa kudrag tu hiyo picha kutoka app moja kwenda app nyingine

Pia Google Pixel 8 Pro imekuja na built-in thermometer. Kwa hiyo unaweza kuitumia simu yako kupima joto la vitu vinavyokuzunguka kama maji, wale wa laboratory mnaweza kupima temperature ya mixture ya conc H₂SO₄ na H₂O kwa kusogeza simu yako karibu na vessel yenye hiyo mixture
Ila thermometer ya hii Google Pixel 8 Pro haiwezi kupima joto la binadamu. Inapima joto la vitu tu.View attachment 2856115


Kuna baadhi ya feature hapo ni kwa watumiaji wa Google Pixel 8 Pro wa Marekani tu. Lakini hata kama unaishi Chitoholi huko unaweza kuzipata pia. Tumia Surf Shark VPN, halafu chagua servers za USA. Simu itaonesha kuwa upo Marekani then unaenjoy hizo feature nzuri na za kuvutia za Google Pixel 8 Pro.

All in all, Google Pixel 8 Pro ni flagship nzuri sana. Kwa wale wanaotafuta flagship nzuri kwa matumizi ya kila siku hakuna haja ya kununua iPhone 15 Pro Max, nunua Google Pixel 8 Pro uenjoy feature nzuri za kipekee na upate 7 years of software updates.
Pia Google Pixel 8 na Google Pixel 8 Pro ni bei rahisi kuliko iPhone 15, iPhone 15 Plus, iPhone 15 Pro au iPhone 15 Pro Max.

Kuna wale ambao tunapenda laptop za MacBook ila hatupendi iPhone. Ili uenjoy MacBook vizuri inabidi uwe na iPhone Hapana sio lazima uwe na iPhone. Hata kama una Mac Book usisite kununua Google Pixel 8 Pro kwa sababu hata simu za Android zinafanya kazi vizuri tu na MacBook. Soma hapa

Muwe na siku njema
 
Msiwekeze Hela zenu Huko, Far Better mtu ununue Samsung ama Iphone!
Samsung na Apple wote wana simu nzuri
Ila Google Pixel 8 Pro ni very new phone na inakuja na features zote hizi kwa 2.2M, hapo muda si mrefu bei itashuka hadi utashangaa

Google Pixel 8 Pro ni simu nzuri sana. Reviews nyingi zimei-appreciate, hakuna haja ya kuitoa maana as if ni Tecno ya laki 2
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom