Ghafla jicho halioni vizuri

galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
978
1,305
Wakuu habari za majukumu. Leo nimeamka asubuhi, najikuta jicho langu la kushoto halioni vizuri. Inakuwa kama unaangalia ukungu (fog), lakini pia mwanga wa dirisha unapoangalia dirishani hali huwa mbaya zaidi. Sijawahi kupata tatizo lolote la macho. Naomba wenye ufahamu na tatizo hili. Natanguliza shukrani.
 
nilikuwa nawaza hivi pia.
Mie baba yangu alienda shambani, bahati mbaya akakuta mahindi yote yameliwa na ng'ombe na hajui ni ng'ombe wa nani, hapo hapo anasema aliona ukungu jicho moja likawa halioni sawia, alivyoenda KCMC ndio wakagundua kuwa amepata presha ya macho, alitibiwa na sasa yuko mzima kabisa, hivyo wahi kapime hata ukikutwa nayo inatibika bila shaka yoyote
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…