Genge la Mafisadi na Viongozi Wastaafu waliotumika kuchafua Utawala wa Magufuli

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
2,155
4,921
Hizi ni habari za ndaaaaaani kabisa ambazo wengi hawazijui na wengine wanazijua ila wameamua kunyamaza kwa sababu kadhaa. Magufuli hakuwa Malaika. Hilo lazima tukubaliane kama Binadamu kama Rais kuna makosa alifanya. Tuendelee na mada yetu.

Mara baada ya Magufuli kuingia madarakani haraka sana alitangaza vita dhidi ya Mafisadi,wahujumu na wauza madawa ya kulevya.

Siku zote haya makundi popote pale duniani huhusisha Viongozi wakubwa Serikalini wa Chama pia na Taasisi mbalimbali. Mtandao huu ulikuwa mkubwa ukihusisha na watoto wa Vigogo ambao walijiwekea pesa nying sana offshore. Kwenye mabenk ya kimataifa huko nje na nyingine kwenye majumba yao.

Ndani ya serikali yake akaanza kutengeneza maadui. Ni wazi asingeweza badilisha kila mtu kila nafasi aliyokuwa nayo kuweka mtu mpya. Kuna watu ambao waliendelea kuwa waaminifu kwa viongozi waliopita kwa kuwapa taarifa na kuamua kumkomoa kutokana na kuziba baadhi ya njia za kifisadi na wizi wa mali ya umma.

Mnakumbuka mmoja ya Wauza madawa ya kulevya ambaye alikamatwa na alikuwa jeuri akapiga simu kwa mkuu wa taasisi ambaye kumbe wakati anapigiwa simu alikuwa na Magufuli na Mkapa. Mkuu wa taasisi akaambiwa aweke Loud speaker. Raia yule wa kigeni akaanza kulalamika na kutukana kuwa vijana wake wamemdhalilisha kumkamata.

Akata mstaafu mmoja mkubwa ajulishwe. Hakujua kuwa aliwekwa loud speaker. Magufuli alikasirika sana na kusema huyo mstaafu anamharibia nchi. Kama si busara za Ben Mkapa hali ilikuwa mbaya sana. Aliyekuwa mkuu wa taasisi mojawapo ya ulinzi aliondolewa yule aliyekuwa anashirikiana na wauza madawa ya kulevya.

Hali hiyo ya kutoridhishwa na Magufuli iliendelea.naye akijua maeneo ambayo kuna ufisadi mwingi ulitengenezewa ngome. Mishahara hewa ilikuwa ni moja ya kitega uchumi kwa baadhi ya viongozi taasisi flani flani.

Likaja suala la vyeti fake. Yes. Kuna watu ambao tulifaidika sana na vyeti fake na hawa walipewa taasisi kadhaa wakafanye kazi huko. Ufanisi ukapungua sana. Vyeti vingi vilichongwa kwa ngazi za Diploma,Degree na Masters. Hasa Diploma na Degree. Hawa ulikuwa unawakuta wengi tu serikalini. Wizarani na mashirika kadhaa ya serikali. Hawa walikuwa pigo jingine katika taifa ambao pia waliadhirika sana na utawala wa magufuli.

Kumbukeni walikuwa na ndugu, walikuwa na watoto na walikuwa vijana pia. Wakasambaza chuki na kisasi sababu ya wazazi na watoto wao. Mimi kazini nilishuhudia ofisini watu 17 wakiwa na vyeti fake. Wakaondolewa kazini. Wakiwa nafasi nyeti sana wengine.

Kisasi na chuki kikawa kikubwa. Magufuli alifikia hatua akawa hamuamini mtu. Sababu alijua kila mara kuna watu walikuwa wakitoa taarifa nje kwa mtandao flani. Mtandao wa kifisadi, mtandao wa wauza madawa.

Hali hii iliendelea na wengine wakaona waje na mbinu mbadala. Ya kumchafua kwa kila namna na kutengeneza hali ya kutoaminika au kukosekana amani. Naye Magufuli akakosa subra akawa na hasira na chuki kwa watu kadhaa. Mara nyingi Ben Mkapa na Askofu Pengo ndiyo ambao waliweza mtuliza. Hata siku ile amemfungia ikulu chini ya uangalizi mke wa mstaafu mmoja mhuni. Aliyeenda kumwomba amwachie alikuwa Ben na Pengo. Hawa ndo Magufuli aliwaelewa na kukubaliana nao kuwa basi asawazishe kwa kumpa nafasi huyo mke kuondoa chuki na mstaafu.

Kama haitoshi ndo yakaibuliwa na Kibiti. Waliokuwa wakifanya ugaidi Kibiti ni watanzania ambao walikuwa wakifadhiliwa na watanzania wengi wakiwa ni viongozi wastaafu. Makusudi waliamua kuleta hali ya sintofahamu katika utawala wa Magufuli. Hawa walikuwa wakipata taarifa za ndani kabisa za kipolisi. Vikao vyote ambavyo vilikuwa vya kimkakati kuwadhibiti walikuwa taarifa zake wanazipata.

Wahusika walikuwa matajiri kadhaa kwa kushirikiana na viongozi wastaafu na waliokuwa katika taasisi za serikali. Hali ilikuwa mbaya kwa askari wetu wengi kuuawa na baadhi ya watu ambao walikuwa wakisalitiwa na wenzao.

Ndipo jeshi lilipoomba kushughulika lenyewe bila kushirikiana na askari. Ndo kwenda kumaliza ule uasi wa kigaidi. Hapo ilibidi watumike baadhi ya watu ambao walikuwa kwa kujua ama kutojua wakicheza ngoma za kichawi. Waandishi kama akina Azory Ngwanda (Mungu airehemu familia yake) na akina Erick Kabendela.

Hawa walitumika kimataifa na kitaifa kuandika mambo ya kweli na yasiyo ya kweli kuuchafua utawala ambao ulishaamua nao liwalo na liwe. Magufuli aliendelea naye kuact katika panic mode na wenzie wakitumia nafasi hiyo hiyo kumtengenezea mambo ya hovyo.

Kumbuka kipindi hiki kisiasa alikuwa ameshagoma kuwa anawapa bakshishi akina Zitto, Mbowe et al. Hawa walizoea kuwa wanapoyakoroga sana wanaitwa na Rais anawatuliza wanatulia. Magufuli aliwakataa hawa na kutengeneza uadui nao mkubwa. Naye akaamua kutumia nguvu kuwadhibiti.

Operation ya pili ikawa ni kumwondoa duniani..... Hii ndo ilikuja kufanikiwa. Hayo ya kuambiwa alikufa kwa Covid 19 ni katika hali ya kuwa brainwash tu watu. Magufuli hakufa kwa Covid 19. Mimi sikuchoma Chanjo na nmezunguka na viongozi toka yeye na na hawa wengine. Nlitengeneza tu cheti fake kwa tsh 100,000 sijawahi umwa Covid 19 wala Covid 20.
 
Wastaafu hivi.
Wastaafu vile.
Lakini hakuna hata jina moja la mstafu.
Wewe na yule alieandika kuwa "vyanzo vya kuaminika vya upinzani na serikalini" ni sawasawa.

Naona inatumika nguvu kubwa sana katika "kumsafisha na kumtakatifusha" mwenda zake kama ambavyo inatumika nguvu kubwa kuweka mambo "yanayosemwa" yalifanywa naye hadharani.

Kwa nini sasa!!??
 
Umesomeka.
 
Mkuu kumbe na wewe ni walewale ,kwa ulifoji cheti cha Covid? ulikuoa unaogopa nini kuweka msimamo wazi kwamba huchanji badala yake ukaenda chonga chet kwa 100,000?

Tukisema inchi ipo na watu wa ajabu utakataa?
Sasa wewe na wale waliofoji vyeti mpo na tofauti gani?
 
Mkuu hebu tuwekee vielelezo vya hiyo simu iliyopigwa mbele ya raisi Magufuli akiwa pamoja na Mkapa, ili na sisi ambao hatukuwahi kuliona au kulisikia hilo tukio tuweze kuliona na kulisikia hapa kwenye uzi wako.

Maana isije kuwa yale ya Lowasa kuchafuliwa kwa sababu za kisiasa, na baadae kusafishwa kwa sababu hizo hizo za kisiasa.

Tanzania watu, au mtu anaweza akakuchafua kwa kukuanzishia shutuma za uongo, na watu wanaokuchukia wakaunga mkono kuwa za kweli. Kumbe nyuma ya pazia ni za uongo. Hivyo unavyotoa shutuma za aina hii ni vyema ukatuwekea na vielelezo ili tujiridhishe kwamba ulichoandika ni cha kweli, hakina chenga ya uongo wala chuki ndani yake.

Pia ingekuwa vizuri ukatuambia na jina la huyo mstafu na cheo chake alichostafia. Je ni raisi mstaafu? waziri mkuu mstaafu? katibu mkuu kiongozi mstaafu? Waziri mstaafu? au katibu mkuu mstaafu?
 
Mkuu kuongezea suala la Kibiti lilianza mapema kabla Magufuli hajaingia madarakani. Magufuli amelikuta katikati, mtoa hoja afanye utafiti wake vizuri.
 
Vita ya uchaguzi imeanza mapema sana lakini pia ajabu watawala wameanzia battle na marehemu ambae hana madhara wanawaacha wapinzani walio hai wenye madhara inashangaza sana.
Kuna jambo linajionesha hapa kuwa matendo yake na heshima yake bado inaishi kwenye mioyo ya wapiga kura na inawaumiza watawala. R.I.P Magufuri better try than never.
 
Hizi ni blablaa za kujitungia
 
Umeandika ngonjera ndefu sana lakini imekosa content.

Unasema tu kuwa Magufuli alia-act katika panic mood, lakini hujasema ni yapi hayo ambayo aliyatenda in panic mood!! Ndiyo hayo ya kum-shoot Ben Sanane kwa mkono wake? Ndiyo hayo ya kumwua Azory Gwanda? Ndiyo hayo ya kutaka kumwua Tundu Lisu? Umezungukazunguka sana lakini hujasema huo uovu alioutenda katika panic mood..

Kikubwa hapa unachotaka kuonesha ni kuwa marehemu alikosa sifa muhimu za uongozi, maana kiongozi inatakiwa wakati wote, katika mazingira ya aina yoyote anatakiwa awe na uwezo wa kudhibiti hasira yake, na kufanya maamuzi ya busara katika kila jambo. Lakini wewe unataka kutuaminisha kuwa marehemu hakuwa na busara, na alikuwa anaamua na kufanya mambo in panic mood, ndicho ulichokilenga?
 
Watu fake wengi sana
 
Kuna ukweli mkubwa.

Ukiangalia wakati ule wa mambo ya Kibiti, Mkuranga, Mawazo, Zitto Kabwe hasa Kabendera walitumika kuandika kwenye magazeti ya kigeni kwamba nchi haina amani, haki za binadamu zinavunjwa, Tanzania iwekewe vikwazo, kuwe na uchunguzi wa kimataifa kisa magaidi wengi waliuwawa.

Magufuli aliamua kudeal na magaidi jino kwa jino, kuwauwa wote bila kupotezeana muda kuwafikisha mahakamani.

Hawa ni magaidi waliokuwa wanaua watu ovyo, wanavamia vituo vya polisi, kuua askari na kuchukua silaha zao. Zitto na Kabendera hawakuwahi kutetea haki za hawa waliouwawa na magaidi bali walikuwa mbele kutetea haki za magaidi.

Kabendera alikuwa analipwa pesa nyingi sana kwa article chache obvious alikuwa na bado anatumika na bado anatumiwa na vyombo vya ujasusi vya magharibi kusambaza pesa kwa wakala wao hapa Tanzania.

Sasa hivi anatumika kumchafua JPM kuweka mambo sawa kwa uchaguzi wa October 2025 kwa kumbambikia uchafu wowote, vitu vyote vichafu, kashfa zote za ovyo unazoweza kumpa binadamu bila ushahidi wowote.
 
Na mimi ni wale wale tu ndugu yangu. Tupo wengi. Nisingechonga cheti nsingekuwa nasafiri nje ya nchi. Halafu nisingekuwa napata mshiko...watoto wangu wasingeenda choo
 
Umeingiza bei gani Kwa andiko km hiki?
 
Lakini nashangaa Magufuli alifariki mwaka 2021 haya ya sasa yanawasaidia nini hawa ndugu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…