FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 39,352
- 45,376
Kwa anaye fahamu sababu ya kuiba vinu vya kutengeneza matairi ya ubora wa hali ya juu kutoka kiwanda maarufu Nchini na Duniani kilichokuwepo Arusha juzi juzi tu cha General tyres na kuvihamishia Kenya ambapo wanavitumia kutengenezea matairi ya Yana tyres then wanakuja kutuuzia hayo matairi huku Tanzania, nini chanzo?
============================
==========================================
==================================
=====================================
============================
Mkuu Mimi niliwahi kufanyakazi General Tyre so kila hatua ya kuifisadi na kuizika niliiona kwa macho yangu mawili.
Kwanza nakanusha kwa sauti kubwa hakuna mold (kinu) cha kupika tyre kilichohamishiwa Yana Kenya. Kilichofanyika ni kuhamisha teknolojia ya kutengeneza tyre baadhi ya sizes hasa 7.50 - 16 HCT 10 PLY ambayo ilikuwa na soko kubwa Tanzania, Congo DRC, Somalia na Kenya kwenyewe.
Kilichofanyika enzi za Mzee wa uwazi na ukweli ni kumruhusu aliyekuwa Mkurugenzi mkuu Devendra Lohani kufanya anavyotaka ikiwa ni pamoja na kupewa mkopo mkubwa kutoka NSSF U$ 10 Million kwa ajili ya kumodernise (mitambo ya kisasa) halikufanyika hata kidogo na bado maengineer & technician wakalazimishwa kuuza formula ya kutengeneza hiyo tyre ambayo msomali mpenda vita alikuwa akiifunga kwenye Land Cruiser p/u na mtutu wa bunduki kubwa alikuwa na uhakika na tyre za general tyre zitafanya kweli.
Enzi hizo hakuna gari iliyokwenda Manyara, Ngorongoro, Serengeti bila kufunga 7.50 - 16 SHCT 12 PLY au 10PLY. Demand ilikuwa kubwa mno ikabidi General tyre mabor Msumbiji watupatie mold za 7.50 - 16 HCT ili kukabiliana na mahitaji makubwa. Pamoja na kuzalishwa kwa siku zaidi ya 1,350 bado ilishindikana kukidhi mahitaji.
Kuona hivyo YANA wakatumia pengo la uongozi na uadilifu wakaanza kuzalisha 7.50 - 16 yenye profile sawa na General Tyre na wakati huo huo juhudi kubwa za kukifunga kiwanda cha General Tyre ambayo ilikuwa chini ya mwenyekiti wa bodi Shelukindo William zilikuwa zikipamba moto.
Mungu mkubwa 7.50 - 16 YANA siku hizi imekumbana na kichapo cha ukweli kutoka Goodride 235 / 85 R 16 tubeless kutoka China imeiondoa kwenye soko kiasi kikubwa. Magari mengi ya utalii siku hizi yameachakufunga YANA kutokana na kukosa ubora na bei yake kuwa juu.
Tanzania ya Mwl Nyerere tutaikumbuka sana.
==========================================
Sababu za kufa General Tyre ni kama ifuatavyo.
Mosi, Bodi ya Wakurugenzi ilikuwa ya kisiasa zaidi badala ya kuzingatia utaalamu.
Wajumbe wengi wa bodi walikuwa ni wabunge wa JMT ambao walitakiwa kuyasimamia mashirika ya umma kupitia kamati kama PAC. Madudu yaliyokuwa yakifanywa na management yalikuwa yakipata baraka za bodi kupitia vikao na posho mbali mbali. Wabunge waliokuwa wakiisumbua Serikali kupitia hoja mbalimbali walikuwa wakitupwa kwenye hizi bodi za ulaji pasipo uwajibikaji. Kamati za kusimamia mashirika ya umma mara nyingi zilijikuta zikishindwa kufanya kazi ipasavyo kwa sababu ya kuwa wajumbe wa bodi za mashirika hayo na wakati huo huo wajumbe wa kamati za bunge. Hili Zitto kalisema sana lakini watawala wetu wametia pamba kwenye masikio.
Laiti wanyama pori wangekuwa wanazalishwa kama bidhaa nyingine mashirika kama TANAPA & Ngorongoro Conservation Area Authority yangeshafungwa siku nyingi. Mashirka kama NSSF na PPF tungeshayasahau kama yalishakuwepo.
Pili, ikumbukwe General Tyre ilianzishwa na Mwl Nyerere ambaye alitembelea USA miaka ya sabini mwanzoni akakuta General Tyre Amerika wana modernise kiwanda chao so mitambo ya zamani haikuwa na kazi kwao wakati huo Mwl Nyerere akawaomba General Tyre wailete mitambo ya zamani Tanzania jambo ambalo walilikubali. General Tyre USA wakapewa 26% na Serikali ikamiliki 74%. Mwl Nyerere angekuwa mlaku kama wanasiasa wengine pengine 74% share zingekuwa zake na familia yake lakini hakufanya hivyo.
Katika makubaliano hayo Tanzania ilikubaliwa kuunda bodi na baadhi ya manager hasa HRM na maeneo mengine hasa ya technical wakaachiwa wamarekani. Kwenye bodi aliingia Mkurugenzi mkuu, mkurugenzi wa fedha na mkurugenzi wa uzalishaji wote hawa Wamarekani, Watanzania badala ya kuingiza vichwa vya ukweli tukawapa ujumbe wa bodi akina Gullamal, Shellukindo na Wabunge wengine wengi kwa ajili ya kulipana posho.
Kwa kuwa General Tyre ilianzishwa na teknolojia ya zamani kama nilivyoonyesha hapo juu. Kati ya mwaka 2003 - 2005 sikumbuki vizuri ilikubaliwa kununua mitambo mipya ya kisasa kwa ajili ya kuendana na kasi kubwa ya maendeleo ya uzalishaji wa tyre.
NSSF ikatoa mkopo wa dola 10 milion Serikali ikiwa mdhamini wa mkopo huo. Badala ya kununua mitambo mipya mitambo ya zamani ikapakwa rangi na fedha zote zikatokomea. Utashangaa leo unaambiwa deni la Taifa linazidi kuongezeka ukichunguza utakuta linaongezeka kwa mambo kama haya.
==================================
Kati ya mwaka 1997 - 2005 General Tyre ilikuwa ikilipa VAT Tsh 375,000,000/= hadi 500,000,000/= kwa mwezi. Nikija kwenye kodi zingine ndio utashangaa hawa viongozi wanaolilia madaraka hadi kufikiwa kuwanunua wachungaji na masheikh huku wakiwa hawawezi kutawala hata kuku ndio nashindwa kuelewa Tanzania tuna laana ya nani.
=====================================
Direct employment 450 iliyopotea na bado wakatafuna u$ 10 million za NSSF hakuna aliyefungwa, aliyeshitakiwa ...........