Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 20,575
- 22,501
vuguvugu la mabadiliko linalochochewa na vijana hususan Africa Mashariki, yaani katika nchi za Kenya, Tanazania, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Sudani Kusini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, limechukua sura mpya hivi sasa....
mathalani,
kuibuka kwa gen z wa Kenya kulichochewa zaidi na hali ngumu ya maisha, ikiambatana na ukosefu wa ajira, rushwa iliyokithiri, kodi, tozo na ushuru ambao uliongezwa maradufu na kuboreshwa zaidi kwenye musuada wa fedha kwa mwaka 2024/2025 kitu ambacho kiliwaunganisha vijana wa kenya bila kujali ukabila wao na kuupinga kwa maandamano ya amani, kushinikiza muswada huo tata kurekibishwa...
na hata baada ya sauti, maoni, mahitaji na matakwa yao kuskizwa,
na hatimae Rais wa Jamuhiri ya Kenya kulazimika kuufutilia mbali musuada huo muhimu wa kikatiba, na majuzi kuwafuta kazi mawaziri wake wote na kumfuta kazi mkuu wa jeshi la polisi Kenya. hivi sasa Dr. William Ruto yuko mbioni kuunda baraza ka mawaziri, huenda likawa na sura ya umoja wa kitaifa likijumuisha wapinzani na vijana....
bado gen z wanapanga kuendelea kuandamana, huku wakiibua madai mengine mapya kabisa, kama vile kumtaka na kumshinikiza Rais William Ruto, waliemchagua wenyewe kihalali kikatiba katika uchagizi mkuu wa kidemokrasia uliyofanyika Aug.2022, na kuthibitishwa na mahakama huru ya Kenya, eti aachie ngazi, dah....
kwa muda sasa muungwana,
Dr.William Ruto amekua akitoa wito kwa gen z na makundi mengine ya kisiasa, kiraia na kidini kuja pamoja katika meza ya mazungumzo, kujadili na kuamua pamoja namna bora ya kukidhi na kuboresha hali za maisha, ajira na mambo yanayolalamikiwa....
lakini wamekaidi na kudinda wito huo muhimu sana kwa umoja, utangamano, maendeleo na amani ya waKenya wote...
PLO Lumumba,
mara kwa mara amewaasa na kuwakanya wakenya katika ujumla wao kutafuta suluhu za kistaarabu na amani, katika makosa, dosari na kasoro zinazoonekana na zisizo onekana ndani na nje ya serikali yao, zinazowaathiri waKenya wote kwa ujumla wao nakutafuta suluhu ya amani...
vinginevyo hayupo atakae kua salama likitokea la kutokea,
watakao athirika, watakao umia, watakao poteza maisha, na kuirudisha kenya nyuma ni wenyewe. Ni vizuri kujizuia na ghadhabu katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazotukabili...
Ndugu wanafamilia wenzangu wa JF,
kutoka maandamano ya amani, hadi maandamano ya uharibifu, uporaji, ghasia na mauaji, Je, kuna nguvu, ushawishi, uchochezi au ufadhili wa kisiasa nyuma yake kutoka ndani au nje ya nchi?
unadhani Dr.William Ruto atakubali kuondoka madarakani kwa maandamano tu au atajitea? unadhani nini kitatokea?
wakalenjini wanadai kusimama, kumlinda na kumchunga mtoto wao dhidi ya watakao mletea fujo, hii ina ashiria nini?
baada ya kenya ,
ni wapi vuguvugu hili la gen z linaelekea miongoni mwa nchi za Africa Mashariki