GEITA: Watoto wawili walipukiwa na bomu la kutupa kwa mkono msituni

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Watoto wawili wamejeruhiwa kwa bomu la kutupa kwa mkono katika Msitu wa Kanyala wilayani hapa walipokwenda kutafuta kuni

Wiki iliyopita msitu huo uliopo wilayani hapa ulitumiwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mazoezi

Mtoto Frank Salim (14) aliyeumia miguuni alisema alijeruhiwa alipokuwa na mwenzake Yohana Alex (18) ambaye amejuruhiwa tumboni

Alisema Alex aliokota bomu hilo na alitaka kuligonga kwenye jiwe lakini wakati akimuonya lililipuka na kuwajeruhi

Akizungumza kwa taabu akiwa chumba cha wagonjwa mahututi, Alex alisema alipokiona kipande cha chuma alifikiri ni almasi

Akizungumza jana Alhamisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema kuwa tukio hilo lililotokea juzi jioni. Alisema chuma cha bomu hilo kilimjeruhi mtoto mmoja na kuingia tumboni na hali yake ni mbaya

Mwabulambo alisema kabla ya tukio hilo, Jeshi la Wananchi lilitangaza kufanya mazoezi katika msitu huo. Hata hivyo, alisema Polisi wamewasiliana nao ili kuondoa mabaki ya mabomu yanayoinekana msituni

Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu aliwatembelea watoto hao waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita aliiomba Serikali kubeba jukumu la matibabu

Alisema msitu huo unatumiwa na wananchi kuokota kuni na kuchunga mifugo, hivyo iwapo ukaguzi hautafanyika haraka kuna uwezekano wa kutokea madhara makubwa

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Brian Mawala alisema aliwapokea watoto hao saa kumi na moja jioni

Alisema Alex amefanyiwa upasuaji baada ya kubainika bandama lilipasuka na hali yake inaendelea vizuri

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema Kikosi cha Jeshi Namba 663 Mkoani Mwanza kiliomba kutumia msitu huo kulenga shabaha ikiwa ni sehemu ya mazoezi kwa wanafunzi

Alisema eneo hilo ambalo lipo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) haliruhusiwi wananchi kuingia bila kibali.

Chanzo: Mwananchi
 
Watoto wawili wamenusurika kufariki dunia kwa kulipukiwa na kitu kinachosadikika kuwa ni bomu katika msitu wahifadhi wa Kanyala uliopo nje kidogo ya mji wa Geita.

Watoto hao walikwenda porini kutafuta kuni ndipo mmoja wao akaokota vitu viwili vinavyosadikika kuwa ni bomu huku mmoja wa watoto hao akimsihi kutochezea vitu hatarishi bila mafanikio.

daktari Mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Geita Brian Mawala amezungumzia maendeleo ya watoto hao Frank Salumu aliyepata majeraha mkononi na mguuni na Yohana Alex aliyepata madhara makubwa tumboni.

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi amesema msitu huo wa hifadhi hutumika na serikali kwa shughuli mbalimbali na kwa muda mrefu wananchi wamekatazwa kutoingia na kufanya shughuli za kibinadamu bila mafanikio, aidha ameitaka jamii kuepuka kuokota vitu wasivyovifahamu au kuvitilia mashaka katika eneo lolote mpaka pale watakapotoa taarifa katika ngazi zinazohusika ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Chanzo: ITV
 

HAPO KWENYE RED HAPO NDO HATARI SANA!
 

Hivyo vyombo vya habari vilivyotangaza habari hii vinaweza kugeuziwa kibati muda wowote
 
Sisi watanzania mara nyingi tumekuwa watu wa kulaumu mambo ambayo ufafanuzi wake uko wazi, kwa mfano Mabom Mbagala Mabom G/mboto watu walilaani sana kwamba yameathiri, bila kujali kuwa hizi kambi zilikuwa mbali na sisi raia lakini katika kutafuta maeneo ya kujenga hatimaye tayari tumezizunguka tena kwa umbali ambao hauzidi hata km. Sasa kwa eneo la msitu kama huo marufuku ya kuingia ipo lakini kwanini bado wanaingia, lakini yakitokezea madhara ndio wanaonekana wao JW ni wazembe wakati sivyo.Nijuavyo mimi eneo lolote ambalo hawa JW hufanyia mafunzo yao watu hawaruhusiwi kuingia.
Pole zao.
 
Huyo wa miaka 18 ni zuzu kweli..

Kama lingetoshea mdomoni nadhani angelimung'unya..
 
Acha ujinga, angejuaje ni bomu na elimu haitolewi? Sio kila ujualo weee kila mtu analijua. Huo ni uzembe ulliopitiliza wa hao waliofanya mazoezi. Na wabebe jukumu na sheria ifuatwe na watoto wapewe fidia
Huyo wa miaka 18 ni zuzu kweli..

Kama lingetoshea mdomoni nadhani angelimung'unya..
 
Acha ujinga, angejuaje ni bomu na elimu haitolewi? Sio kila ujualo weee kila mtu analijua. Huo ni uzembe ulliopitiliza wa hao waliofanya mazoezi. Na wabebe jukumu na sheria ifuatwe na watoto wapewe fidia
Kuwekwa kwa zuio kwenye eneo husika inatosha, tatizo kwanini watu waingie eneo hilo. Ni sawa na kusema wewe una dojo lako, then mtu aingie kwenye dojo lako na ang'oe punching bag kwa sababu tu hatambui ni la kazi gani je ni sahihi.
Maeneo yote wanajeshi wanapofanyia mazoezi huwa yameziuliwa wananchi kuingia na hii yote ni kwa sababu ya kuepusha madhara kama hayo, sasa utakuta watu wanaingia kwa kulazimisha. Hao waliofanya mazoezi ni uzembe gani waliofanya na sheria ipi ifuatwe? Kisheria walishakatazwa sasa kwanini wameingia?
 
Acha ujinga, angejuaje ni bomu na elimu haitolewi? Sio kila ujualo weee kila mtu analijua. Huo ni uzembe ulliopitiliza wa hao waliofanya mazoezi. Na wabebe jukumu na sheria ifuatwe na watoto wapewe fidia
Hebu rudia tena kusoma kwa makini kabisa halafu ukimaliza utajua ni nani wakuacha ujinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…