NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,317
- 4,431
Msema kweli ni mpenzi wa mungu na ukiona mtu anakuambia mapungufu yako anakupenda ujirekebishe
Mimi gazeti la MWANANCHI la kwenye mitandao nalipenda sana sababu lina habari za uhakika.
Tatizo ni moja tu huwa sio waangalifu kwenye sentensi na maneno wanayoandika.Naomba kabla ya kurusha huku kwenye mitandao wahakiki sababu linaweza leta athari katika lugha ya kiswahili kwa vizazi vijavyo nitatoa mifano hapo chini gazeti la leo mitandaoni someni maandishi mekundu.
Amesema kati ya Januari na Desemba 2023, diaspora walituma pesa nyumbani zenye thamani ya Dola 569.3
Sahihisho: mwezi Desemba 2023 bado haujafika.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa serikali Mtaa wa Mbae Chundi, Sada Ally alisema kuwa chui wamekuwa tishio katika eneo hilo na kusababisha wananchi wengi kuogopa kufuga mifugo mbalimbali.
“Hawa fisi wamekuwa wakituathiri sana yaani usiku wa kuamkia jana walikuja nyumbani kwangu mabandani nikawafukuza yaani hatuna raha wanakula mifugo yetu sana yaani wanaonekana hadi asubuhi,” amesema.
Sahihisho: wanaoongelewa kichwa cha habari cha gazeti ni Fisi lakini chui amechomekwa hapo.
Tulipofika tulikuta tayari wananchi wenye hasira wameshachoma moto na kuwaua,” amesema.
Sahihisho: mahindi ndio wangesema wameshachoma lakini kwa fisi wangesema wameshawachoma.
Hili gazeti mitandaoni limekuwa likikosea mno mara nyingi hii ni mifano michache.