Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,149
- 6,992
Gari aina ya IST imetumbukia baharini ikiwa na watu wawili eneo la ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam, ambapo watu hao wamenusurika na kukimbizwa hospitali, huku jitihada za kulitoa gari hilo zikiendelea, chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto na uokoaji.
---
Kamanda wa Polisi Kinondoni ACP Mtatiro Kintikwi, amesema wamefanikiwa kulitoa gari dogo aina ya IST lililotumbukia baharini, katika eneo la ufukwe wa Coco uliopo mkoani Dar es Salaam, ambapo amebainisha kuwa walimkuta mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Michael Deus (26), mjasiriamali na mkazi wa Mbezi Louis, mkoani humo.