Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,388
Naam, Nchi yetu kwa sasa inazidi kuharibu dhana nzima ya uongozi sababu ya uwepo wa Nadharia ya Gain acceptance yaani kuhitaji kukubalika. Pia Nadharia ya Referrent Power yaani kuiga nguvu ya uongozi.
Dhana hii ya Gain acceptance/ Referrent power inawaathiri sana viongozi na dhamira ya uongozi.
Hii inatokea endapo viongozi wa chini au kati wanaiga mfumo mzima wa kiongozi/viongozi wa juu.
Viongozi wengi wa kati na chini hufanya vitu ili wakubalike kwa viongozi wa juu ili kupata nafasi zaidi kwa mfano mkuu wa wilaya anaweza fanya chochote kiwe kizuri au kibaya ili kimufurahishe Kiongozi wa juu na pengine anategemea kupandishwa cheo na kuwa hata mkuu wa mkoa.
Mfano wa watu walio jaribu kufanya nadharia ya Gain acceptance/ Referrent power ni Sabaya, Chalamila, Ndugai, polepole, Dorothy Heshima na wengine kipindi cha Magufuli ili wakubali zaidi.
Ukirejea kwa Sabaya ndio sababu ya kumkuta hadi mashitaka aliyo nayo sababu alitaka kumfurahisha Kiongozi wa juu, Mwingine ni Dorothy Gwajima huyu kipindi cha Magufuli alikuwa pia akipinga uwepo wa chanjo na Kuhamasisha Upigaji nyungu na kujifukiza lakini baada ya kuwepo na awamu nyingine ya Samia kiongozi huyo huyo amekuwa akipigia chapuo chanjo. Hii yote ni juu ya dhana ya Gain acceptance/ Referrent power.
Leo hii tumeona Ndugai akitoa kauli iliyo onekana kwenda kinyume na Rais aliyepo hivyo ili kuenda na nadharia ya Gain acceptance/ Referrent power Imemubidi kuomba msamaha licha ya kuwa pengine awali alikuwa sahihi hivyo ili kuendana na uongozi imebidi aukane ukweli wote ili aendelee kubaki kwenye nyadhifa yake pasipo kuathiriwa na utawala huu.
Mwingine leo hii tunaona ndugu Mwigulu nae kuendelea Kuhamasisha ukopaji pasipo kujua unaweza athiri pakubwa Mwigulu: Tutaendelea kukopa, deni ni himilivu kwa vile Mwigulu anahitajika kusifu na kufurahisha uongozi nae anaamua kupigia chapuo nadharia ya Gain acceptance/ Referrent power.
Ndugu watanzania itoshe tu kusema kwamba Gain acceptance/ Referrent power Inaathiri sana mfumo mzima wa uongozi na hii ni kwasababu kiongozi wa juu ukiekinzana nae hata kama upo sahihi basi hutaaminika na kibarua kinaweza kuota Nyasi.
Finally Tukatae Gain acceptance/ Referrent power