Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

Huu mradi naukumbuka sana ulikuwa implemented sengerema pia ukerewe na uliphaseout 2015 December mfadhili wake alikuwa bill&Melinda gates foundation na tatizo la hii miradi ni kuwa mradi ukiisha hata nguvu ya ufatiliaji inatoweka kabisa!ila nilichogundua pia bei ya mbegu ni kubwa sana japo masoko hayatafutwi.
 
Kama kawaida upepo unahamia kwenye viazi lishe.Ndugu zangu kilimo cha kupata milioni 20 kwa heka kwa mvuno mmoja hakipo hata utambike,najua kuna watu watabisha ila watakaoamua wajaribu halafu watuletee mrejesho.Ukiamua kulima usiwe MTU wa kufuata upepo kwani ni lazima upotee
 
Nimekuelewa sana kaka ngoja nijipange kwa ajili ya mbegu ,Je kilimo hiki hakifananai na zile story za jatropha , ufugaji kware ,na ufugaji wa sungura kweli maana wanaoanzishaga huwa wako vzur kwwnye maelezo
 
Hiki ndo kilimo Hamasishi, Kinavutia sana kwenye Makaratasi tunaambiwa hakina changamoto mingi sana kuliko hata uhalisia wenyewe.

Heka moja kwa gunia 19-24,
1. Hatujajuzana kama kinaitaji maji ya kiasi gani???
2. Hatujajuzwa kama kinashambuliwa na magonjwa ya namna gani na tiba zake zikoje,
3.Hatujaambiwa yanakubali kwatika udongo wenye Ph ya % ngapi....

Ila Asante kwa kunipatia hamasa, Kwa kuwa nimeiona namba yako hapo chini ntakutafuta zaidi kwa Shamba darasa la picha zaid
 
Soko la hivyo viazi ni wapi?!! Hakuna soko la uhakika, hakuna muamko waw watu kusisitiza kiazi lishe anapokwenda sokoni, utalima kiazi lishe lakini utauza kama kiazi cha kawaida!
Nimejaribu kusoma kwa makini sana maelezo yake!kwa summary tu ni kuwa wanataka hivyo viazi lishe vilimwe kwa wingi ... wakulima wachangamkie hiyo fursa ya pekee maana kipato kitaongezeka..na akadadavua na mahesabu kabisa!Tatizo kubwa linalowakumba wakulima ni SOKO!ni wapi aende kuuza hivyo viazi lishe vyake!Tunataka aweke wazi je viwanda vya kutengeneza biscuits vinachukua?Je wamejaribu kuhangaika kujaribu soko lake nje?Angalia matunda;nyanya;matikiti na hata mihogo huharibika kwa kukosa soko la uhakika!unapeleka mazao yako kkoo unamkabidhi dalali unasubiri kulaliwa au kutapeliwa kabisa!Tunataka utoe maelezo ya kutosha ya kuhusu soko. .Nataka kishawishi cha kutosha kwa nini nisilime viazi vya kawaida au mazao mengine kama mtama, mahindi,uwele, mbaazi au choroko but nilime viazi lishe!au ni promo tu za kawaida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Demand take ni majanga bora mihogo,songea kule yangu miaka ya2000s vinalimwa tumekula sana tukiwa shule na njiani along songea njombe road wakulima walikuwa wanapanga magunia kutafuta Wateja kwa bei chee sijui kwa sasa
 
 
 
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…