Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,096
Ni miaka mingi sana imepita ila nakumbuka kama vile ilitokea jana tu. Ni siku ambayo yalitolewa matokea ya mtihani wa darasa la saba. Kwa miaka ile enzi ya mwalimu shule za serikali ndio zilikua shule bora kabisa kitaaluma, na elimu katika shule hizo ilikua ikitolewa bila malipo. Japo kulikua na shule za binafsi lakini hazikua bora kwa namna yoyote ile kulinganisha na zile za Serikali(ukiacha shule za seminary). Wanafunzi waliokua wakijiunga na shule kutokea mikoa ya mbali walikua wanasafirishwa na serikali na wale waliotumia nauli zao walikua wanarudishiwa cash walipofika mashuleni kwao!
Miaka hiyo kwa watu wengi sana kama hukuchaguliwa katika shule za serikali(wenyewe tukiita kupass) basi dunia yako na ndoto zako za kielimu zilikua zinaishia hapo. Vijana wengi waliokua na uwezo mkubwa sana wa kitaaluma darasani hata nje ya hapo ndoto zao zilizimwa kwa kutochaguliwa kwenda sekondari na ilikua inasikitisha sana kuwaona walipoishia baadhi ya 'vipinga' wa enzi hizo. Itoshe tu kusema kua ku pass kwenda sekondari ilikua ni ndoto kubwa kwa kila mwanafunzi na mzazi wa wakati huo. Ingawa mpaka leo sijajua vigezo gani hasa vilikua vinatumika kuchagua wanafunzi maana kuna watoto walikua na uwezo mkubwa darasani lakini waliachwa!
Nakumbuka ilikua ni siku ya Jumamosi tarehe za katikati ya December nilipotakiwa na mama nijiandae kwenda sokoni kununua kitoweo soko kubwa la mji huo ambalo lilikua mbali kidogo na sehemu tuliyokua tunaishi, na pia hakukua na usafiri wa umma hivo ilibidi kutembea umbali mrefu kiasi. Sisi tumelelewa katika familia ya kubwa (extended family) tukilelewa pamoja na watoto wa mashangazi, wajomba, baba wakubwa n.k. Kuna wakati home kulikua na familia ya watu takriban 28 na kila mtu alikua amepangiwa majukumu yake.
Wakati nipo njiani naelekea sokoni nikawa nakutana na watu wakiwa vikundi vikundi na baada ya kudadisi nikagundua matokeo ya darasa la saba yametoka na ndio ilikua gumzo la asubuhi hiyo. Akili ikaniruka, mchanganyiko wa wasiwasi na woga juu ya matokeo ukanivaa, nikapatwa na kihoro mithili ya mtu alieenda kupima HIV na sasa ameitwa akapokee majibu yake! safari ya sokoni haikuwepo tena nikabadili njia nikaelekea ofisi za Halmashauri ya mji yanapobandikwa matokeo, nikiwa naomba Mungu katika pumzi zangu hadi nilipofika.
Ilinichukua dakika kadhaa mpaka nilipoliona karatasi lililokua limechapwa jina langu likionyesha namba yangu ya mtihani, shule niliyotoka na shule niliyochaguliwa kwenda kusoma. Nilimshukuru Mungu kwa namna ambayo sikuwahi kumshukuru Muumba wangu kabda!, Nikaondoka pale kimyakimya huku nikijifinyafinya mara kadhaa ili kuhakikisha sipo usingizini, kwamba labda ile ilikua ni ndoto tamu tu pengine muda si mrefu nitaamka. Nusu nilitembea nusu nilikimbia mbio kurudi nyumbani. Nilipofika katika uwanja wa nyumbani nilipiga kelele 'nimepasi nimepasi nimepasi jamani' kisha nikaingia chumbani kwetu (boys) nikajirusha kitandani
Kelele walizopiga wanafamilia baada ya kuwapa habari hiyo na kuwathibitishia ukweli huo kwamba nimeona kwa macho yangu, hazikua za dunia hii! Utadhani limefungwa goli la sekunde ya mwisho kabisa ya dakika ya mwisho ya nyongeza kuipatia timu nafasi ya kwenda kombe la dunia. Mama alifurahi sana, ndugu zangu wa tumbo moja walifurahi, ndugu wengine tuliokua tuna lelewa pamoja walifurahi sana sana na hata majirani waliosogea pale nyumbani asubuhi ile walikua wamefurahi. Kuna wakati nilipoinuka kutoka kitandani na kuchungulia nje nilikuta mtoto washangazi yangu na mtoto wa mama mdogo waliokua wamegombana na hawakua wakisemeshana hapo nyuma wakikumbatiana kwa bashasha na furaha kubwa. Niliguswa sana na hali ile kwakweli, ilikua ni furaha ya kweli furaha halisi furaha, furaha isiyosahaulika.
Baba nae aliporudi kutoka kazini alikua keshapata habari na sina maneno ya kuelezea jinsi alivyofurahi. Siku kadhaa baadae baba alipokea kutoka posta School Joining Instruction kutoka shule ya sekondari niliyopangiwa ambayo kwakweli Mkuu wa Shule ni kama alikua anaongea na mwanafunzi husika, tena mmoja mmoja. Mistari michache ya mwanzo ya barua hiyo ilisomeka hivi:
' Mwanafunzi Mpendwa,
Ninayofuraha kukuarifu kua umechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari.................. iliyopo mkoa wa..........Nakukaribisha kwa furaha huku nikitumaini kwamba unatambua bahati na fursa ya kipekee uliyoipata miongoni mwa vijana wenzako wa Kitanzania na kwamba utajifunza na kufanyakazi kwa bidii ili kutimiza matarajio yako na ya Taifa kwa ujumla.'
Sasa hivi wanafamilia tuliolelewa pamoja nyumbani tumekua na kila mtu ana maisha yake(japo kuna wachache pia walikwisha tangulia mbele ya haki). Kama binaadamu hua tuna tofautiana na wakati mwingine hutokea kukwaruzana na ugomvi serious kabisa. Lakini mara zote ikiwa mimi ni miongoni mwa wahusika kwenye ugomvi huo wa ndugu na hata kama mimi ndio nimekosewa basi hua naikumbuka sana siku ile ya Jumamosi ya December na jinsi ndugu zangu wote walivyofurahi pengine kuliko mimi mwenyewe, furaha ya kweli kwa ajili ya mafanikio yangu na kisha narudisha moyo nyuma nikisema kua damu ni nzito kuliko maji na mengine haya ni kazi tu ya shetani. Let's share our memories