Funguo ya gari imechomoka kwenye handle yake, msaada waungwana

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,107
Salam,
Ufunguo umechomoka kwenye handle yake baada ya handle kubomoka. Nimeshaunga na gundi lakini wapi.... Je, naweza kupata hiyo handle yenye remote ya namna hiyo?? Na je ni rahisi kubadilisha huo utumbo wa remote toka kwenye Hilo kava kwenda kava lingine??? Au ni nini kifanyike????

NB
Sijabandika kuonyesha kuwa ninamiliki gari, kwa hiyo watembea kwa miguu msilete mapovu yenu hapa.
 
Pole sana mimi nilihangaika sana kupata taa ya mazida Cx7 niliomba msaada huku kijana mmoja alijitahidi kutafuta alikosa mmoja akasema nenda Befoward Autoparts nikawapata wapo kariakoo ila niliingia google nikaagiza na ufunguo wa pili maana ulikuja mmoja sensor remote control ila unaagiziwa toka japan
 
tatizo ni gari aina gani?
Sio kila gari ni gari
 
Simple nunua remote nyingine kisha I program upya.
Lakini unatakiwa uwe ndani ya gari... Funguo yako unaiweka kwenye on position pale kwenye ignition.
Ukiletewa menu una reset then utakua tayari kutumia remote yako.
 
Simple nunua remote nyingine kisha I program upya.
Lakini unatakiwa uwe ndani ya gari... Funguo yako unaiweka kwenye on position pale kwenye ignition.
Ukiletewa menu una reset then utakua tayari kutumia remote yako.
Hiyo menu ya ufunguo inatokea au itaonekana wapi ?, kwenye display ya gari ?
 
Hiyo menu ya ufunguo inatokea au itaonekana wapi ?, kwenye display ya gari ?
Gari kama hiyo lazima imekuja na kama kitv fulani ambacho unatumia kama radio.
Sasa unacho fanya unaweka funguo then una Anza kufanya hiyo process ya kutoa funguo toka acc mpaka on position.
Unarudia hiyo action mpaka menu ya ku reprogram funguo itokee.
Hii ni njia ya short kati tu.
 
Wacha kujishtukia, kwani kunamtu amekuambia kwamba unagari?

Kuweka picha ya funguo mbovu kwani ndio kumilikigari, au unatutafuta maneno sisi watembea kwamiguu.
 
Sometime huku ukihitaji ushauri unaweza kukasirika ila ndo uhuru wa id fake ...najuwa wengi tunapenda sana remote lakn kwa tatzo lako ni dogo sana nenda kachongeshe funguo nyingine then ufunge pamoja na hyo remote so itakuwa remot kwaajil ya kufunga na kufungulia mlango ufunguo wa kuwashia gari
 
Pole sana Mkuu, kama uko Dar nenda kule Mtaa wa Lumumba, kaongee na wale vijana waouza mapambo ya magari watakuelekeza sehemu ya kuchonga funguo na sehemu ya utakayopata cover ya hiyo sensor kama bado ni nzima. Mimi cover ya sensor ilipasuka nikabadilisha. Ila ufunguo na sensor havitakuwa pamoja kama ilvyokuwa, unaweza kuziweka pamoja kwa kutumia ring. Kama unahitaji ufafanuzi zaidi, njoo inbox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…