APPROXIMATELY
JF-Expert Member
- Aug 10, 2021
- 2,035
- 2,712
Habari za muda huu ndugu wana Jamii Forums? Natumaini mnaendelea vyema na ujenzi wa taifa letu hili pendwa Tanzania, changamoto zipo ila cha msingi ni kuzishinda huku tukimtanguliza Mungu mbele.
Napenda kujikita kwa mada huska kama ifuatavyo,
Afya yako ni jambo la msingi sana. Afya yako kuwa nzuri haijalishi unakipato gani au hali yako ya kimaisha ipoje, kama wewe ni tajiri au masikini kinachohitajika ni wewe kulinda afya yako kwa gharama yeyote ile.
Ni kweli huwezi pinga makusidio ya Mwenyezi Mungu linapokuja swala la kuumwa, ila unaweza zuia magonjwa mengine kwa ulaji wako wa chakula na mazoezi.
Kuna pesa iliyojificha ndani ya afya za binadamu, laiti ukijua siri hii ninayokupa leo utajiri upo nauona ule pale, tena ni utajiri usio na shaka kabisa, hata Mwenyenzi Mungu anaubariki kabisa.
Mungu ametupa kila ufunguzi wa matatizo yote Duniani, hakuna lisilowezekana hapa Duniani, yote yanawezekana kabisa, ukifuata kanuni Mungu alizotupa sisi binadamu (anything is possible).
Siri yenyewe nakufungulia kama hivi;
Watu wengi wanahitaji kula chakula kinzuri tena kwa bei isiyokubwa sana, bei anayomudu mlaji, tena kula chakula kisafi kilichopikwa kwa usafi unaoridhisha machoni mwa binadamu na mdomoni anapokitafuna mlaji huska.
Kwanza ebu tuangalie huko mtaani, huko ambako vinatoka vyakula vya kila siku. Kweli hali ni mbaya sana, yaani watu wanaotutengenezea hivyo vyakula ni wachafu sana.
1. Wakaangaji wa samaki na kuku
Hawa watu ni wachafu tena siyo waaminifu hata kidogo, samaki wanakaanga na mafuta meusi yaliokaa zaidi ya week hata mbili. Kazi yao ni kuongezea mafuta mapya juu ya mafuta yale machafu.
Watu wanavumilia kula tu kwakuwa hawana njia nyingine ya kuwapata hao samaki wakiwa wamekaangwa tayari, labda hawana muda wa kukanga wenyewe. Ebu fikiria hii fursa kwa jicho la tofauti sana, kwa mtu anayenielewa kashatengeneza picha kichwani mwake.
Kama umenielewa hapa inahitaji akili za kuzaliwa, anza kukaanga hao samaki au kuku kwa usafi wa maana. Hapa zingatia yafuatayo;
A. Brand office yako, jitafutie jina nzuri kwa mfano uncle ma kuku, aunt masamaki n.k, tengeneza bango kubwa lililodizainiwa vinzuri, meza safi na viti vya wateja.
B. usafi
Hapa ndiyo panapohitajika sana, kuwa usafi, tena wa kimavazi na kwenye kazi yako. Hapa utawavuta wateja wengi sana.
C. Huduma nzuri
Hapa kwenye huduma nzuri, ongea na wateja wako vinzuri, daima usikorofishane na wateja wako kwenye masuala ya bei au kimaneno. Siyo mteja shabiki wa Simba halafu yeye Yanga unaanza kumsema, lazima atakukimbia.
Samaki au kuku wakilala sema ukweli hawa wamelala nimepunguza bei kidogo, mteja yeye ataamua kununua wapya au wajana.
2. wakaangaji wa chipsi
Hapa kuna hela nyingi sana, mjini watu wengi wanakula kiepe, tena wapigaji wa chipsi wanapika ovyo ovyo sana.
Wachafu sana, yale maji wanaoshea viazi ukiyaangalia kweli kama huna moyo hizo chipsi unaweza kuziacha kuzinunua.
Ukiwa na pesa yako wekeza kwenye hii biashara, zingatia utendaji kazi wako pia wafanyakazi wako. Hii biashara ukizingatia kweli unaweza piga shifting, maana unaweza jikuta ulali hata siku moja.
Locatio ya kutega ni vyuoni au maeneo yenye watu wengi na maduka mengi. Usafi, huduma nzuri na kujali wateja wako, mafuta yakilala yachuje kwa kitambaa kisafi. Usiwauzie hata siku moja ndaza, nina maana usiwauzie zilizolala.
Mzigo mwingine upo hapa, kama unaweza kuleta maziwa Dar es Salaam, yaani utapiga ela mpaka utashangaa. Ukiweza kuuza yakiwa fresh au mgando, tena yakiwa yameganda vyema kwa ustadi wa hali ya juu kuna ela nyingi sana. Watu wanaleta maziwa ila yana maji sana, yani maziwa ninayokunywa Moshi ni tofauti na maziwa ya Dar.
Hapa unaingia mzigoni mwenyewe, unafuata maziwa kwa mkulima unahakikishwa hauweki maji hata tone. Ukiyaleta town akienda kuyachemsha mteja na kukuta yanachemka mpaka yanamwagika, na ukiyaeeka kwenye kikombe juu yana siagi tena ya njano. Hapa utapiga pesa za watu mpaka utazikimbia, ishu inakuja kuyaleta town sasa.
Ukiwa na magari yaliyo na friji, ambayo utaweza kuyatoa hata mikoani, utakuwa umebuni bonge la biashara lisilo na ushindani. Hapa uwe na center ya watu kukutania na kuyanunua, uwe na magari yenye friji kubwa, uwe na vipimo vya kucheki maziwa kama yana maji au yameganda.
Biashara nyingine yenye pesa ndefu sana, hii biashara ya vyakula vya asili. Siyo siri town watu wanahitaji vyakula vyao vya asili, vilivyowalea toka wakiwa watoto.
Nakumbuka vyakula vya asili nilivyakuwa nakula zamani sasa kuvipata mpaka nirudi home mama anipikie. Muda mwingine natamani kula vyakula hivyo ila kuvipata huwezi, wanawake hawa tuliowaoa hawajui vyakula vya asili zaidi ya wali, ugali n.k.
Nakumbuka sana;
~ Kibulu
~ Ngararumu
~ Losholoo
~ Kitawa
~ Viberee
~ Machalali
~ Mtori
Hivyo ni baadhi ya vyakula, vipo vingi sana, kila tamaduni zinavyakula vyao. Unaonaje ukifungua sehemu ambayo wanauza vyakula vya asili? Hapa madhari, mpaka mavazi unayafanya ya asili ili kuvutia watu wengi.
Nakuhakikishia utapiga pesa mpaka utazikimbia. Tumechoka kula vyakula vya kisasa, Watanzania tubadilike sasa. Hii ni biashara ipo, ila siyo kama ninavyoiona inatakiwa iweje.
Kwa mjini ukizingatia usafi, huduma nzuri kwa wateja wako kuna pesa nyingi sana. Hakuna kitu kinaingiza pesa Duniani kama chakula. kama utafanya biashara za vyakula utapiga pesa tamu sana.
Uaminifu ni jambo lingine, Dunia ya sasa hakuna uaminifu tena, wafanyabiashara ni watenda dhambi sana, waongo na wezi sana. Biashara unanua kwa pesa yako ila bado unaibiwa, unamuamini mtu tena bado anakuibia!
Kwenye haya maisha ukizingatia uaminifu utatoboa tu. Daima usipende kumuibia mtu mali yake, Mungu huambariki mtu yule ambaye hapendi dhuluma na kuiba mali za watu.
Mungu atubariki kwenye kazi za mikono yetu. Mambo yanapoenda vibaya piga magoti mlilie yeye pekee, daima kumbuka Mungu ndiye muweza.
One time,
Once again,
Approximately.
To God,
To be glory.