Full time: Morocco 2-0 Tanzania | FIFA World Cup Qualification | Stade Municipal d’ Oujda | 26.03.2025

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
630
2,104
Usiku wa leo saa 6:30 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Morocco.

Ni mchezo wa aina yake kwani Morocco anaongoza kundi E akiwa na alama 12 huku Taifa Stars ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 6.

Je Taifa Stars itaondoka na alama 3 au ni Morocco?
Mchezo utakuwa live kupitia Azam Sports 1HD na DStv 227
================================================

1’ Mpira umeanza kwa Taifa Stars kuanzisha mtanange

3’ Morocco wanapata kona lakini kipa wa Stars wanaondosha hatari

4’ Stars wamekuja na mbinu ya kupoozesha mashambulizi huku muda mwingi wakiwa nyuma ya mpira

5’ Morocco wanaliandama lango la Stars kama ugomvi, wanapata kona nyingine

7’ Morocco 0-0 Tanzania

9’ Golikioa wa Stars yupo chini baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Morocco

10’ Stars bado wana uoga wa mechi na wameamua kuwaheshimu wenyeji wao, muda mwingi wapo nyuma ya mpira, bado ni 0-0

11’ Ally Salim Katoro anapasha wakati huu kipa namba akigangea na jopo la madaktari wa Stars

13’ Kipa amesimama sasa na mbungi inaendelea

15’ Morocco 0-0 Tanzania

17’ Tanzania bado tunacheza soka la kujihami muda mwingi hii ni hatari kwetu maana tunakaribisha mashambulizi zaidi

19’ Shomari Kapombe leo anageuzwa tu kama chapati hapa

20’ Kipa wa Stars japo ni mgeni kwenye mechi za kimataifa ila anajiimini vizuri na anacheza krosi kwa utulivu, ni hazina ya baadae

21’ Kikosi chote cha Stars kimerudi kukaba huku kikitegemea counter attack kwa Kibu na Msuva

22’ Mohamed Hussein anamchezea faulo Diaz nje ya box la Stars

23’ Morocco wanaenda kupiga faulo hiyo na mpigaji ni Diaz ila wanakosea na ukuta wa STARS unakaa uzuri

24’ Mohamed Hussein anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Mazroui

25’ Morocco wanapiga faulo lakini mabeki wa Stars wanaokoa hatari langoni mwao

25’ Morocco 0-0 Tanzania

28’ Morocco licha ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ya mchezo wanashindwa kuifungua beki ya Stars

29’ Golikipa wa Stars yupo chini tena akigangwa huku mchezo ukiwa umesimama, kwa mujibu wa sheria za soka, kipa ana dakika 6 za kutibiwa kabla ya kufanyiwa sub uwanjani

30’ Mtanange unaendelea kipa amekwashasimama

31’ Wachezaji wa Stars muda mwingi wa mchezo wanacheza faulo za hapa na pale

32’ Offside kwa Kibu Denis Prosper

33’ Mashabiki wa Morocco wameanza kuhanikiza ili timu yao ipate goli

35’ Morocco 0-0 Tanzania

37’ Msuva anapiga shuti lakini anashindwa kulenga lango

39’ Kibu yupo chini amefanyiwa madhambi na wachezaji wa Morocco

40’ Morocco 0-0 Tanzania

41’ Feitoto anapata nafasi ya wazi lakini mkeaju aliopiga unaenda nje

43’ Umiliki wa mpira Morocco 78% na Tanzania ni 22%

45’ Zinaongezwa dakika 4 ili kufidia muda uliopotea

45’ + 01 Amrabat wa Morocco anapiga shuti lakini linapaa, iankuwa salama kwa Stars

HT’ Morocco 0-0 Tanzania

46’ Morocco wanaanza mpira kuashiria kipindi cha pili kimeanza

47’ Morocco wameanza kwa kasi na washafika langoni mwa Stars

51’ Morocco wanapata goli kupitia beki wao Aguerd anayekipiga Real Sociedad

53’ Morocco wanashambulia lango la Stars mfululizo

54’ Amrabat anawekwa chini na Feitoto

55’ Morocco wanapata penati baada ya Iba Bacca kuunawa mpira ndani ya box

58’ Brahm Diaz anaweka goli la pili kwa Morocco kwa mkwaju wa Penati

59’ Mlima wa matokeo ushakuwa mkubwa kwa Taifa Stars

60’ Morocco 2-0 Tanzania

62’ Goli la tatu la Morocco linakataliwa mfungaji ameotea

63’ Mchezaji wa Tanzania ambaye walau ameonyesha uwezo leo mpaka sasa ni Fei toto

64’ Shuti lililopigwa na Mzize linafakwa kirahisi na Bono

70’ Taifa Stars wanafanya sub tatu, Mzize, Mudathir na Mohamed Hussein wanatoka, nafasi zao zinachukuliwa na Yusuph Kagoma, Charles M’mombwa na Pascal Msindo

72’ Taifa Stars wanakosa nafasi baada ya shuti la Kibu kupanguliwa uzuri na golikipa Bono na kushindwa kutumia rebound vizuri

74’ Ball Possession Morocco 77% kwa Tanzania 23%

76’ Msuva anapaisha shuti lake baada ya kumegewa nafasi nzuri na mwenzake

80’ Morocco 2-0 Tanzania

82’ Msuva anatoka na nafasi yake kuchukuliwa naa Selemani Mwalimu

85’ Morocco 2-0 Tanzania

87’ Morocco wanaliandama goli la Stars kama wanatudai vile

88’ Mpaka sasa Taifa Stars imepuga shuti moja tu lililolenga lango

90’ Kutakuwa na dakika 4 za nyongeza

90+01’ Feitoto anapiga shuti lakini anapaisha

90+02’ Kibu anatoka nafasi yake anaingia Haji Mnoga

FT’ Morocco 2-0 Tanzania
 

Attachments

  • Screenshot 2025-03-26 005233.png
    Screenshot 2025-03-26 005233.png
    189.1 KB · Views: 2
Usiku wa leo saa 6:30 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Morocco.

Ni mchezo wa aina yake kwani Morocco anaongoza kundi E akiwa na alama 12 huku Taifa Stars ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 6.

Je Taifa Stars itaondoka na alama 3 au ni Morocco?
Mchezo utakuwa live kupitia Azam Sports 1HD na DStv 227
vip cc wa startimes ni chanel gani
 
Usiku wa leo saa 6:30 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Morocco.

Ni mchezo wa aina yake kwani Morocco anaongoza kundi E akiwa na alama 12 huku Taifa Stars ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 6.

Je Taifa Stars itaondoka na alama 3 au ni Morocco?
Mchezo utakuwa live kupitia Azam Sports 1HD na DStv 227
kwahiyo kumbe wanacheza kesho
 
Hivi utashangaa kuna watu watakesha mpaka usiku wa manane kuangalia mechi ambayo matokeo yake tayari yanajulikana! Imagine hiyo timu ya Karia na ccm, imefungwa 3-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani! Sasa huko ugenini si itafungwa goli 7-0!

Kocha mwenyewe sasa wa hiyo timu! CV yake inaonesha amewahi kufundisha Mlandege Fc, Mchambawima Fc, Namungo Fc, Coastal Union Fc, Urojo Fc!! Not serious at all.
 
Back
Top Bottom