FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,170
5,525
1699126629552.png

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, tarehe 05.11.2023 iliyokuwa ikisubiriwa na Watanzania wengi imewadia. Siku ambayo wapenzi wa soka watashuhudia Derby ya Kariakoo, miongoni mwa Derby bora kati ya zile zinazoheshimika barano Afrika.

Mechi hii itaanza muda wa saa 11:00Jioni.

Kaa nami katika uzi huu upate kushuhudia matukio mbalimbali
F-LERgQWgAAcI6R.jpeg

Kikosi cha Simba
F-LENGTW0AArpe9.jpeg

Kikosi cha Yanga
Timu zinaingia uwanjani, mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa
Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Mkapa
2' Timu zinasomana, pasi za hapa na pale

3' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kennedy Musonda anaifungia Yanga goli kwa kichwa huru, akiwa katikati ya walinzi wa Simba
7’ Dickson Job anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Saido
8’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga goli kwa kichwa akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Saido
13' Timu zote zinaonekana kuwa na presha ndani na nje ya uwanja
22’ Fabrice Ngoma anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Azizi Ki
30’ Yanga wanamiliki pira muda mwingi
40’ Simba wanaonesha uhai na kujipanga
43’ Shambulizi kali langoni kwa Yanga, mpira wa Kapombe aliopiga kapombe unaokolewa
45' Simba wanafanya shambulizi lingine kali lakini Yanga wanaokoa

MAPUMZIKO
1699198211449.png

Kipindi cha pili kimeanza
57’ Kipa wa Yanga anamchezea faulo Kibu Denis
59’ Kibu anashindwa kurejea uwanjani, nafasi yake inachuliwa na Luis
64’ GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Maxi Nzengeli anafunga goli la pili kwa Yanga, akipiga shuti kali
Baleke anatoka anaingia Moses Phiri
72’ Musonda ametoka ameingia Clement Mzize
73’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Azizi Ki anafunga goli la tatu kwa Yanga, ikiwa ni goli lake la 7 katika Ligi Kuu 2023/24
77' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Max anafunga goli la nne kwa Yanga
87' Penati, Yanga wanapata
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Pacome Zouzoua anafunga kwa kumchambua Manula
90' Zinaongezwa dakika 3

FULL TIME
 
Joto linazidi kupanda kuelekea game ya watani wa Jadi, Simba vs Yanga hapo kesho 05 Nov 2023

Ukiwa kama shabiki wa soka bila kuangalia mapenzi ya timu yako weka ubashiri wako ni kwa namna gani unaiona game hiyo inaisha hapo kesho.

Je, ni Simba yenye kikosi bora kabisa chini ya Master Robertinho kupata matokeo au Yanga chini ya Miguel Gamondi?

Wengi wanasema hizi game hazitabiriki lakini nataka tuone ni wana JF wangapi wanaweza kuipatia matokeo ya hii game kwa 100% (Correct score)

NB: Ubashiri ubase kwenye uhalisia wa vikosi na ubora wa timu shindani na si ushabiki/mapenzi ya timu yako
FB_IMG_1699134930016.jpg
FB_IMG_1699135007790.jpg
FB_IMG_1699135152460.jpg
 
Back
Top Bottom