Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania NBC Premier League kuendelea kupigwa leo Mei 11, 2022 ambapo Simba SC wanapambana na Kagera Sugar kwenye Dimba la Benjamin Mkapa
Mchezo unatarajiwa kuwa mkali hasa baada ya Kagera Sugar kuchukua alama tatu mbele ya Simba SC kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, hivyo mchezo wa leo ni kama wa kulipa kisasi kwa Simba SC, vile vile mchezo huu watatumia kuendelea kuweka Presha kwa kinara wa Ligi Kuu.
Kocha wa Simba SC Pablo Franco amesema kuwa, watakuja na mbinu tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.
"Utakuwa mchezo mgumu lakini tunakwenda kucheza tofauti kabisa na tulivyocheza kule Kagera"alisema Pablo
Naye Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Buherwa B, amesema kuwa wachezaji wake wapo sawa hakuna majeruhi yeyote, kwahivyo hawana namna yoyote ile zaidi ya kuhitaji alama tatu.
"Tunatambua ukubwa wa Simba lakini hakuna namna yoyote, tunahitaji alama tatu muhimu kwetu" alisema Buherwa
Nani kuibuka na ushindi? Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.. Usikose Ukaambiwa
Kulipewa Mwana...Kulitaka Mwana
=============
Mpira umeanza uwanja wa Mkapa, dakika 90 za jasho na damu kusaka alama tatu
Simba SC 0-0 Kagera Sugar
05' Timu zote zinacheza kwa utulivu hasa eneo la kati, Simba wakijaribu kutafuta mpenyezo nyuma ya mabeki wa Kagera huku Kagera wakijibu shambulizi moja
Mfuko anamuweka chini Kibu, ni free kick kuelekea Kagera, inapigwa kulee wanaokoa.
13' Kibu Goooooooooooooaaal gooal
Kibu Denis anaipatia Simba SC bao la kwanza, akitumia nafasi ya Krosi ya Bwalya | Simba SC 1-0 Kagera Sugar
15' Simba wanashambulia lango la Kagera Sugar kama nyuki, almanusura wapinge bao la pili baada piga nikupige kuokolewa.
Kagera Sugar wanapata Kona, inapigwa kulee, lakini ni Offside Luhende
19' Simba wanashindwa kutumia nafasi ya mpira wa Krosi uliopigwa na Kibu
23' Bocco anaweka kambani mpira lakini, Kibedera kipo juu kuashiria kabla ya kufunga alikuwa ameotea..!
Kipama anatoa mpira nje na kuwa Kona, inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa piga tena wanaokoa
Abdallah mfuko yupo nje akipatiwa matibabu baada ya kuumia
Kweke Kiizaa, inapigwa kulee Nje, ilikuwa nafasi ya kufunga kwa Kagera Sugar
30' Bocco Goooooooooooooaaal gooal
John Bocco anaipatia Simba SC bao la pili kwa shuti kali, akipokea pasi murua kutoka kwa Bwalya| Simba SC 2-0 Kagera Sugar
Haya kagera sugar wapo nyuma wakipiga pasi za hapa na pale, wanajaribu kutafuta mpenyezo kwa Simba
35' Imetokea Shambulizi kali kuelekea Kagera, lakini Sakho na Bocco, Bwalya wanashindwa kutumia nafasi ya Krosi ya Kibu
37' Goo laaaaaa ni Offside, kwa John Bocco, kibendera kipo juu
Safu ya mbele ya Kagera Sugar inakosa mbinu ya kupenya ulinzi mkali wa mabeki wa Simba | Simba SC 2-0 Kagera Sugar
Kocha Francis Baraza anapanga vizuri Kikosi chake, Kumbuka wapo nyuma ya mabao mawili kwa bila
45+2' Kuelekea kuwa mapumziko
Kapombe anakwenda, anaangushwa ndani ya box na mabeki wa Kagera Sugar, lakini refa anakataa, anasema hapana.
Kagera wanapiga mbele huku, Simba wanakaa imara, haya mpira upo katikati ya Uwanja
Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka mbele ya mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar
HT: Simba SC 2-0 Kagera Sugar
Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili
47' Simba wanawavuta Kagera, Materema anafanya faulo kwa Onyango mpira unapigwa kuelekea Kagera
50' Kibu anapiga shutii... Loooooooo almanusura wapinge bao la tatu hapa Kagera Sugar, shuti linaokolewa na golikipa
Mpira upo lango la Simba SC lakini Kiza amedhibitiwa vilivyo hakuna nafasi ya kupenya kabisa.
54' Ametoka Kiiza na ameingia Yusuf mbaraka, na ametoka Nassoro na ameingia Mwijage upande wa Kagera Sugar
55' Free Kick inapigwa kuelekea Kagera Sugar, lakini inababatiza ukuta wa Kagera
56' Mzamiru anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Kagera Sugar, huku Shambulizi la kagera sugar likidakwa na Manula
61' Kona inapigwa kuelekea Simba lakini Wawa anarukaaaa na kuokoa hatari ile
62' Mwijage anapiga shutii kwa mbali lakini linapaa nje ya lango la Simba SC, wanajaribu kupiga kutoka mbali
Sakho anapiga Krosi, lakini inapotea baada ya Mzamiru kuwa mbali na lango
66' Mbaraka Yusuf, yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha.
68' Ametoka Bocco na Kibu na nafasi zao zimechukuliwa na Banda na Kagere upande wa Simba SC
75' Shuti la Peter Banda linagonga nyavu ndogo kwa nje, ilikuwa nafasi kwa Simba, salama kwa Kagera
79' Ametoka Sakho na ameingia Mhilu upande wa Simba SC, golikipa wa Kagera Sugar kwake Mwijage anapiga shutii Ooooh njeee
Kagera wanajenga mashambulizi lango la Simba, lakini Wawa na Onyango wanakaa imara kuona hakuna hatari yoyote
85' Matumaini ya Kagera Sugar kupata bao yanazidi kufifia, Walinzi wa Simba wapo imara
Wanashambulia lango Kagera wakijibu kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa Simba, ngoja Tuone itakuwaje
90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu
Ametoka Wawa na Henock na wameingia Kennedy na Israel upande wa Simba SC
Mhilu upande wa kulia anapiga Krosi lakini golikipa wa Kagera anadaka bila wasiwasi
Kagera wanapata Kona, haya ngoja tuone, inapigwa kulee lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick
Unapigwa kuelekea mbele kuleee
Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar
FT: Simba SC 2-0 Kagera Sugar
........ Ghazwat.....