FT: Ligi Kuu: Yanga S.C 2-0 Namungo F.C: Uwanja wa Mkapa, 04/02/2023

mzee wa bwaksi

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,253
3,968
Wale mabingwa Kwa kutandaza soka safi, soka maridadi soka lenye ladha ya asali hapa nawazungumzia Young Africans jioni ya leo majira ya 12:30 watashuka katika dimba la Benjamin Mkapa kumenyana na Namungo F.C. katika mwendelezo wa ligi kuu ya Nbc

Ikumbekwe katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dec 7 mwaka jana pale katika dimba la Kassim Majaliwa mkoani Lindi, Namungo walinyonyolewa bao 2-0 na Yanga. Hivyo Leo wataingia wakiwa na kiu ya kulipa kisasi cha kufungwa mechi ya duru ya kwanza.
Kwa upande wao Yanga ushindi ni muhimu sana kwao ili kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi na kuusogerea ubingwa ambao wanayo nafasi kubwa ya kuutetea.

Timu zote zimejiandaa vema na mchezo huu na macho na masikio yote yataelekezwa uwanjani hapo Lupaso saa 12.30 jioni ya Leo

Usiwe mbali na Uzi huu kwani utakipata kile kitachojili uwanjani,...................

Timu zote ndio zinaingia uwanjani ambapo Yanga wamevalia jezi Yao pendwa jezi ya bahati rangi Nyeusi huku Namungo F.C wakivalia jezi zao rangi ya Dhahabu

00" Kipyenga kimepulizwa tayari kuashiria kuanza Kwa mpambano huu


02" Yanga wameanza Kwa Kasi kupeleka mashambulizi langoni mwa Namungo ambapo krosi ya Djuma Shaban inaondolewa na kuwa Kona ambayo hata hivyo haijazaa bao

07" Faulo inapigwa na yule yule mkali Aziz K eneo zuri lakini shuti lake linaenda nje

18" Bado milango migumu kwa timu zote

22" Aziz kiii shuti lake linaenda nje ya lango la Namungo

27" Kichuya anapiga shuti mtoto inakuwa chakula Kwa mdaka mishale

40" Mayele kwenye nafasi nzuri yakuiandikia bao Yanga ila anapiga shuti juuu

44" Kona inapigwa na Djuma shaban kuelekea lango la Namungo
Gooool Dickson Job anaruka juu na kupiga kichwa mpira kuiandikia Yanga goli la kwanza

45+2" Mpira ni mapumziko Yanga wanakwenda vyumbani wakiwa mbele kwa goli Moja. Tutarejea kipindi cha pili

Kipindi cha pili kimeanza hapa Lupaso

50" Aziz kiii anaweka goli la pili Kwa Yanga baada ya makosa ya kolikipa wa Namungo
Yanga 2-0 Namungo

60" Aziz nusura aiandikie Yanga goli la tatu pale. What a player

70" Mayeleeeee anokoa pale Deogratius Munishi na kuwa Kona ambayo haikuzaa matunda. Wananchi wanang'ara hapa Lupaso

80" anatoka Aziz anaingia Zawadi Mauya, pia anatoka Jesus Moloko anaingia Dickson Ambundo. Bado ubao unasoma 2-0

85"Musondaaaaa..... Mayeleeeee wanateseka sana Namungo hapa kwa Mkapa

90" Mayeleeeee oooh lalahha mpira unakwenda nje..... Almanusura pale Mayele aiandikie Yanga goli la 3

90+3" Yanga bado inaliandama lango la Namungo japo muda umeenda na refarii anaangalia saa yake.

Na mpira umekwisha huku vinara Yanga wakizidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa ushindi wa magoli 2-0. Tukutane wakati mwingine


View attachment 2506200View attachment 2506201
 
Mwenendo wa mchezo hapa kibanda umiza ......

Anapigwa mwingine........makolo jasho linawatoka
1674412603260.jpg
 
Team Imepoteana Bado Wanahaha Na Mkataba Wa Kifuani Sijui Mwisho Wao Ni Upi
 
Back
Top Bottom