FT: Argentina 3-3 (4-2 Penalties) France - World Cup Final - December 18, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Wachezaji wa Ufaransa waliokosa penati ni Kingsley Junior Coman na Aurélien Djani Tchouaméni.

Baada ya dakika 90 kukamilika matokeo yakiwa 2-2, zikaongezwa dakika 30 matokeo yakawa 3-3, ndipo ikaamuliwa zipigwe penati na Argentina kushinda kwa matuta 4-2

Muda wa penati

Mwamuzi anakamilisha dakika 30

120' Zinaongezwa dakika 3
Mbappé anasawazisha kwa Ufaransa
117' GOOOOOOOOOOOOO
Ufaransa wanapata penati
Messi anafunga goli la tatu baada ya kazi nzuri ya Martinez
108' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mchezo unaendelea

105' Kipindi cha kwanza cha dakika 30 kimekamilika
104' Argentina wanakosa nafasi mbili za wazi
97' Presha inaongezeka kwa timu zote
95' Timu zote zinachukua tahadhari kila zinapopoteza mpira
Mchezo umeanza

Sasa zinaongezwa dakika 30

90+8' Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha dakika 90
90+1' Presha imegeuka na kuwa kubwa kwa Argentina
90' Zinaongezwa dakika 8 za nyongeza
80' Kylian Mbappé anaongeza goli la pili kwa Ufaransa
Kylian Mbappé anafunga
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
78' Ufaransa wanapata penati
77' Mashambuliaji ya kupokezana kwa zamu

FkRe39IXkAA9eXE.jpg
Kipindi cha pili Didier Deschamps akafika kwenye benchi akiwa na bandeji kwenye kidole, nini kilitokea vyumbani?
FkRe37sX0AEtEsN.jpg

Kipindi cha kwanza kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps hakuwa na bandeji kwenye kidole chake

64’ Marcos Acuna anaingia kuchukua nafasi ya mfungaji wa goli la pili, Angel di Maria
62' Argentina shambulizi kali lakini kipa wa Ufaransa anaokoa
56' Kasi ya mchezo imepungua kiasi
50' Ufaransa wakajipanga taratibu
47' Argentina wanaaza kwa presha kubwa ileile
Kipindi cha pili kimeanza

Messi anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika Hatua ya Makundi, 16 Bora, Robo Fainali, Nusu Fainali na Fainali katika michuano ya wakati mmoja

MAPUMZIKO

45' Zinaongezwa dakika 7 za nyongeza

Kumbuka kuwa Ángel Di María ameshawahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi katika Fainali ya Champions League na Copa América

40' Ufaransa wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili
36' Di Maria anaipatia Argentina goli la pili
30' Presha ni kubwa kwa Ufaransa kwa
22' Lionel Messi anaipatia Argentina bao la kwanza akimhamisha kipa wa Ufaransa
21' Argentina wanapata penati
16' Di Maria anapata nafasi nzuri, shuti lake linapaa juu

Nikukumbushe tu Messi na Mbappé kila mmoja amefunga magoli Matano katika michuano hii.
Messi ana asisti 4, Mbappé ana asisti 3


14' Ufaransa wamefika langoni mwa wapinzani na sekunde chache baadaye Argentina wakajibu mapigo
10' Antoine Griezmann ameshacheza tackles mara mbili licha ya kuwa yeye ni kiungo mshambuliaji
7' Ufaransa wanaongeza umakini kadiri muda unavyosogea mbele
5' Argentina wameanza kwa kumiliki mpira na kufanya mashambulizi makubwa mawili
3' Presha ni kubwa kwa wachezaji wa timu zote
Mchezo umeanza

France.png

Kikosi cha Ufaransa

Argentina.png

Kikosi cha Argentina

Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi na mbili kamili jioni ya leo.

Ufaransa wakishinda wanaweka historia
Kama wakishinda itakuwa timu ya kwanza baada ya Brazil mwaka 1962 kutetea taji la Kombe la Dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom