Freeman Mbowe: Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
219
541
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, anatarajiwa kutoa tamko la chama hicho juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania. Viongozi na Wafuasi wa chama hicho wanajadili kwa kina mstakabali wa CHADEMA, kwa kuzingatia hali ya kisiasa na changamoto wanazokabiliana nazo.

Updates..........
Tundu Lissu

Lissu amesema kwa sasa ni wakati muafaka kwa viongozi, wanachama na wananchi wote kwa ujumla wake kufanya maamuzi magumu kwa kuwa huko mbele mambo yatakuwa mabaya zaidi huko mbele endapo hatua stahiki hazitachukuliwa

Matukio hayo ni pamoja na matukio ya utekaji, mauwaji nk

Freeman Mbowe

Ameyataja maazimio ya

Kwa Muujibu wa katiba ya chama chetu ndiyo inamajukumu ya mwisho ya kiutendaji kwa ngazi ya matukio ya Kitaifa.

Kwa misingi hiyo basi imeamulika kamati kuu ya chama chetu iitwe ikae kwenye kikao maalumu tarehe 16 na 17 septembar ambao ni jumatatu na jumanne ya wiki ijayo. Kujadili na mambo mingine muhimu kujadili swala la utekaji, mauwaji, kupotea kwa viongozi wetu na gilimba mbalimbali ambazo tumekuwa tukifanyiwa na Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Ili yale yote hatimaye tunayohamua katika mkutano huu yakapate huhalali wa kikatiba, kikanuni na kiutendaji.

La pili vikao vyote vimetambua kwamba pamoja na kumaliza kumzika mzee wetu Ali Kibao, bado tunaviongozi wetu muhimu ambao hadi sasa hivi hatujui wamewapeleka wapi.

Kwa makusudi kabisa na itifaki ndani ya chama chetu. Vikao vyote vimetambua kwamba Ndugu yetu Jacob Mlai Katibu wa Chama wa Wilaya ya Temeke aliyetekwa na wezake hadi leo hatujui alipo.

Deoniz Kipanya Katibu Mwenezi wa chama chetu jimbo la Sumbawanga Mjini na yeye ni zaidi ya wiki tano hatujui wamempeleka wapi, kijana wetu Deusdedith Soka, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA wilaya ya Temeke naye hatunaye miongoni mwetu na hawajatuambia wamewapeleka wapi, Kombo Mbwana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa wilaya ya Handeni ambaye walimteka, wakamtesa, wakamtweza na huyu alikamatwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi wakishirikiana na Polisi, na baada ya muda wa wiki takribani sita ndiyo wakasema wanaye, wamempeleka mahakamani kwa makosa ambayo yana dhamana lakini eti wamefuta dhamana na Mahakama imekubali wafute dhamana! Bado wamemuweka rumande.

Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho, na kwa sababu wao wamekataa kulifikisha mwisho, sisi tutawalazimisha walifikishe mwisho. Ili tufanikiwe hili, ndugu zangu Wanachadema tunahitaji kuwa kitu kimoja, kila mmoja wetu anapaswa kuwa bega la kulillia mwenzake, 'a crying shoulder to any of us', na tukubaliane kwamba kila tone la damu ya mwanachadema inayopotea tutaitetea kwa nguvu kubwa bila kuogopa

1.Tunaipa Serikali mpaka siku ya jumamosi ya tarehe 21 ya mwezi huu wa tisa watueleze watoto wetu, wanachama wetu na viongozi wetu niliwataja hapa wako wapi? na watuambie wawalejeshe wakiwa salama kama awawaleshi wakiwa salama waturejeshe wakiwa mauti kama awawezi kuturejeshe kwenye umauti watuambie wamekwenda kuwatupa wapi? au kuwapotezea wapia?

2.
Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?

Sasa baada ya mashauriano ya viongozi wa ngazi zote hizi, tumekubaliana, watu pekee ambao tuna imani wanaweza kuja kufanya uchunguzi wa haki katika nchi yetu, iwe lazima ni chombo cha kimataifa cha uchunguzi, na kipekee tumependekeza chombo kinachoitwa Scotland Yard kutoka jeshi la polisi la Uingereza kuja kufanya uchunguzi huu.

Tutaanza na kampeni ya Samia Must Go ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji kwenye matukio ya utekaji.

Mbowe pia ametoa rai kwa viongozi wa CHADEMA siku 12 kuanzia sasa kuja Dar kwaajili ya kupeana mikakati muhimu kwa hatua zaidi.

Soma Pia:

View: https://www.youtube.com/watch?v=5zHswMJROiI
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, anatarajiwa kutoa tamko la chama hicho juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania. Viongozi na Wafuasi wa chama hicho wanajadili kwa kina mstakabali wa CHADEMA, kwa kuzingatia hali ya kisiasa na changamoto wanazokabiliana nazo.

View: https://www.youtube.com/watch?v=5zHswMJROiI

Kwa kiasi fulani mtu huyu atakuwa amewapunguzia ushawishi wake baadhi ya wafuasi wake kutokana na misimamo yake ya legelege dhidi ya uovu wanaotendewa wafuasi wake.
 
Kwa kiasi fulani mtu huyu atakuwa amewapunguzia ushawishi wake baadhi ya wafuasi wake kutokana na misimamo yake ya legelege dhidi ya uovu wanaotendewa wafuasi wake.
Yaani kama mimi sina imani kabisa na Mbowe kwenye haya mapambano. Ni mtu anayejaribu kutaka asifiwe na wapinzani, na wakati huohuo na serekali eti anafanyanya siasa za kistaarabu. Cdm wajue Mbowe anawapoteza.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, anatarajiwa kutoa tamko la chama hicho juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania. Viongozi na Wafuasi wa chama hicho wanajadili kwa kina mstakabali wa CHADEMA, kwa kuzingatia hali ya kisiasa na changamoto wanazokabiliana nazo.

View: https://www.youtube.com/watch?v=5zHswMJROiI

Hayo matamko mzee wetu watekaji wameshayazoea😀
 
Back
Top Bottom