Freeman Mbowe: Scotland Yard ya Uingereza ichunguze Matukio ya Utekaji na Uuaji nchini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,170
5,526

"Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?"

"Sasa baada ya mashauriano ya viongozi wa ngazi zote hizi, tumekubaliana, watu pekee ambao tuna imani wanaweza kuja kufanya uchunguzi wa haki katika nchi yetu, iwe lazima ni chombo cha kimataifa cha uchunguzi, na kipekee tumependekeza chombo kinachoitwa Scotland Yard kutoka jeshi la polisi la Uingereza kuja kufanya uchunguzi huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Septemba 11, 2024 Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

PIA SOMA
- News Alert: - Freeman Mbowe: Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho
 
Hakuna lisilowezekana naamini, jambo la kufanya ni kuwalazimisha serikali mpaka wafanye kile wananchi wanataka.

Kutangazwa ni hatua ya kwanza, kitachofuata ili kulazimisha utekelezaji wa hilo ndio muhimu zaidi.

Mkumbuke haya mambo hayaji tu kama kupokea mkate kwenye sahani, lazima yapiganiwe, mkiitwa muitike, sio kulalamika tu hapa JF.
 
Wafanye na uchunguzi wa kwa nini yeye ana uenyekiti wa kifalme miaka nenda rudi yeye ni mwenyekiti
 
Jamani watanzania hali ni mbaya sana.
Msitu umeshakauka bado njiti moja tu ya moto msitu unawaka.

Kiongozi mwenye hekima anathamini sana uhai wa wananchi wake.

damu za watu wasio na hatia mnazozimwaga zinathamani kubwa kuliko vyeo.

Kuna mmoja aliondoka kwa tabia kama hizihizi ila kwa kipindi hichi mmezidi..

Cheo utakipata na kitaondoka tu, kama uliua, ulitesa elewa utaishi maisha ya majuto huku ukipata mateso makali sana.

Munao waua tambueni wanawake zao, watoto na uzao wao. Vipi mnajali kuhusu wao? Wengine wanashindwa hata kujua mmewazika wapi? Aisee Hapana! Hapana!!!

Kama tunavyopigania kutokomeza magonjwa, ajali, na majanga mengine ili tu KULINDA UHAI tulionao leo hii mtu anachinjwa na kuchunwa kama kuku? Kweli? Hii ni BIG NO.

MUNGU ULIYE JUU! JUKUMU LA KUTOA UHAI NI LAKO! HIKI KINACHOTOKEA TUNAOMBA SANA UJIDHILISHE KWA WATU HAWA. HUJAWAHI KUSHINDWA NA SHETANI.

Sio mbali sana Matoke yanakuja itakuwa ni fadhaha kwa utawala huu. Waliopewa uhai na neema ya kutulinda leo wamegeuka kuwa Miungu watu wanachagua nani aishi nani afe. NO!!!! Mungu sio John.

NB: damu ya mwenye haki mmoja inatosha kuangusha utawala wa kidhalimu.
 
"Tumekaa kama viongozi tumeshauriana kwa kina, kama kweli tume ya kimahakama ya kijaji, kwa mazingira ya nchi yetu ilivyo, kwa namna tulivyoliona bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapuuza utekaji, kwa namna ambavyo tumeiona mahakama kuu inapuuzs utekaji, hivi kweli hiyo rai ya kumtaka Rais aunde tume huru ya kimahakama na watu wenyewe ni haohao wa mifumo tutakuwa salama?"

"Sasa baada ya mashauriano ya viongozi wa ngazi zote hizi, tumekubaliana, watu pekee ambao tuna imani wanaweza kuja kufanya uchunguzi wa haki katika nchi yetu, iwe lazima ni chombo cha kimataifa cha uchunguzi, na kipekee tumependekeza chombo kinachoitwa Scotland Yard kutoka jeshi la polisi la Uingereza kuja kufanya uchunguzi huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Septemba 11, 2024 Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

PIA SOMA
- News Alert: - Freeman Mbowe: Vikao vya CHADEMA vimesema 'This Must Come to an End', lazima jambo hili lifike mwisho
hakuna haja,
na wala hakuna sababu hata moja kufikia hatua hiyo ya aibu kwa hisia potofu tu za kisiasa kutoka kwa wanasiasa wa upinzani waliofilisika hoja, dhidi kwa taasisi imara na kisasa sana za ulinzi Tanzania na zinazo aminika zaidi mataifa mbalimbali duniani na ulimwengu mzima...

hakuna taifa la lolote la ng'ambo linaloweza kukubali kuhadaiwa na mihemko ya mtua aliekosa uhalali wa uongozi na king"ang'anizi kwa kubadili katiba ndani ya taasisi yake binafsi anayoingoza ili abaki madarakani,

lakini pia hakuna Taifa ambalo linaweza kupoteza muda kumskiliza na kumuamini mtu ambae, kwa masamaha wa raisi alisamehewa uhalifu wa kigaidi :pulpTRAVOLTA:
 
Sometimes wapinzani hua wanaongea vitu havimake sense.

Ni taifa gani sovereignty linaalika nchi nyingine kufanya uchunguzi kwenye nchi yake?

Scotland yard wakisema wahusika ni mtu huyu, nani anatakiwa kumuwajibisha huyo mtu? Scotland yard au mahakama za Tanzania?

Hii drama waliwahi kuiraise muda fulani ikafifia naona wameanza nayo upya
 
Hakuna lisilowezekana naamini, jambo la kufanya ni kuwalazimisha serikali mpaka wafanye kile wananchi wanataka.

Kutangazwa ni hatua ya kwanza, kitachofuata ili kulazimisha utekelezaji wa hilo ndio muhimu zaidi.

Mkumbuke haya mambo hayaji tu kama kupokea mkate kwenye sahani, lazima yapiganiwe, mkiitwa muitike, sio kulalamika tu hapa JF.
Kile wananchi wanataka au Chadema wanataka?
 
Hakuna lisilowezekana naamini, jambo la kufanya ni kuwalazimisha serikali mpaka wafanye kile wananchi wanataka.

Kutangazwa ni hatua ya kwanza, kitachofuata ili kulazimisha utekelezaji wa hilo ndio muhimu zaidi.

Mkumbuke haya mambo hayaji tu kama kupokea mkate kwenye sahani, lazima yapiganiwe, mkiitwa muitike, sio kulalamika tu hapa JF.
Wa Tz bado sana, hatuna uthubutu.
Wananchi waoga, viongozi waoga.
Ngoja tuisome namba kwanza, yakitufika shingoni tutachukua hatua.
 
Back
Top Bottom