Freeman Mbowe ni nahodha mwaminifu ambaye meli yake itatia nanga Januari 21

OPEN the Door

Senior Member
Nov 15, 2024
170
84
Freeman Aikaeli Mbowe, aka Saluti ya Zege, kwa wanasiasa wengine amekuwa mwalimu na mkufunzi wa siasa za Bongo.

Kati ya wanasiasa wengi, nadhani watamkumbuka kwa mafundisho yake. Aliwafunza wengine namna ya kuongoza.

Maneno yake, nanukuu: "Nimeongoza chama hiki kwa muda mrefu kwa josho na damu, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni."

Kweli aliwafundisha siasa wanasiasa vijana hadi chama tawala kikawaona na kuwapangia kazi, kama ukuu wa wilaya.

Huyu, FAM, namfananisha na nahodha mwaminifu ambaye ameonyesha namna ya kuendesha siasa za kidemokrasia.

Meli yake itatia nanga mnamo tarehe 21/01/2025. Bila shaka, uchaguzi ukiwa wa haki na uwazi, atakubaliana na matokeo, lakini hawa wagombea wengine nao watakubali matokeo.

Pia, nawashauri wanachama wa Chadema wasithubutu kubomoa chama kwa kuhama baada ya mshindi kupatikana. Mimi si mwanachama wa Chadema, ila napenda siasa za ushindani. Tanzania kwanza.
 
IMG-20250116-WA0060.jpg
 
Huyu Mwamba hakushiriki mdahalo Kwa kuwa mdahalo huo haukuwa na sababu kwake,ikiwa alishatuhumiwa na Tundu Antipas Lisu kuwa mla fedha za Abdul jambo ambalo halina ushahidi. Pamoja na hayo, mdahalo wa wagombea nafasi za uongozi ndani ya vyama vya siasa una faida Gani endapo maswali yanayoulizwa kila siku ni Yale Yale yaliyoulizwa kwenye mahojiano mbalimbali?. Heri Mwamba kutoshiriki maana hakuna jipya.
 
Back
Top Bottom