Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 25,146
- 76,727
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mapori ya HALUNGU akiwa njiani anaelekea Mbozi kwenye Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya kutoka Mlowo ambapo mkutano wale ulizuiwa na Jeshi la Polisi kwa Kutawanya Watu kwa mabomu ya machozi
Magari yameharibiwa kwa kuvunjwa Vioo,Watu waliokuwa katika msafara wa Mbowe wamepigwa vibaya mno,wamepoteza simu na fedha.
Polisi wamempakia Mheshimiwa Mbowe katika Defender na Kutoweka naye pasipo Julikana.
Viongozi wengine waandamizi wamekamatwa na Kupakiwa katika gari tofauti na ile iliyombeba Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Pia soma
- LGE2024 - Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo
======
UPDATES
=======
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi leo tarehe 22 Novemba,2024 katika Pori la Halungu lililopo Wilaya ya Mbozi wamevamia Msafara na kumkamata Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao .
Msafara wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ulikuwa umeshafanya Mikutano ya kampeni katika Kata ya Itaka,Kijiji Cha Itewe na Kata ya Halungu Mjini.
Awali mkutano wa kwanza uliokuwa ufanyike katika mji wa Mlowo uliozuiliwa na Polisi pamoja na wenyeji wetu ambao ni Chama Cha ACT Wazalendo kutualika kushiriki kwenye mkutano wa pamoja ila Polisi walikataa na kutawanya wananchi Kwa mabomy ya machozi .
Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu.
Waliokamatwa ni :
1. Mhe.Freeman Mbowe
2. Mhe. Joseph Mbilinyi - Mwenyekiti Kanda ya Nyassa
3. Mhe. Pascal Haongo- Mbunge wa Mbozi mashariki Mstaafu
4. Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Wilaya ya Mbozi
5. B Appolinary Boniface - Mkuu wa Digital platform
6. Paul Joseph - Afisa habari Kanda ya Nyassa
6. Calvin Ndabila - Afisa habari Kanda ya Nyassa
7. Mdude Nyagali - Mwanaharakati na mwanachama wetu
8. Wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa Bwire,Adamoo na Lingwenya
Jeshi la Polisi wameondoka na viongozi wetu na hajajasema wanawapeleka wapi na mpaka Sasa hatujui wanashikiliwa wapi na Kwa sababu gani.
Chadema Kwa hatua ya Sasa tunasema yafuatayo;
1. Tunalaani kitendo hiki kwani kinaonyesha wazi kuwa ni mkakati wa Polisi kuhujumu kampeni za chama chetu Kwa kushirikiana na CCM
2. Polisi wawaachie mara Moja na bila masharti yoyote ili waendelee na ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
3. Wanachama na Viongozi wetu waendelee na kampeni za kuondoa CCM madarakani .
4. Tunaialika jumuiya ya kimataifa kuja kushuhudia uvunjifu wa Haki za kidemokrasia Kwa vyama vya upinzani nchini katika uchaguzi huu unaoendelea nchini .
Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2024
John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje