Fredy Mtei: Utaratibu wa TRA kufunga akauti za beki kwa wenye changamoto za kikodi haukuwa rafiki

informer 06

Member
May 11, 2024
58
42
Mkurugenzi Mtendaji Wa Pwani Youth Network (PYN), Fredy Mtei amesema kuwa hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kuhusu kuboresha changamoto za kikodi zinaleta matumaini ambayo yanaweza kupunguza kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa.

"TRA imeshaanza kujisahihisha kwa namna mbalimbali katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, hivi karibuni tuliona waliondoa hile Sheria iliyokuwa ikiwataka 'kufrizi' akauti za mteja pale ambapo anakuwa ameshindwa kulipa kodi kwa wakati." amesema Fredy

Anaongeza "Hilo ni jambo jema kwa kuwa litasaidia biashara nyingi ziweze kuendelea kwa sababu unapozuia biashara ya Mtu asitumie hizo fedha na zile fedha zikawa haziingii kwenye mzunguko inakuwa inakwamisha biashara za Watu wengi na hile pesa uliyotegemea kuipata hautoipata."

Lakini pia amesema kuwa wanayo matumaini juu ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili kukusanya maoni kuhusu maboresho ya Sheria za Kodi.

Amesema kundi la vijana limekuwa sehemu wanaoathirika na changamoto za kikodi hivyo mamlaka zinapoonesha nia ya kutatua changamoto hiyo inaongeza chachu ya vijana kujihusisha na shughuli mbalimbali ambazo zinachangia ulipaji Kodi kwa namna mbalimbali.

Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika Mkoani Pwani November 4-5, 2024 ikiwa ni baada ya uzinduzi wa mradi wa 'Kijana Wajibika; Lipa Kodi Yako na Shiriki' ambao unatekelezwa na Pwani Youth Network (PYN) kwa ushirikiano na Restless Development Tanzania.

Mradi huo umetajwa kuwa unalenga kuwajengea uwelewa vijana kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi, ikiwemo kuhakikisha vijana wanashiriki kusimamia uwazi ujumuishi na uwajibikaji wa Serikali na wadau katika matumizi ya Kodi.

Vijana takribani 30 kutoka Halmashauri ya Mji wa Kibaha wamenufaka na mafunzo ambayo yametolewa kwa siku mbili, ambapo yametolewa na wataalamu mbalimbali ikiwemo kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Baadhi ya mawasilisho yaliyotolewa ni pamoja na changamoto za kikodi ambazo zinawakabili vijana pamoja na namna vijana wanavyoweza kushiriki katika kupanga kwa uwazi matumizi ya Kodi kuanzia ngazi za chini ngazi ya Vijiji na Mitaa.
 
Back
Top Bottom