Frame Kubwa Inapangishwa Bamaga Ustawi

relight

Member
Dec 30, 2015
24
2
Frame Kubwa (Futi 41 x 15 ) inapangishwa maeneo ya Bamaga Opposite Chuo cha Ustawi wa Jamii. Frame inaangalia Barabara kuu. Frame ilikuwa Studio ya Picha, Ina Patishen 4, Yaani Vyumba Vinne vilivyogawanywa.
Frame yaweza kutumika kwa kitu chochote. Hata Mini Supermarket au Duka Kubwa, au Kuendelea kama Ofisi yenye vyumba Vinne.
Kwa Mwezi ni 900,000
Haina dalali.

Kuna Gharama Chache za kumrudishia Mpangaji anayeondoka.
1. Milango ya Aluminium
2. Gharama za kuweka Tiles
3. Meter ya Luku - (Umeme)

Tuwasiliane Tafadhali kwa Namba 0769711544
View attachment 326376 View attachment 326377 View attachment 326378 View attachment 326379 View attachment 326380
 
Hembu kuwa muwazi hizo gharama za mpangaji anaeondoka.
Halafu unasema kuna patishen nne ?ukubwa huo ni sawa na 12meters by 4.5meters,mbona ndogo saana kulingana na sifa umezoipa,
La pili
Maana siku hizi watu kwa kuchomekea,inamaana hamkukubaliana akiweka Tiles na luuku iwe inakatwa kwenye kodi?

Maana Luku,Aluminiun na Tiles kwa ukubwa huo sio chini ya 3m ambazo anatakiwa alipe mpangaji mpya,kwa biashara gani ya kuingiza pesa hiyo..

Sasa ili mtu apange hapo,inabidi awe na 13millions kama kodi na gharama za mpangaji alieondoka.

Aisee hembu jipangeni wakuu,
 
Mbona kama kuna mtu anataka kuveshwa koti la mvua kipindi cha jua,inakuaje anaeondoka alipwe ina maana hakua na makubaliano ya ukarabati na mwenye jengo nitakua bahili wa kwanza kukubali kua alikarabati bila kukata kwenye kodi.
 
Anayeondoka analipwa na nani? Na je hizo garama za matengenezo zinatoka wapi? Kama utaelezea vuzuri mimi napataka hapo nifungue barbershop, na mambo mengine, jibu maswali ya wadau hapo juu
 
Samahani Wadau, nilikuwa maeneo mbali na huduma ya Internet.
1. Kodi kwa Mwezi ni Tsh 900,000
2. Eneo lilikuwa linapangishwa kama lilivyo na Wenye Frame hawahusiki na Any Cost za Ukarabati wa eneo, ilikuwa aidha uchukue kama lilivyo au uache. Kwahiyo katika makubaliano na Mwenye Jengo ilikuwa ni kwamba mtu akihama atarudishiwa gharama za kutengeneza eneo kutoka kwa Mpangaji mpya anayeingia.
3. Gharama za kurudisha zitatofautiana na Mpangaji mpya atakayekuja, kwa sababu eneo kwa sasa lipo katika mkao kama Ofisi, hgivyo kuna Milango 3 ya Aluminium midogo, na Mlango Mkubwa wa Mbele. Hivyo sio kila Mpangaji anayekuja atahitaji hiyo milango wala hizo Patisheni. Pia kuna AC Mbili.
4. Gharama Pekee iliyo kwa watu wote ni Tiles Pekee na Mlango wa Mbele wa Aluminium.
5. Kama mteja hatapenda kuchukua mlango wa Mbele wa Aluminum napo ni SAWA TU.

Pia ningependa kuomba wanajamii wenzangu kama wewe hujavutiwa au huhitaji hicho kitu sio lazima uweke COMMENT yako hapa. Waache tu wale ambao wanahitaji. Tunatofautiana.
Tuwasiliane.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…