Form Six kwenda kwenye Mafunzo ya Jeshi

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
1,018
2,130
Nina binti yangu kamaliza Form Six kachaguliwa kwenda jeshi.

Nilikua nauliza je asipoenda inakuaje? Kuna hatua gani wanachukuliwa?

Maana yeye alipokua Form Two alifanyiwa operation KCMC ya tumbo.

Naombeni mwenye kufaham anijushe
 
Nina bint yangu kamaliza form six kachaguliwa kwenda jeshi
Nilikua nauliza je asipoenda inakuaje? Kuna hatua gani wanachukuliwa?
maana yeye alipokua form two alifanyiwa operation KCMC ya tumbo...
Naomben mwenye kufaham anijushe
Sio compulsory then km Afya yake Mbovu muache atulie tu nyumbn kwanza hayo Mambo ya kizamani huko Jkt.
 
Nina bint yangu kamaliza form six kachaguliwa kwenda jeshi
Nilikua nauliza je asipoenda inakuaje? Kuna hatua gani wanachukuliwa?
maana yeye alipokua form two alifanyiwa operation KCMC ya tumbo...
Naomben mwenye kufaham anijushe
Mimi Sikuenda. Na maisha yanaendelea.
Ila kama ana mpango wa kufanya kazi maeneo yanayohusu jeshi na ulinzi ni vyema akaenda.!
 
Ngojanikupe ujanja utanishukuru baadae..
Mwambie aende kujisajili tu kuwa alifika kambini....Akifika atafute marafiki huko halafu kozi ikianza anatoroka.
Halafu wale marafiki zake anakuwa anawasiliana nao kuwa vyeti vikitoka wamhakikishie cheti chake.
Siku ya kuhitimu arudi tena kuchukua cheti chake
 
mh ngumu kumeza
 
JKT ni sehemu ambayo vijana hujifunza ukakamavu, kuwa mwepesi kwa jambo fulani linalokubidi, kutunza muda vizuri hususani kwa wale ambao hufuatilia vizuri mafunzo hayo, zaidi huongeza uzalendo kwa taifa letu.

Pia siyo vijana wote hupata fursa hiyo ya kwenda JKT, mara nyingi ni wale waliofaulu vizuri kidato cha nne, hivyo cheti cha JKT ni added advantage mahali fulani kama watu watalingana vigezo.

Kama huyo binti yako alifanyiwa Operation, anaweza kwenda tu lakini akatoa taarifa za operation yake Kama ikiwezekana awe na vithibitisho, basi huko atapata mafunzo ya scale(kiwango) cha kifanga na siyo tembo Kama wale wazima.

Vijana waende JKT kama wamechaguliwa.
 
Kama yeye yuko tayari kwenda,mruhusu aende,wagonjwa wagonjwa na walemavu huwa wanaripoti Ruvu
 
Ngojanikupe ujanja utanishukuru baadae..
Mwambie aende kujisajili tu kuwa alifika kambini....Akifika atafute marafiki huko halafu kozi ikianza anatoroka.
Halafu wale marafiki zake anakuwa anawasiliana nao kuwa vyeti vikitoka wamhakikishie cheti chake.
Siku ya kuhitimu arudi tena kuchukua cheti chake
Mmh! Inawezekana kweli?
Wa kwangu pia amechaguliwa bado najiuliza aende au asiende coz nasikia wanasema cheti cha JKT kitakuja kumsaidia huko mbeleni kwenye masuala ya ajira, bado niko njia panda, japokua amepangiwa hapo ruvu tu
 
Back
Top Bottom