sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,245
๐๐๐๐ 4 ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ฟ๐๐๐ ๐๐ผ ๐๐๐๐๐๐๐ผ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ฟ๐ผ ๐๐ผ๐๐ ๐๐๐๐๐ฟ๐ผ ๐๐๐๐ 6, ๐๐๐๐๐๐๐พ๐๐๐๐๐ผ ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ ๐๐๐๐๐ผ ๐๐ผ๐๐ผ
Muhimu; Kama una changamoto za kiuchumi ni vyema ukasome form 6 kwenye shule ya serikali uliyochaguliwa ili umalize form 6 na ujaribu bahati yako kuomba mkopo wa serikali ili usome chuo, Post hii nawalenga wale ambao wana uwezo wa kulipia ada za chuo ambazo zina range kuanzia laki 9 hadi milioni 1.3, shule nyingi za private ada ni milioni 2 na kitu, kama unaweza lipia hizo shule basi ni wazi unaweza kuchagua kusoma chuo
๐) ๐๐, ๐ฆ๐ก๐ข๐ญ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ฐ๐ ๐๐จ๐ซ๐ฆ ๐ ๐๐ง๐๐๐ง๐ณ๐ข๐ ๐ฅ๐๐ฏ๐๐ฅ ๐ข๐ฉ๐ข ๐ง๐ ๐ข๐ง๐๐๐ก๐ฎ๐ค๐ฎ๐ ๐ฆ๐ข๐๐ค๐ ๐ฆ๐ข๐ง๐ ๐๐ฉ๐ข ๐ก๐๐๐ข ๐๐ฆ๐๐ฅ๐ข๐ณ๐ ๐๐๐ ๐ซ๐๐?
Utaanzia certificate, kiingilio ni kuwa na D nne, (D mojawapo iwe angalau ya hesabu)
Cerificate utasoma mwaka 1
Diploma utasoma Miaka 2
Degree utasoma Miaka 3 au 4
Katika kila hatua unapomaliza unapewa cheti cha kungilia hatua inayofata
๐) ๐๐, ๐ฆ๐ญ๐ฎ ๐๐ฅ๐ข๐๐ฆ๐๐ฅ๐ข๐ณ๐ ๐๐จ๐ซ๐ฆ ๐ ๐๐ง๐๐๐ง๐ณ๐ข๐ ๐ฅ๐๐ฏ๐๐ฅ ๐ข๐ฉ๐ข
Mtu aliemaliza form 6 ataanzia ngazi ya degree na kuisoma kwa miaka 3 au 4, hatapitia certificate na Diploma
๐) ๐๐ฐ๐๐ง๐ข๐ง๐ข ๐ฎ๐๐ง๐๐ ๐๐ก๐ฎ๐จ ๐๐๐๐๐ ๐ฒ๐ ๐๐จ๐ซ๐ฆ ๐??
- Form 6 hakuna kozi ya iliyojikita kwenye directly kwenye IT ila ukienda chuo utapata nafasi ya kusomea kozi zinazohusu IT, form 6 kuna kombi za pcm, pgm, pcb, cbg n.k hazifikii hata theluthi kwa kinachofundishwa kwenye IT au computer science, kuna kozi mpya imeanzishwa ya phiysics, chemistry na computer lakini kiukweli bado huu sio mbadala, Na ndio maana wenzetu Kenya mtu akimaliza tu form 4 anaenda chuo, Waliifuta form 5 na 6.
- Mtu wa form 6 atasomea elimu ya IT kwa miaka 3 au 4 na atakuwa na cheti cha degree pekee ila Mtu alieunga chuo baada ya form 4 atasomea IT miaka 6 au 7 na atakua na vyeti vya certificate, Diploma na Degree, hivi vyeti vinahusiana moja kwa moja na IT tofauti na vyeti vya form 6 vya pcm, pcb, pgm, n.k.
- Form 6 huwezi kupata ajira ila kwa mtu mwenye diploma anaweza kuajiriwa, ukimaliza diploma yako una sifa za kuajirika tayari, Pia mkikutana huko degree na waliomaliza form 6, yule wa form 6 akishindwa kumaliza chuo basi atabaki na cheti cha form 6 ambacho haajiriki ila mwenye cheti cha diploma hata akishindwa kumaliza degree anaweza kuajirika kwa diploma yake, Licha ya hivyo kuna kazi ambazo zinahitaji mtu awe na diploma na sio degree, Hapa mwenye cheti cha degree pekee hawezi kupewa hii kazi, ila mwenye cheti cha diploma nadegree anaweza kutumia cheti chake cha Diploma kupewa kazi,
- Kwenda field ni kufanya kazi kwa vitendo kwenye mashirika / Taasisi za serikali au private mfano TRA, Halmashauri, Bandarini, Tanroads, n.k hili ni somo la lazima chuoni na linajenga mwanafunzi kupata uzoefu nje ya darasani, Ukianza certificate utafanya field, ukiingia diploma utafanya field na ukiingia degree kuna field, Hii ni advantage kwa mtu aliemaliza form 4 na kwenda chuo, Kwa mtu alieingia degree kwa form 6 ataifanya mara 1 tu huku mwenzake itakuwa ni mara ya 3.
๐) ๐๐, ๐ง๐ข๐ฌ๐จ๐ฆ๐ ๐๐ก๐ฎ๐จ ๐ ๐๐ง๐ข?
Kundi A - vyuo vya nje - Wenye uwezo nawasihi sana msipoteze mudahapa nchini, Kama nyumbani mambo yapo vizuri sioni sababu ya wewe kung'ang'ania kusomea hapa nchini, kama hauna uwezo unaweza kupata scholarship kupitia mitihani ya SAT pale ubalozi wa marekani na mimi ni shahidi, kuna dogo namjua anasomeshwa uturuki, Nenda ubalozi wa marekani kaulizie mitihani ya SAT, Kiingilio huwa ni dola 64 ambayo haizidi laki na nusu ya pesa yetu, hapoinabidi uwe tayari umeanza form 5 na ukipata hio scholarship huna haja ya kumaliza form 6, Vito vya mitihani huwa ni International school of Tanganyika, Dar International Academy, n.k Mtihani ujao unafanyika November, Tembelea hapa kujua vituo vya kufanyia pepa na tarehe >> Find SAT Test Centers
Kundi B - UDSM - Kwa upande wa UDSM hakuna mtu asiejua kwamba udsm ndio chuo baba kwa Tanzania, Maprofesa, Viongozi wa taasisi, wakurugenzi, Mawaziri, Researchers, n.k karibu asilimia 90 wamesomea UDSM, pambana kufa kupona usomee hapa, cheti pekee bila hata kujali ufaulu kinaweza kuku boost kupata ajira, cheo, n.k
Kundi C.Vyuo specific kwajili ya IT - Hivi ni vyuo vimejikita zaidi kwenye elimu ya fani flani, kwenye Sayansi na Teknolojia kuna vyuo vyake kama DIT, MUST, Arusha Tech, n.k Ni vyuo vizuri maana vimejikita zaidi kwenye texhnology na ukisomea IT inakuwa relevant, Ila natoa onyo kwamba hivi vyuo wamekaza mno elimu zao, Hesabu ni nyingi, Masomo ni mengi, Ratiba zimebana ile, Yaani inahitaji kujitoa mno!! Wanafunzi wengi wa hivi vyuo huwa wanadanganwa na waalim wao kwamba kwakuwa wanakaziwa sana, wanasoma masomo mengi, mitihani migumu, n.k basi wao ndio cream ๐๐ Hizo stori huwa zinaishia huko huko vyuoni, hali ya ajira ni tofauti kabisa, Ajira kinachoangaliwa zaidi ni kwamba una cheti, stori imeisha hapo, Mambo ya ulisoma masomo mangapi, mitihani migumu, n.k yanabaki huko huko vyuoni, wanaotaka kwenda vyuo hivi wawe tayari kujitoa maana ukipata ufaulu mdogo unaweza kushindwa kukosa sifa za kusoma masters au kupata scholarship kufadhiliwa kusoma nje ya nchi.
Kundi D. Vyuo vya serikali General - Hivi vyuo vipo kwajili ya kutoa kozi nyingi kwa usawa,Ukiachana na UDSM ambayo nishaitaja kuna UDOM wana taasisi yao inaitwa college of Informatics, Ukikosa hapo nenda Mzumbe nao ni chuo general
Kundi E. Vyuo vya serikali Specific ila indirect - Havina utofauti na kundi C ila hivi ni kwajili ya mambo mengine Mfano kuna IAA hiki ni chuo kipo Arusha kimelenga uhasibu lakini huku kwenye teknolojia hawapo nyuma wana kozi za cyber security, IT, Computer science, kozi za kutengeneza app, Media, n.k, vyuo vingine kuna IFM, Ardhi, TIA, n.k
Kundi F.Private universities - ukikosa kabisa nenda Private, ila kiukweli vyuo vyao vingi vina skendo za kufungiwa fungiwa, walimu wenye sifa ndogo, n.k pia serikali imeweka kipaumbele kwenye wahitimu wa vyuo vyao vya serikali kundi A hadi C..
MUHIMU: Unapoomba ushauri hakikisha kwanza unamuuliza chuo alichosomea anaekupa ushauri, wengi wana tabia ya kusifia sana vyuo walivyosoma mpaka kuvuka mipaka, Kwahio na wewe hapa usiingie mkenge.