Follow the Money; Baada ya Shutuma za ADANI kutoa Rushwa, Tuwachunguze Madalali waliowapigia Chapuo kama walipewa chochote wakae mbali na mali za UMMA

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,465
22,843
Kuna mambo wengi tuliyaona hususan katika suala la Umeme, kuna nchi kama Bangladesh baada ya ADANI kwenda bei za Umeme zikaongezeka....

Na sio hivyo tu hata Kenya ni kwamba dalili zilikuwa bei ya Umeme utaongezeka

Shutuma za ADANI na Kampuni ya Azure Power kutoa Rushwa ili kupata Tender na kunufaisha Kampuni yao ya Solar huko India
Ni kwamba hawa jamaa walipanga kutenga dollar 265 milioni za kuweza kuhonga baadhi ya viongozi wa India kwa ajili biashara yao ya solar

Hizo Hongo ziligundulika / zililipwa vipi ?
Mmoja wa Kiongozi na ndugu wa Adani, (Sagar Adani) alikuwa anatumia simu yake kuweka details na mtiririko wa kusambaza Hongo kwa viongozi wa India; Viongozi wa Azure walikuwa wametenga mpaka Excel na Powerpoint ya jinsi gani watawalipa ADANI kutokana na Hongo zilizotolewa ili ADANI na Azure waweze kufaidika. Kwenye project moja ya 2.3 Gigawatts Hongo ilikuwa imetengwa ya dollar 30,000 kwa megawatt, hawa jamaa mwanzo walipanga waweke hio fee kama development fee ila mwisho wakasema wawape ADANI project yao moja kama baadhi ya malipo....

Baadhi ya hizi habari zilipatikana baada ya FBI kuchukua vifaa vya kielektroniki mwaka jana kutoka kwa Sagar Adani (Director wa moja ya Kampuni ya ADANI na Mpwa wake Adani) katika uchunguzi wao

Nini Kifanyike
Ushauri wangu sababu hawa ADANI inaonekana wao na rushwa ni pete na kidole; na mara nyingi miradi yao ya umeme inaongeza gharama kwa mtumiaji ni vema tukaangalia hawa madalali kama walipewa kitu (wapo tayari kuliangamiza taifa ka vijisenti) hivyo wakalishwe mbali kabisa na mali za UMMA; kwa Taifa ambalo lilipigwa na kina DOWANS na mpaka leo tunaugulia maumivu hatuhitaji tena kuendelea kupigwa. Vilevile kuwe na Total Transparency / UWAZI kwa chochote kinachohusu mali ya UMMA; Tusipoangalia sio Kodi zetu pekee zitakazoendelea kuwanufaisha wachache bali hata Gharama ya Nishati
 
Back
Top Bottom