Florent Ibenge amvuta kocha wa Tabora United, aliyewafunga Yanga na kumpa jukumu

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,459
3,788
Wakati zikisalia saa chache kabla ya Yanga kushuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kupambana na Al Hilal ya Sudan, kocha wa Waarabu hao Florent Ibenge amemvuta mjini kocha mmoja aliyewatibulia wenyeji wake.

Ibenge amemuita jijini Dar es Salaam haraka kocha Anicet Kiazmak ambaye ni kocha wa Tabora United iliyoichapa Yanga wiki chache zilizopita kwenye mchezo wa Ligi.

Ibenge alifanya kazi na Kiazmak pamoja wakiwa Al Hilal ambapo taarifa ambazo Mwananchi imezipata ni kwamba kocha huyo anatakiwa kuja kufanya uchambuzi wa mwisho wa kiufundi kuelekea mchezo wa timu hizo mbili utakaoanza saa 10:00 jioni.

Tayari Kiazmak ameshatua jijiji Dar es Salaam asubuhi hii kwa treni akitokea Tabora akipitia Dodoma tayari kwa kikao hicho na bosi wake wa zamani.

Ibenge anamuamini Kiazmak kwenye eneo la kuwachambua wapinzani ambapo Wakongomani hao wawili watajifungia kwa lengo moja la kuwatafutia dawa wenyeji.
1732611432997.png
 
Uto atachapwa kwa mara ya 3 mtawalia.

Pale Utopolo shida ipo kwa Hersi Said. Fukuzeni huyo
 
Haha! watu mnakelele sawa ngojeni kije kiwake hakuna kushika shati la mtu
 
Wakati zikisalia saa chache kabla ya Yanga kushuka Uwanja wa Benjamin Mkapa kupambana na Al Hilal ya Sudan, kocha wa Waarabu hao Florent Ibenge amemvuta mjini kocha mmoja aliyewatibulia wenyeji wake.

Ibenge amemuita jijini Dar es Salaam haraka kocha Anicet Kiazmak ambaye ni kocha wa Tabora United iliyoichapa Yanga wiki chache zilizopita kwenye mchezo wa Ligi.

Ibenge alifanya kazi na Kiazmak pamoja wakiwa Al Hilal ambapo taarifa ambazo Mwananchi imezipata ni kwamba kocha huyo anatakiwa kuja kufanya uchambuzi wa mwisho wa kiufundi kuelekea mchezo wa timu hizo mbili utakaoanza saa 10:00 jioni.

Tayari Kiazmak ameshatua jijiji Dar es Salaam asubuhi hii kwa treni akitokea Tabora akipitia Dodoma tayari kwa kikao hicho na bosi wake wa zamani.

Ibenge anamuamini Kiazmak kwenye eneo la kuwachambua wapinzani ambapo Wakongomani hao wawili watajifungia kwa lengo moja la kuwatafutia dawa wenyeji.
Uyo kocha asijione mwamba sana kwakuwa aliwafunga yanga, Yanga alifungwa kwasababu zinazojulikana na sio eti kwakuwa yeye alikuwa Bora kimbinu na quality ya wachezaji wake, atakuja kuondoka Tz bila kuaga siku akijaa kwenye mfumo na yanga awanaga dogo wamemtunza tu!
 
Tabora alimfunga yanga kutokana na kukosa wachezaji wake wengi eneo la defense, wangekuwa full mkoko Tabora angepigwa kama ngoma
 
Back
Top Bottom