Finyango ya ushauri-kuepuka anguko la uchumi tuendako

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Nini Kifanyike?

SIASA
Ipo haja ya kuangalia mzigo ambao nchi inabeba kupitia michakato mbalimbali ya kiasiasa na demokrasia.Idadi ya Wizara -Mawaziri/Manaibu Waziri ipunguzwe (Tupunguze gharama kubwa),Idadi ya Majimbo ya uchaguzi ipunguzwe na pia wabunge (Kwa miaka 5 tunatumia fedha kiasi gani kulipa wabunge-Mishahara,Posho,Viinua Mgongo,Etc)..

Madiwani:Viwango vya Sifa,uzoefu na weredi viongezwe ikiwamo elimu,exposure..

Wakuu wa Mikoa/Wilaya:Waondelewe badala Yao watumishi wa umma Wapewe majukumu kupitia hierarchy Za kiutumishi (Hii itapunguza utitiri wa gharama na vyeo)

TOZO KWA DOLA
Malipo ya tozo,fees,ada,pango Kwa dola ni uhujumu uchumi..Fedha Za Tanzania zitumike..Hatuna sababu ya kutengeneza mahitaji (Demand) isiyo ya lazima..
Bandari/shipping lines/CFS/Transporters ..Apartments..Vyuo..Kwa nini walazimishe kulipwa USD?..Ikibidi hata mishahara ya watumishi kwenye baadhi ya Makampuni,taasisi na mashirika (NGO’s) ilipwe Kwa TZS.

KODI
Kufanyike review ya kina kwenye utitiri wa kodi ktk mamlaka zetu na halmashauri zetu..Taasisi..Kodi zinazodidimiza na kifubaza maendeleo ya Viwanda,Uwekezaji na biashara zipunguzwe au kuondolewa.
Tumepoteza wafanyabiashara wengi waliohamia nchi jirani Kama Malawi,Zambia,DRC,Mozambique sababu ya ongezeko la kodi ktk bidhaa nyingi..Tuangalie upya..Tujiulize Kwa nini?

MIRADI

Mwisho nchi ipunguze miradi ya miundombinu inayokula fedha nyingi ambazo kimsingi wanalipwa wakandarasi wa kigeni..

ZABUNI

Zabuni kubwa za taasisi Za Serikali zenye thamani mabilioni ya fedha ktk procurement (IFB/ICT/ICB/RT)ya nchi wapewe wazawa kimkakati ili malipo yake yabaki nchini badala ya sasa fedha nyingi kwenda nje..

MIKOPO

Ni wakati wa kusitisha mikopo isiyo na tija ya haraka Kwa nchi.Ikopwe MIKOPO ya kujenga viwanda (Tuzarishe na kuuza kisha kupata faida),Kilimo (Boost Export),Elimu (Uwekezaji kwenye taaluma Za Kisasa-Engineering,AI,Robotics Science,Nuclear Science,Management Sciences,ICT…)
 
Back
Top Bottom