Final ya kombe la dunia 1950 ilivyoondoka na ndoto za wabrazil

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
Moja ya mechi muhimu na iliyokuwa na maajabu mengi katika historia ya dunia basi ni World Cup 1950 kati ya Brazil vs Uruguay
Finali hii ilipigwa katika dimba maracana huko brazili

Ni fainali iliyochukua watazamaji wengi kuwahi kutokea katika historia ya kombe la dunia





Hiki ndio kilikuwa kikosi cha Brazil
GK 1 Moacir Barbosa
RB 2 Augusto (c)
LB 3 Juvenal
RH 4 José Carlos Bauer
CH 5 Danilo
LH 6 Bigode
OR 7 Friaça
IR 8 Zizinho
CF 9 Ademir
IL 10 Jair
OL 11 Chico
Manager:
Flávio Costa


Hiki ndio kilikuwa kikosi cha wageni Uruguay

GK 1 Roque Máspoli
RB 2 Matías González
LB 3 Eusebio Tejera
RH 4 Schubert Gambetta
CH 5 Obdulio Varela (c)
LH 6 Víctor Rodríguez Andrade
OR 7 Alcides Ghiggia
IR 8 Julio Pérez
CF 9 Omar Óscar Míguez
IL 10 Juan Alberto Schiaffino
OL 11 Rubén Morán

Manager:
Juan López Fontana


Formation ya vikosi ilikuwa kama ifuatavyo


Final hii ilivuta hisia ya wengi sana dunia kwa wakati huo,katika fainali hii Brazil waliamini watashinda na ndio mabingwa wapya wa kombe la dunia.Brazili ilikuwa ni team inayotishika duniani kote.Hakuna team iliyokuwa inaweza kukutana na Brazil na ikajipa zaidi ya asilimia 40% ikatoka Salama.

Brazili akiwa mwenyeji ambaye aliweza kutinga finali na kukutana na waamerica wenzake Uruguay.Kwa kipindi hicho Uruguay ilikuwa ni team dhaifu kabisa na ilisifika kwa kucheza rafu tu na sio mpira hivyo Brazil walikuwa na uhakika watashinda kwa kishindo katika dimba lao la maracana(Uwanja uliochezwa finali ya 2014).

Uwanja mzima walivaa T-shirt zilizoandikwa "Brazil is the champions" huku wakiimba kwa furaha nyimbo za kibrazili zenye morali kwa wachezaji wao.

Uwanja wote wa Maracana ulipambwa mwa maneno matamu "We`re the champions of the world 1950".Mtangazaji aliyekuwa aliyekuwa anatangaza mechi alivalia jezi yake nzuriii nyeupe iliyoandika "Brazil is the champions"..Mabinti warembo waliopamba uwanja waliweza kuacha vifua vyao wazi ili maneno "Brazil is the champions " yaweze kusomeka

Upande wa Uruguay walikuwa na mgogoro na kocha wao Juan López Fontana uliopelekea kocha wao kupewa "last chance".Last chance iliyomwamuru kuwa endapo atarudi nyumbani bila kombe basi ndio utakuwa mwisho wake wa kuishi maana oksijeni yake ni fainali na Brazil tu.

Ni mechi iliyovunja record ya mahudhurio kwa wakati huko( Attendance: 199,854)
R

Referee: George Reader (England)

Alianzisha kipute kati huku team ya Brazil ikaanza kwa soka lao maarufu kama Samba,Dunia ilisimama kwa muda kuangalia mpira wa pasi fupi ukitulia kwenye miguu yenye sumaku ya wabrazili.

Huku nyimbo za kusifu zikiendelea kwa sauti kubwa na ya kusisimua

Hatimaye nnamo dk 47(nyongeza kipindi cha kwanza) kile kikosi bora au ukipenda waite mabingwa wapya watarajiwa wanafanikiwa kupata goal lililofungwa na Friaça hivyo ubao kusomeka Brazil 1 vs 0 Uruguay.

Uwanja mzima ulifulika kwa shangwe.

HT Brazil 1 vs 0 Uruguay


Kocha wa Uruguay akaana kifo chake kipo mbioni,aliamini kuwa huo ndio mwisho wake duniani.Pale refa alipopuliza kipenga cha kumaliza kipindi cha kwanza kocha huyo wa Uruguay akatumia nafasi kuwapungia mkono wa kwaheri mashabiki wote waliokuwa uwanjani hapo.

Taharuki iliwakuta wachezaji wa Uruguay baada ya kugundua kocha ameshakimbia hivyo hayupo katika vyumba vya kubadilishia nguo hivyo wamebaki wakiwa yaani ni watoto ambao hawana mzazi.

Captain wa team ya Uruguay Obdulio Varela akaamua kubeba jukumu lote la kocha,akaamua kufanya mabadiliko ya kikosi ili kuongeza nguvu uwanjani.Captain akaamuru jeshi lake libadili mchezo yaani wacheze vile walivyozoea kucheza(wale tuliokulia uswahilini tunaita "cha uruguay")

Dakikan za mapumziko zikaisha na wanaume wa uruguay haooo wanarudi dimbani kwa kujiamini zaidi.

Upande wa Brazil full shangwe wakiamini sasa wanaingia kukabidhiwa mwali wao.

Mpira safari hii ulikuwa mkali kiasi kwamba mashabiki wakanyamaza kuimba kuanza kushuhudia cha uruguay(Vumbi linavyotimka) huku ubabe ubabe tu uwanjani.

Wachezaji wa Brazil wakaanza kuingiwa na woga wa mechi ile(walikuwa wanavunja tu)..

Mnamo dakika 66,Schiaffino anaiandikia Uruguay goal la kusawazisha hivyo ubao kusomeka

66`Brazil 1 vs 1 Uruguay

H
ii iliwavunja moyo mashabiki wa Brazil na kuanza kushangaa uwanjani wasiamini wanachokishuhudia.



Wakiwa hawaamini wanachokiona gafla Uruguay wanapata corner dk ya 79 na
Ghiggia anaiandikia Uruguay Goal la pili na ndio goal la ushind.


Final ubao ukasoma


Kuanzia siku hiyo ya final(july 16,1950) Brazil waliamini jezi nyeupe zinagundu hivyo kuanzia hapo walikubali kuacha kutumia jezi hizo na kuhamia jezi za njano ambazo wanazitumia mpaka leo.

Fifa 2014 katika uwanja ule ule maracana alialikwa Alcides Ghiggia katika ufunguzi awasalimie wapenzi wa soka duniani.



Na haya ndio maneno yake ""Brazil is like a second home""


Alcides Ghiggia alikufa tarehe na mwezi ule ule aliowafunga Brazili(alikufa july 16 ,2015) na Final ilfanyika july 16 ,1950.


By Deadbody
 

Alikuwa na asili ya Italy na Uruguay,na amewahi kuchezea Ac Milan na Inter Milan.

Alifariki akiwa na miaka 88 hiyo tarehe 16 July 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…