Filamu inaitwa QUEEN OF KATWE.Ni kisa cha kweli kinachoelezea historia ya binti wa miaka 10 (PHIONA MUTESI) anaeishi katika lindi la umasikini uliokithiri na mama yake (LUPITA NYONG'O )npamoja na wadogo zake baada ya baba yao kufariki na kuwaacha wangali wadogo.
Filamu imetengenezwa KATWE kampala Uganda, Urusi na Sudan na inaakisi moja kwa moja maisha duni kabisa ya familia nyingi za kiafrika. PHIONA hakubahatika kwenda shule hivyo hajui kusoma wala kuandika kama ilivyo kwa wadogo zake. Shughuli kubwa wanayoifanya ni kuamka asubuhi na mapema na kwenda mitaani kuuza mahindi ya kuchemshwa kupata kipato cha kila siku.
Baadae anatokea mwalimu wa michezo(kocha Robert katende) anamfundisha mchezo wa Chess.PHIONA anajifunza kwa bidii usiku na mchana akiamini kuwa Chess huenda ikabadilisha maisha yake na familia yake.
KAMPUNI ILIYOTENGENEZA FILAMU HII NI WALT DISNEY.
Ikumbukwe kuwa kampuni hii si kampuni ndogo ni moja ya kampuni kongwe kabisa HOLYWOOD na kampuni ya mwanzo kabisa kubuni na kutengeneza animation mwaka 1923. Na pia iliendelea kudumu hata kipindi kigumu kabisa kutokea katika soko la filamu hii ilikuwa ni baada ya vita kuu ya pili ya dunia Mwaka 1945. Hii iliendelea kudumu na inafanya vizuri mpaka sasa.
KUTUMIKA KWA NYIMBO.
Sound iliyotumika katika moja ya scene ilitengenezwa na mtayarishaji mkongwe P FUNK Majani na PROF.JAY ndie alieitumia katika nyimbo aliyoipa jina la NIKUSAIDIEJE akiwa amemshirikisha Ferooz. Baadae ikarudiwa na Josee Chameleone kutoka Uganda japo ilileta mgogoro mkubwa.
SWALI ni kwamba je P Funk mwenyewe kanufaika na haki miliki ya kazi yake au hafahamu lolote juu ya hii filamu mpya iliyotoka mwishoni mwa mwaka? Profefa je? Analijua hilo pia. Kwa maana kutumika kwa sound ya P Funk kwenye filamu kubwa Holywood ni lazima malipo yamefanyika sehemu. Wasi wasi wangu ni kwamba wa Tanzania si wafuatiliaji wa mambo na ninawasiwasi pia malipo yamefanyika Uganda kwa Josee Chameleone.