Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 14,999
- 31,290
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema mji wa Tarime una nafasi ya kipekee ya kudai haki kupitia chama hicho cha upinzani hasa kikipewa uongozi na wananchi. Lissu ameyasema hayo leo Novemba 21, 2024, wakati akiongea na wananchi wa Tarime akiwa njiani kuelekea kuzindua kampeni za chama hicho kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika eneo la Nyamongo, Tarime vijijini, mkoani Mara.
Lissu amewahimiza wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuwapigia kura wagombea wa chama hicho ili waweze kuongoza mji wa Tarime, kama ilivyokuwa huko nyuma. Amefafanua kuwa, katika Wilaya ya Tarime, CHADEMA kina wagombea 427 kati ya 486 waliohitajika, ikiwa ni asilimia 87.9. Aidha, ameongeza kuwa, katika mitaa 81 wilayani humo, CHADEMA kina wagombea wenyeviti 77 na wagombea ujumbe 350.