Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 368
- 952
Jana kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche amemuacha tena kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Feitoto' na Jonas Mkude kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Sudan.
Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Feitoto kuachwa na Amrouche akitangulia kukosa mechi dhidi ya Niger na Algeria, wakati Taifa Stars ikisaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika, nchini Ivory Coast.
Mara ya mwisho Amrouche kumuita Fei toto ni pale alipochaguliwa kuingia katika kikosi hicho katika mechi mbili dhidi ya Uganda, mchezo ulichezwa katika Uwanja wa Mkapa, Machi 28, baada ya ule uliofanyika Morocco.
Taifa Stars imeshaingia kambini ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan utakaofanyika nchini Saudi Arabia na kikosi hicho kitaondoka nchini leo kwenda nchini humo.
Kikosi hicho kitaondoka na wachezaji 26 wanaocheza ndani na nje ya nchi, wakiwemo makipa Beno Kakolanya, Metacha Mnata na Ally Salum.
Kocha wa zamani wa Yanga, Charles Mkwasa alisema kilichokea wakati wa mechi za mwisho za kufuzu kwa Afcon 2023 ndicho kilichopo kwa sasa na kocha (Amrouche) anatakiwa kuheshimiwa katika uamuzi wake.
"Mwanzo ilionekana kama hakufanya sawa, lakini nini kilitokea? Malengo yake yalitimia. Hata sasa tunaweza kumlaumu lakini hatutakuwa tunatenda haki, kwani yeye ndiye kocha na anajua nini anafanya," alisema kocha huyo wa zamani wa Ruvu Shooting.
Mabeki kwenye kikosi hicho ni Israel Patrick Mwenda(Simba), Abdulrazak Mohamed Hamza (Supersport United), Nickson Kibabage, Ibrahim Abdullah 'Bacca', Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (Yanga) na Abdulmalik Adam (Mafunzo). Viungo ni Sospeter Bajana (Azam FC), Kibu Denis, Mzamiru Yassin (wote Simba), Baraka Majogoro (Chippa United), Mudathiri Yahya (Yanga), Abdi Banda, Abdulmalik Adam, Novatus Dismas (FC Shaktar) Wakati washambuliaji ni George Mpole (FC Lupopo), Said Khamis (Jedinstvo Ub), Nassor Saadun (Ihefu), Morice Michael, Ben Anthony, Saimon Msuva (JS Kabylie) na Mbwana Samatta (PAOK).