Feisal Salum Feitoto amekosa mzazi

Lyrics Master

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
479
667
Mbwana Samatta amekulia katika viunga vya Mbagala huko ndiko kuliko mtambulishan katika uga wa kandanda. Historia ya huyu mchezaji haikuwa rahisi kutoboa hadi kufikia hapo alipofikia. Kuna kipindi alikuwa anakosa hata sh. 200 ya nauli ya kumpeleka mazoezi. Waliokuwa karibu yake walimsaidia pesa ya nauli. Sina haja ya kueleza mengi kuhusu mchezaji huyu aliyecheza African Lyon kwa miaka miwili kuanzia 2008 hadi 2010 alipohamia club yake pendwa ya Simba SC. Kila mtu anayefuatilia na asiyefuatilia soka katika nchi hii anamjua Mbwana Samatta.

Ifahamike hapa, lengo sio kumzungumzia Mbwana Samatta, ila tu nataka nikukumbushe au niwakumbushe wachezaji wa Kitanzania njia alizopitia Mbwana Samatta.

Ndio, baada ya kuwika na African Lyon, 2008-2010 Mbwana Samatta alisajiliwa na Simba SC kwa ada ya usajili ambayo ni siri hadi leo lakini moja ya kipendele katika mkataba wake ilikuwa ni lazima Simba SC wampatie gari mpya aina ya Toyota Mark II Grand GX 110.

Siku zikaenda zikarudi lakini team yake ya Simba hawakutimiza ahadi ya kumpatia gari ambayo walimuahidi, Toyota Mark II Grand GX 110. Kumbuka kipindi hicho Samatta alishaanza kuteka mioyo ya wana Msimbazi wa uhodari wake wa kupachika nyavu… nini kilitokea??

Mbwana Samatta, AKAGOMA. Hii ilikuwa ni mwaka 2011 mwanzoni hapo club ya Simba inakabiliwa na mechi ngumu mbeleni dhidi ya TP Mazembe katika ligi ya Mabingwa Afrika.

Hapo ndipo akaibuka Kenny Mwaisabula Maarufu kama “MZAZI’’ huyu ni mmoja katika ya watu walimsaidia Mbwana Samatta katika makuzi ya kisoka. Hata zile mia mbili mia mbili za nauli za kwenda kwenye mazoezi Mbwana Samatta amepatiwa sana na huyu “MZAZI”

Kenny Mwaisabula, ‘’MZAZI’’ kupitia gazeti la Mwanasporti na kupitia ukaribu aliokuwa nao na Mbwana Samatta alimsihi sana kijana wake asigomee mazoezi wala mechi za Simba. Katika Makala yake hiyo ‘’MZAZI’’ alimuomba Mbwana Samatta aendelee tu kucheza mpira ipo siku atapata kile anachotaka kupitia huo mpira, cha msingi asiache mazoezi na aongezee bidii kwenye mechi kwani kwa kufanya hivyo ipo siku atapata na atakuwa na uwezo wa kununua Zaidi gari mia moja kama hiyo aliyoahidiwa na Simba.

Haikuishia hapo, ‘’MZAZI” akakaa na Mbwana Samatta nakumueleza kuwa Simba SC wapo kwenye ligi ya mabingwa Afrika na kama ataendelea kugoma hawezi kupata chance ya kucheza michezo hiyo mikubwa Zaidi kwa upande wa vilabu barani Afrika.

Ndipo Samatta akamsikiliza ‘’MZAZI’’ Kenny Mwaisabula. Akarudi Kambini. Mechi ya kwanza Simba akacheza na TP Mazembe ugenini tarehe 20/03/2011 na Samatta akiwa ndani Simba akafungwa 3-1 pale Lubumbashi.

Mechi ya pili pale taifa Mnyama anakufa tena 3-2 dhidi ya TP Mazembe magoal ya Simba yalifungwa na SHija Mkina dakika ya 58 kwa Assist ya Mbwana Samatta na goal la pili la Simba lilifungwa na Mbwana Samatta mwenyewe dakika ya 70. Hii mechi Mbwana aling’aa sana. Mwingine aliyeng’aa sana kwenye mechi hii ni Mganda Patrick Ochan. TP Mazembe wakaondoka na majina mawili, Patrick Ochan na Mbwana Samatta. Mwaka huo huo 2011, Mbwana Samatta na Patrick Ochan wakatua TP Mazembe.

Bila ushauri wa ‘’MZAZI’’ Mbwana Samatta angeendelea kugoma na angeendelea kugoma sidhani kama TP Mazembe wangemuona akiwa kwao Mbagala alisubiri GX 110 aliyoahidiwa na Simba SC.

Baada ya hapo wazungu wanasema ‘’the rest is history’’ kila mtu anajua ukwasi wa Captain Diego Mbwana Samatta, niliyecheza nae pale Mbeya viwanja vya MBATTA kipindi cha utoto wetu.

Bahati mbaya sana ndugu yetu Feisal Salum Abdallah ‘’FEITOTO’’ amekosa mtu kama ‘’MZAZI’’ katika carrier yake ya kucheza mpira, mtu ambaye anaona mbali na kukitazama mbali kipaji cha FEITOTO. Huyu mtu amekosekana katika maisha ya Feitoto. Watu walionyuma ya Feisal kwasasa ni wale watu ambao wamefikiri leo tu na sio kesho na kesho kutwa na huyu mchezaji.

Ndio, hakuna ubishi ya kuwa FEITOTO ameibeba sana Yanga katika mabega yake na anastahili kupata donge nono katika mshahara wake lakini njia alizotumia ni kama tu zile Hasira za mkizi. Timu yake ya YANGA inakaribia kuanza kucheza michuano ya kimataifa lakini yeye hayupo kikosini. Na bila shaka hii michuano ya Kombe La Shirikisho la Afrika ingekuwa ni Platform kwake kujitangaza kimataifa Zaidi na huenda angepata team nzuri nje ya Nchi ambayo ingekidhi mahitaji yake mara Zaidi ya watu wanaomrubuni kwasasa.

Naamini kabisa FEITOTO angekuwa na ‘’MZAZI’’ angeshauriwa aendelee kucheza huku akiendelea kubargain juu ya maslahi yake mapya kitu ambacho team yake ya YANGA wasingeshindwa kusimsikiliza.

Feisal Amekosa mtu kama Kenny Mwaisabula.

Nawasilisha.

N.B;

FEISAL SALUM FEITOTO RAMADHANI SINGANO A.K.A MESSI ANAOMBA UPOKEE SIMU YAKE ANAKUPIGIA
 
Feisal na wachezaji wengine wanaoshiriki mashindano ya Caf walitakiwa kipindi hiki wawe wanafanya mazoezi ya kufa mtu, wawe wanajifunza kwa kuangalia mechi mbalimbali kubwa zilizo pita na kupata picha halisi Ushindani ulivyo na namna gani ya kucheza mashindano ya Caf.

Hii michuano kwenye group stage Ina mechi hazipungui Tano ambazo kama mchezaji ataweka nguvu na akilizake zote.
Ndio platform ya kuachana na soka la bongo kwenda kuogelea mihela.

Feisal akilizake zipo kwenye milioni 10 za wachezaji wenzake wenye Mikataba mizuri pale Yanga lakini kama ange ki washa kwenye group stage upo uwezekano wa kulamba mamilioni ya kutosha kwenye klabu mpya zilizo na uwezo mkubwa wa kifedha Africa au Ulaya.
 
Ongeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.

Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.

Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.

Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
 
Hapo Feisal akili yake inamwambia hata Msuva alikaa miezi 6 bila timu na akapata timu nzuri na ikamlipa vizuri na akarudi kwenye kiwango chake na yeye anajiaminisha hivyo hivyo.

Top talented midfielder Feisal but poor you. Reduce you Ego young brother.
Sure, dogo angetulia tu acheze mpira angepata zaidi ya hicho
 
Feisal na wachezaji wengine wanao shiriki mashindano ya Caf walitakiwa kipindi hiki wawe wanafanya mazoezi ya kufa mtu, wawe wanajifunza kwa kuangalia mechi mbalimbali kubwa zilizo pita na kupata picha halisi Ushindani ulivyo na namna gani ya kucheza mashindano ya Caf.

Hii michuano kwenye group stage Ina mechi hazipungui Tano ambazo kama mchezaji ataweka nguvu na akilizake zote.
Ndio platform ya kuachana na soka la bongo kwenda kuogelea mihela.

Feisal akilizake zipo kwenye milioni 10 za wachezaji wenzake wenye Mikataba mizuri pale Yanga lakini kama ange ki washa kwenye group stage upo uwezekano wa kulamba mamilioni ya kutosha kwenye klabu mpya zilizo na uwezo mkubwa wa kifedha Africa au Ulaya.
Ajibu bila shaka alisha wajibu nyinyi watu mnajitia ujuaji wa kifala, ww kama unaona kwenda Ulaya ni rahisi basi na ww tumia shughuri unayo ifanya ikufikishe huko Ulaya na sio kuwapangia watu wengine watimizeje ndoto zao.

Ww umejuaje kama Fei ana ndoto za kucheza nje ya nchi?
Muacheni mtoto wa watu aende anapo pataka msimpangie.
 
Feisal na wachezaji wengine wanao shiriki mashindano ya Caf walitakiwa kipindi hiki wawe wanafanya mazoezi ya kufa mtu, wawe wanajifunza kwa kuangalia mechi mbalimbali kubwa zilizo pita na kupata picha halisi Ushindani ulivyo na namna gani ya kucheza mashindano ya Caf.

Hii michuano kwenye group stage Ina mechi hazipungui Tano ambazo kama mchezaji ataweka nguvu na akilizake zote.
Ndio platform ya kuachana na soka la bongo kwenda kuogelea mihela.

Feisal akilizake zipo kwenye milioni 10 za wachezaji wenzake wenye Mikataba mizuri pale Yanga lakini kama ange ki washa kwenye group stage upo uwezekano wa kulamba mamilioni ya kutosha kwenye klabu mpya zilizo na uwezo mkubwa wa kifedha Africa au Ulaya.
Sahihi Kabisa Kaka ameshimdwa hata kujifunza kwa Luis Miquissone dogo analamba si chini ya 90M pale Club Al Ahly dogo alikiwasha sana hatua ya makundi Hadi akaonwq
 
Ongeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.

Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Mbwana Samatta hakuvunja mkataba Simba ndio aende Tp Mazembe, Bali TP Mazembe walifikia makubaliano na Simba, Samatta akauzwa kama sikosei 150M Mazembe waliilipa Simba SC
 
Ongeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.

Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Umbumbumbu ni mzigo, siku umbumbumbu ukiisha kichwani mtaelewa ata vitu vidogo.
Samata na Ochan waliuzwa Kwa makubaliano ya Mazembe na Simba.
Feisal amesha ambiwa kama kunatimu Ina muhitaji aende mezani wazungumze na Yanga.
Feisal ni Mali ya Yanga mpaka 30 Mei 2024 kuendelea kuwa Kiburi na kukaza shingo ana jiharibia mwenyewe.
Kwa kesi yake ilivyo Feisal ata aende Cas hatoboi atakula muda wake, fedha zake na mwishowe atarudishwa Yanga kumaliza mkataba wake ila kwakua wanao mshauri ni vilaza wenzake basi tusubiri tuone.

Kuna wapuuzi wanamdanganya wakati shauri lake likiendelea ata pewa nafasiya kutafuta timu, Ao jamaa wanazidi kumuingiza choo Cha kike , Feisal amefanya jaribio la Kuvunja mkataba kihuni Kwa namna alivyo fanya ni uharamia katika soka na atarudishwa Yanga na haohao CAS.
 
Nyinyi utopolo mna roho za kichawi sana hata ngasa mlisha kuharibia dili la kwenda sudani ambalo linge mpatia pesa kibao hivyo nyinyi hatuwashangai.
 
Ongeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.

Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Hiyo timu si impeleke maombi Yanga, au haijui utaratibu?
 
Umbumbumbu ni mzigo, siku umbumbumbu ukiisha kichwani mtaelewa ata vitu vidogo.
Samata na Ochan waliuzwa Kwa makubaliano ya Mazembe na Simba.
Feisal amesha ambiwa kama kunatimu Ina muhitaji aende mezani wazungumze na Yanga.
Feisal ni Mali ya Yanga mpaka 30 Mei 2024 kuendelea kuwa Kiburi na kukaza shingo ana jiharibia mwenyewe.
Kwa kesi yake ilivyo Feisal ata aende Cas hatoboi atakula muda wake, fedha zake na mwishowe atarudishwa Yanga kumaliza mkataba wake ila kwakua wanao mshauri ni vilaza wenzake basi tusubiri tuone.

Kuna wapuuzi wanamdanganya wakati shauri lake likiendelea ata pewa nafasiya kutafuta timu, Ao jamaa wanazidi kumuingiza choo Cha kike , Feisal amefanya jaribio la Kuvunja mkataba kihuni Kwa namna alivyo fanya ni uharamia katika soka na atarudishwa Yanga na haohao CAS.
Umemaliza kila kitu Mkuu
 
Sahihi Kabisa Kaka ameshimdwa hata kujifunza kwa Luis Miquissone dogo analamba si chini ya 90M pale Club Al Ahly dogo alikiwasha sana hatua ya makundi Hadi akaonwq
Usilazimishe mtu atimize ndoto zake kwa mtazamo wako? kila mtu ana ndoto zake na ana namna ya kuzitimiza usimpangie.
 
Umemaliza kila kitu Mkuu
Ajamaliza chochote kubalini utopolo ni kikundi kilicho jaa wachawi.
Hili suala la fei viongozi wa utopolo wangekuwa na akili wangetumia busara tu kumuachia dogo asepe na sio kumngangania ili kumkomoa.

Kama ni suala la kufuata sheria Utopolo ndo mabingwa wa uvunjanji wa kanuni za soka ndani ya nchi hii.
 
Mbwana Samatta amekulia katika viunga vya Mbagala huko ndiko kuliko mtambulishan katika uga wa kandanda. Historia ya huyu mchezaji haikuwa rahisi kutoboa hadi kufikia hapo alipofikia. Kuna kipindi alikuwa anakosa hata sh. 200 ya nauli ya kumpeleka mazoezi. Waliokuwa karibu yake walimsaidia pesa ya nauli. Sina haja ya kueleza mengi kuhusu mchezaji huyu aliyecheza African Lyon kwa miaka miwili kuanzia 2008 hadi 2010 alipohamia club yake pendwa ya Simba SC. Kila mtu anayefuatilia na asiyefuatilia soka katika nchi hii anamjua Mbwana Samatta.

Ifahamike hapa, lengo sio kumzungumzia Mbwana Samatta, ila tu nataka nikukumbushe au niwakumbushe wachezaji wa Kitanzania njia alizopitia Mbwana Samatta.

Ndio, baada ya kuwika na African Lyon, 2008-2010 Mbwana Samatta alisajiliwa na Simba SC kwa ada ya usajili ambayo ni siri hadi leo lakini moja ya kipendele katika mkataba wake ilikuwa ni lazima Simba SC wampatie gari mpya aina ya Toyota Mark II Grand GX 110.

Siku zikaenda zikarudi lakini team yake ya Simba hawakutimiza ahadi ya kumpatia gari ambayo walimuahidi, Toyota Mark II Grand GX 110. Kumbuka kipindi hicho Samatta alishaanza kuteka mioyo ya wana Msimbazi wa uhodari wake wa kupachika nyavu… nini kilitokea??

Mbwana Samatta, AKAGOMA. Hii ilikuwa ni mwaka 2011 mwanzoni hapo club ya Simba inakabiliwa na mechi ngumu mbeleni dhidi ya TP Mazembe katika ligi ya Mabingwa Afrika.

Hapo ndipo akaibuka Kenny Mwaisabula Maarufu kama “MZAZI’’ huyu ni mmoja katika ya watu walimsaidia Mbwana Samatta katika makuzi ya kisoka. Hata zile mia mbili mia mbili za nauli za kwenda kwenye mazoezi Mbwana Samatta amepatiwa sana na huyu “MZAZI”

Kenny Mwaisabula, ‘’MZAZI’’ kupitia gazeti la Mwanasporti na kupitia ukaribu aliokuwa nao na Mbwana Samatta alimsihi sana kijana wake asigomee mazoezi wala mechi za Simba. Katika Makala yake hiyo ‘’MZAZI’’ alimuomba Mbwana Samatta aendelee tu kucheza mpira ipo siku atapata kile anachotaka kupitia huo mpira, cha msingi asiache mazoezi na aongezee bidii kwenye mechi kwani kwa kufanya hivyo ipo siku atapata na atakuwa na uwezo wa kununua Zaidi gari mia moja kama hiyo aliyoahidiwa na Simba.

Haikuishia hapo, ‘’MZAZI” akakaa na Mbwana Samatta nakumueleza kuwa Simba SC wapo kwenye ligi ya mabingwa Afrika na kama ataendelea kugoma hawezi kupata chance ya kucheza michezo hiyo mikubwa Zaidi kwa upande wa vilabu barani Afrika.

Ndipo Samatta akamsikiliza ‘’MZAZI’’ Kenny Mwaisabula. Akarudi Kambini. Mechi ya kwanza Simba akacheza na TP Mazembe ugenini tarehe 20/03/2011 na Samatta akiwa ndani Simba akafungwa 3-1 pale Lubumbashi.

Mechi ya pili pale taifa Mnyama anakufa tena 3-2 dhidi ya TP Mazembe magoal ya Simba yalifungwa na SHija Mkina dakika ya 58 kwa Assist ya Mbwana Samatta na goal la pili la Simba lilifungwa na Mbwana Samatta mwenyewe dakika ya 70. Hii mechi Mbwana aling’aa sana. Mwingine aliyeng’aa sana kwenye mechi hii ni Mganda Patrick Ochan. TP Mazembe wakaondoka na majina mawili, Patrick Ochan na Mbwana Samatta. Mwaka huo huo 2011, Mbwana Samatta na Patrick Ochan wakatua TP Mazembe.

Bila ushauri wa ‘’MZAZI’’ Mbwana Samatta angeendelea kugoma na angeendelea kugoma sidhani kama TP Mazembe wangemuona akiwa kwao Mbagala alisubiri GX 110 aliyoahidiwa na Simba SC.

Baada ya hapo wazungu wanasema ‘’the rest is history’’ kila mtu anajua ukwasi wa Captain Diego Mbwana Samatta, niliyecheza nae pale Mbeya viwanja vya MBATTA kipindi cha utoto wetu.

Bahati mbaya sana ndugu yetu Feisal Salum Abdallah ‘’FEITOTO’’ amekosa mtu kama ‘’MZAZI’’ katika carrier yake ya kucheza mpira, mtu ambaye anaona mbali na kukitazama mbali kipaji cha FEITOTO. Huyu mtu amekosekana katika maisha ya Feitoto. Watu walionyuma ya Feisal kwasasa ni wale watu ambao wamefikiri leo tu na sio kesho na kesho kutwa na huyu mchezaji.

Ndio, hakuna ubishi ya kuwa FEITOTO ameibeba sana Yanga katika mabega yake na anastahili kupata donge nono katika mshahara wake lakini njia alizotumia ni kama tu zile Hasira za mkizi. Timu yake ya YANGA inakaribia kuanza kucheza michuano ya kimataifa lakini yeye hayupo kikosini. Na bila shaka hii michuano ya Kombe La Shirikisho la Afrika ingekuwa ni Platform kwake kujitangaza kimataifa Zaidi na huenda angepata team nzuri nje ya Nchi ambayo ingekidhi mahitaji yake mara Zaidi ya watu wanaomrubuni kwasasa.

Naamini kabisa FEITOTO angekuwa na ‘’MZAZI’’ angeshauriwa aendelee kucheza huku akiendelea kubargain juu ya maslahi yake mapya kitu ambacho team yake ya YANGA wasingeshindwa kusimsikiliza.

Feisal Amekosa mtu kama Kenny Mwaisabula.

Nawasilisha.

N.B;

FEISAL SALUM FEITOTO RAMADHANI SINGANO A.K.A MESSI ANAOMBA UPOKEE SIMU YAKE ANAKUPIGIA
hivi fai toto kweli ni mchezaji mzuri sana kiasi cha kusumbu aakili za watanzania? hamna kazi zingine za kufanya?
 
Back
Top Bottom