Fedha nyingi za miradi ya maendeleo zinafika kikamilifu na kwa wakati muafaka, na kazi yake inaonekana maeneo husika ikiwemo huku vijijini

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
15,569
17,692
miradi ya maji, barabara, vituo vya afya, zahanati na hospitali; vyumba vya madarasa, maabara, ofisi na nyumba za watumishi wa umma, masoko ya kisasa na vituo vya polisi, miradi ya umeme, kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na ufugaji kisasa, huduma za usafirishaji ardhini, majini na angani nakadhalika, n.k...

serikali sikivu ya CCM,
chini ya kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, iliahidi kwa maneno na sasa inatekeleza kwa vitendo ahadi zake zote iliyowaahidi waTanzania, kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Imeddhamira kukamilisha miradi yote kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2025..

kwa kasi ya maendeleo hayo mijini na vijijini, eti kuna vibaraka waliorubuniwa na watu wa magharibi, hawayaoni haya na bila aibu wanawahadaa wananchi ambao tayari wameamua kumuunga mkono kiongozi wa waTanzania wote, mpendwa Dr.Samia Suluhu Hassan, katika nia na azma yake hii njema ya kuwaletea wanainchi wa Tanzania maendeleo endelevu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi..

nawasihi vibaraka na wapinzani wote nchini kutokupoteza muda na rasilimali zao nyingine bila sababu yoyote.
Mama aunaupiga mwingi right, left, right and center...
mtashindana nae lakini hamtashinda..

Shukran na Asanti ni kwa Mwenyezi Mungu, kwa kumjalia na kumpa Dr.Samia Suluhu Hassan, afya njema, nguvu na uwezo wa kazi nzuri sana anazofanya nchi nzima kwa maslahi mapana ya waTanzania wote 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom