FedEx and TRA issue at Dar Airport

Kinyasi

Member
Nov 22, 2010
72
31
Ndugu wadau wa Ughaibuni na Bongo,

Ni matumaini yangu mpo salama na mna enjoy spring season hasa kwa wale wenzangu tulio kenye ukanda wa baridi.

Nilikuwa napenda kujua kama kuna mwenye this experience anapotuma mzigo kwenda Dar na kuandikiwa ridiculous tax invoice isiyolingana na thamani ya mzigo? Kuna matukio mawili hivi: Mosi kuna siku nilikuma mzigo una thamani ya $278 na uzito wa 21 pounds, ulipofika Fedex Dar wakadai nitoe Tsh. 50,000/= processing fee na 200,000/= ya kulipa agent afanye clearance ya mzigo airport. Pili kuna mzigo mwingine nimetuma kwenda Dar kwa njia ya Fedex una thamani ya $625 na uzito wa pound 23, Fedex wakanambia upo Customs ya TRA airport, zinahitajika tsh. 50,000/= processing fee ya Fedex na Tsh.470,000/= (Laki 4 na Sabini Elfu) kuutoa mzigo kwenye custom ya TRA airport.

Kinachonishangaza, kuna rafiki yangu nipo nae hapa New York alituma mzigo wake wenye thamani na uzito sawa na scenerio namba 1 kwa Fedex kwenda Morogoro akautoa kwa kulipia Tsh. 30,000/= (Thelasini elfu tu). Ninachojiuliza, Je issue ni Fedex au custom ya TRA au kitu kingine zaidi? Mbona nikituma kwa njia ya USPS mizigo yenye thamani na uzito wa ranges kama nilizozitaja hapo juu na ikifika Posta ya Dar, wanachaji siyo zaidi ya Tsh. 10,000/= (Elfu kumi tu)?

Kingine kinachonishangaza zaidi kuna mzigo mwingine wa thamani ya euro 700 na uzito wa kg 25, niliouagiza hivi karibuni toka Germany kwa njia ya DHL, umefika Dar na ukakombolewa kwa Tsh. 2,800/= (Elfu mbili na mia nane tu).

Ninachojiuliza, je issue ni Fedex au Custom ya TRA airport au something else nisichokijua? Je ni nani yupo sahihi ( kwenye makato ya kutoa mizigo ) kati ya Fedex na TRA aiport kwa upande mmoja na Shirika la Posta na DHL Dar kwa upande mwingine?

Binafsi nahisi kama kuna kitu hakipo sawa hapo kwenye custom ya TRA airport, kuna kama kamchezo kanachezwa kutuibia kwa kutubambikia kodi zisizo na kichwa wala miguu. Kwa mfano sioni sababu ya Fedex na TRA kulazimisha agent alipwe pesa za kuutoa mzigo wakati unaweza kutolewa na mpokeaji kwa kufanya malipo ya kodi kwenye custom za TRA airport bila kumtumia agent.

Natanguliza shukrani kwa wale watakao share experience zao kwenye hii issue.

Kinyasi N Monyi
Rochester, NY.
5/02/2016
 
Bidhaa za kutoka nje zina kodi aina mbili (1) Excise duty ambayo kwa bidhaa nyingi ni 25% (2) VAT ambayo inatozwa 18% kwenye Gharama ya mzigo + Excise duty. Uliyolipa wewe ndio sahihi huyo Rafiki kakwepa kodi
 
Hizi ishu za kodi zinaumiza kwa kweli, nimetoa mzigo wiki iliyopita hapo airport uliotumwa toka ethiopia wenye kilo 80, kodi ilikuwa milioni 6 hao jamaa DHL laki 6 Na agent laki 3. Hiyo ya agent ndio niliishangaa sana....!!
 
Kawaida tra wanaweza kuamua kukagua mzigo na mara nyingi utalipia import duty 25% na vat 18% ya thamani ya invoice. Kuhusu clearance charge fedex hiyo elfu hamsini ni kukupa documents ambayo ni fixed. Agent ni makubaliano yako na yeye.
 
Duh! Sasa kwanini ukitumwa kwa Posta at DHL hizo kodi ulizozitaja haziwagi applicable? Kwa mfano Posta unalipia no more than tsh. 10,000= na DHL unalipia tsh. 2,800/= tu? Ina maana hao Posta na DHL wanakwepa kodi au?
 
Duh! Pole sana mkuu. Vitu kama hivi vinatukatisha tamaa sana wasafirishaji.
 
Kawaida tra wanaweza kuamua kukagua mzigo na mara nyingi utalipia import duty 25% na vat 18% ya thamani ya invoice. Kuhusu clearance charge fedex hiyo elfu hamsini ni kukupa documents ambayo ni fixed. Agent ni makubaliano yako na yeye.

Hivi Kwanini wanalazimisha kumtumia agent kukutolea mzigo? Kwanini basi wasiruhusu mtu achukue invoice na kwenda mwenyewe Custom za TRA kulipia mzigo wake? Ndugu yangu alipowaambia ataenda mwenyewe, akakataliwa na kuambiwa kwamba mzigo unatolewa na ma-agent tu.
 
Tra wametoa leseni kwa maagent ambao wanajua kufanya declaration na hata kama kodi itakuwa imekusanywa ndogo maadamu agent yupo wanamahali pa kudai kuliko individual ambaye atakuwa ameshaondoka.
 
kuagiza mzigo nje ya nchi kuna drama nyingi sana tanzania.

kitu hicho hicho kimoja mwenzako anaweza lipa kodi laki moja, wewe ukalipishwa milioni 2 na mwingine asilipishwe kabisa...

huko bandarini sasa hivi ndio kodi za kukomoana maana target wanalazimisha zifikiwe kwa ku uplift vitu ovyo....
 
Mimi nilitoa box la 1kg thamani € 320 wenye postal €85.
Nililipa 18% VAT ikiwa pamoja na ya kusafirisha yaani na ya 85€ + 0.6% assesment nadhani ilifika zaidi ya 210,000/=
Hapo sijawekewa custom duty
airport charges 25000/= +agency fee 80 000/= + Vat 13 000/=

Nililia nikataka kuuacha
 
Tra wametoa leseni kwa maagent ambao wanajua kufanya declaration na hata kama kodi itakuwa imekusanywa ndogo maadamu agent yupo wanamahali pa kudai kuliko individual ambaye atakuwa ameshaondoka.
Hii ni njia ya kuhalalisha ulaji tu na wala hai-make sense yoyote! Eti kama kodi imekusanywa ndogo! Ina maana wanafanya kazi kwa kubahatisha? Na kama wanajua wao ni wazembe kiasi cha kukosea kukusanya kodi inayotakiwa mpaka waje kufuatilia tena baada ya mzigo kutoka kwanini wasichukue contacts za mwenye mzigo! Tanzania nchi imeoza hii. Unakuta wanaweka taratibu za kijinga kabisa. Nadhani ni kwa ajili wanajua watanzania ni wapole na hawafuatilii!
 
Hiyo fee ya agent ni wizi tu. Ukifuatilia utakuta kuna mgao wanagawana kati ya hao ma-agent na maofisa waliopitisha hiyo sheria ya wizi. Au ni kampuni zao na ndugu zao! BTW wanapotoza hizo kodi huwa hawaangalii aina ya bidhaa bali ni thamani tu?
 
Hawa FeDEx ni laghai sana. Ilibidi niutelekeleze mzigo wangu wa thamani. Hayo ya TRA nafikiri wanadanganya. Wanatoa risit za kupriti kariakoo.
Ukiwabana wanakubali kuwa huongeza kwa ajili ya ofsi yao hapo Ubungo. Hata staff wao mpaka delivery boys sio waaminifu. Ofice pio sio customer inviting.

Mzigo hata kkama ukilipiwa full nje utalazimiishwa kulipia tena. Huko Airpot mizigo hucheleweshwa kwa makusudi kuonngeaza storage charges. Seems the bussness does not have regulator in this. Country. Owners nasikia ni Wahindi wako ktkt ya city. Shame thing. Ubungo wameweka Waswahili wenye roho ngumu.

Nilikuwa napenda kujua kama kuna mwenye this experience anapotuma mzigo kwenda Dar na kuandikiwa ridiculous tax invoice isiyolingana na thamani ya mzigo? Kuna matukio mawili hivi: Mosi kuna siku nilikuma mzigo una thamani ya $278 na uzito wa 21 pounds, ulipofika Fedex Dar wakadai nitoe Tsh. 50,000/= processing fee na 200,000/= ya kulipa agent afanye clearance ya mzigo airport. Pili kuna mzigo mwingine nimetuma kwenda Dar kwa njia ya Fedex una thamani ya $625 na uzito wa pound 23, Fedex wakanambia upo Customs ya TRA airport, zinahitajika tsh. 50,000/= processing fee ya Fedex na Tsh.470,000/= (Laki 4 na Sabini Elfu) kuutoa mzigo kwenye custom ya TRA airport.

Kinachonishangaza, kuna rafiki yangu nipo nae hapa New York alituma mzigo wake wenye thamani na uzito sawa na scenerio namba 1 kwa Fedex kwenda Morogoro akautoa kwa kulipia Tsh. 30,000/= (Thelasini elfu tu). Ninachojiuliza, Je issue ni Fedex au custom ya TRA au kitu kingine zaidi? Mbona nikituma kwa njia ya USPS mizigo yenye thamani na uzito wa ranges kama nilizozitaja hapo juu na ikifika Posta ya Dar, wanachaji siyo zaidi ya Tsh. 10,000/= (Elfu kumi tu)?

Kingine kinachonishangaza zaidi kuna mzigo mwingine wa thamani ya euro 700 na uzito wa kg 25, niliouagiza hivi karibuni toka Germany kwa njia ya DHL, umefika Dar na ukakombolewa kwa Tsh. 2,800/= (Elfu mbili na mia nane tu).

Ninachojiuliza, je issue ni Fedex au Custom ya TRA airport au something else nisichokijua? Je ni nani yupo sahihi ( kwenye makato ya kutoa mizigo ) kati ya Fedex na TRA aiport kwa upande mmoja na Shirika la Posta na DHL Dar kwa upande mwingine?

Binafsi nahisi kama kuna kitu hakipo sawa hapo kwenye custom ya TRA airport, kuna kama kamchezo kanachezwa kutuibia kwa kutubambikia kodi zisizo na kichwa wala miguu. Kwa mfano sioni sababu ya Fedex na TRA kulazimisha agent alipwe pesa za kuutoa mzigo wakati unaweza kutolewa na mpokeaji kwa kufanya malipo ya kodi kwenye custom za TRA airport bila kumtumia agent.

Natanguliza shukrani kwa wale watakao share experience zao kwenye hii issue.

Kinyasi N Monyi
Rochester, NY.
5/02/2016[/QUOTE]
 
Kawaida tra wanaweza kuamua kukagua mzigo na mara nyingi utalipia import duty 25% na vat 18% ya thamani ya invoice. Kuhusu clearance charge fedex hiyo elfu hamsini ni kukupa documents ambayo ni fixed. Agent ni makubaliano yako na yeye.
Mambo mengine ni wizi mtu. Kutia document peke yake tu shs 50,000. Kutoa tu tena photo copy. Ni wizi bila ssbabu kwa kuwa yule aliyetuma alishalipa.
 
Nimepokea parcels, nyakati tofauti kupitia UPS na TNT, hawa jamaa hawana tatizo hasa TNT, wanafanya kwa weledi sana kazi yao.
 
Inategemea mzigo / bidhaa uliyotuma. Kuna mizigo lazima ilipiwe tena custom hata km mtumaji ameshalipia gharama za kutuma. hii ni kulingana na sheria za importArtation za nchi husika. ishanitokea Mara nyingi sana
 
Hizi ishu za kodi zinaumiza kwa kweli, nimetoa mzigo wiki iliyopita hapo airport uliotumwa toka ethiopia wenye kilo 80, kodi ilikuwa milioni 6 hao jamaa DHL laki 6 Na agent laki 3. Hiyo ya agent ndio niliishangaa sana....!!
Kilo sio issue kodi inategemea aina ya mzigo.
 
Duh! Sasa kwanini ukitumwa kwa Posta at DHL hizo kodi ulizozitaja haziwagi applicable? Kwa mfano Posta unalipia no more than tsh. 10,000= na DHL unalipia tsh. 2,800/= tu? Ina maana hao Posta na DHL wanakwepa kodi au?
Vifurushi vyote vinatakiwa vipitie "Custom Desk" hapo Posta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…