BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 505
- 1,218
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 21, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake Francis Kiwanga, amesema ushirikiano baina ya Mataifa hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa wananchi.
“Katika kipindi cha miaka 14, tumepata rasilimali fedha ambazo zimetuwezesha kufanyakazi na taasisi zaidi ya 6000, katika kuboresha maisha na kuondoa umasikini hapa nchini” amesema Kiwanga.
Aidha amebainisha kuwa Denmark imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania tangu kipindi cha Baba wa Taifa, na kwamba wameendelea kufanyakazi katika Awamu zote za uongozi na kwamba Sherehe hizo zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka mitatu ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaad Spandet, amesema Serikali ya Denmark itaendelea kudumisha ushirikiano uliopo na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia.
Aidha ameipongeza FCS kwa kazi kubwa inayofanya kwa kuwafikia wananchi wengi katika miradi ya kijamii kwa kushirikiana na Asasi nyingine za Kiraia nchini.