leo maeneo ya kinondoni kwenye vituo vya mabasi nimeona matangazo ya fast jet ya kazi yamebandikwa zikiwemo nafasi za maafisa waandamizi kabisa, nilishindwa kupata picha kutokana na wingi wa watu ila kama tangazo litaendelea kuwepo ntaambatanisha na picha, nimejiuliza maswali haya matangazo siyo ya matapeli kweli kwani iliwahi kutokea shirika Fulani la ndege nadhani ni Qatar nalo lilifanya vivyo hivyo ambapo badae kama kumbukumbu zangu ni sahihi ikaja kugundulika kuwa ni utapeli, ni kweli mmeshindwa kutoa tangazo hata kwenye magazeti ya bei rahisi.