FARU FAUSTA

KACK

Senior Member
Mar 28, 2015
129
106
Viumbe Wote Wana Mwanzo Wa Maisha Yao (Huenda After Fertilization) Na Huwa pia Na Mwisho Wa Maisha Hapa Duniani ( Kifo)

Faru Fausta Anagharamiwa Pesa Nyingi Zaidi Ya Shilingi Million Mbili Kwa Siku.
Anayegharamia Huduma Hizi Ni Serikali Ileile Ambayo Wananchi Wake (Binadamu) Wanakatisha Maisha Kwa Kukosa Fedha Kidogo Za Matibabu.

Huenda Tumekosa Weledi Wa Kupambanua Hili Suala Bila Kuangalia Wanyama Wanatuingizia Faida Kiasi Gani Iliyo Na Thamani Kuliko Binadamu.

Ushauri:
Faru Fausta Amezeeka, Kaliingizia Taifa Utajiri Ambao Mchango Wake Huenda Wananchi Wa Chini Tusiutambue, Lakini Serikali Ni Lazima Itambue kuwa Faru Huyo Ipo Siku Atakufa.

Kwa Kuwa Faru Huyo Atakufa Ni Bora Gharama Inayotumika Kumtibu Itumike Kuajiri Askari Wa Wanyama Pori Wakaongeze Nguvu Ya Kulinda Wanyama Wengine Kama Tembo Vijana Wenye Afya Njema Ambao wanakatishwa Uhai Na Majangili Ktk Mbuga Zetu .

Kiasi Hicho Cha 64 M kwa Mwezi Kinatosha Kuajiri Watu hao kwa idadi inayoweza kuleta mabadiliko.

Pia Faru Fausta Akifa Mwili Wake uwe treated Ili Usioze Na Uwekwe Sehemu Maalumu Ktk Moja Ya Mbuga Za wanyama Ili Aendelee kuwa Kivutio Kwa Watalii. Wazo Hili Linaweza Kutokua Na Uzito Kwa Mtu asiyetaka Kufikiria Mbali.
Huenda Miaka Ijayo Hatutakua Na Wanyama Wa Aina Hiyo Ktk Uso Wa Dunia, Zitakuwepo Historia Tu Kwa Vizazi Vitakavyokuwepo. Uwepo Wa kielelezo Halisi Cha Mnyama Aliyekufa Miaka Kadhaa Itakua Kivutio Kikubwa Kwa Watalii Na Itaingiza Pesa Nyingi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…