Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,665
- 1,228
šBukoba_Kagera
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Comred Faris Buruhani, amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kwamba vijana wa Chama Cha Mapinduzi watakuwa mstari wa mbele katika kulinda na kudumisha amani na utulivu kabla, wakati na baada ya zoezi la upigaji kura litakalofanyika kote nchini tarehe 27/11/2024 katika vijiji, vitongoji na mitaa yote.
Comred Faris ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika mitaa minane (08) inayounda Kata ya Kitendaguro, Bukoba Mjini.
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Aidha, Comred Faris ametoa rai kwa vijana wa vyama vingine ya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huu kulinda na kudumisha amani na utulivu kama wanavyofanya vijana wa CCM na kuonya kwamba vijana wa CCM hawatawafumbia macho watu wote wanaojipanga kuleta vurugu kwenye uchaguzi huu, maana yapo maisha baada ya uchaguzi.
#SerikaliZaMitaa
#SuutiYaWananchi
#JitokezeUshirikiUchaguzi