Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 263
- 429
Kuna wakati unataka heshima kutoka kwa wale wanaokuzunguka katika jamii kwa sababu unaona unastahili kupata hiyo heshima.
Ingawaje kuheshimiwa sio jambo rahisi ambalo unaweza kulipata kutokana na tabia zako binafsi na mtazamo wa jamii inayokuzunguka.
Hata hivyo kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kukupa heshima kutoka kwa watu wanaokuzunguka haijalishi una kipato gani, cheo na umaarufu.
Mambo haya yakizingatiwa yataweza kukufanya ukuze heshima yako mbele ya jamii iwapo utatayaishi vema.
Jambo la kwanza ni kujenga tabia ya kuwajali watu wengine, Kuvaa kiatu cha uhusika wao ili kujua maumivu yao na furaha yao.
Hii itakusaidia kuwapa faraja pale ambapo wamekumbwa na matatizo na kuwapongeza pale wanapongeza pale wanapofanikiwa.
Kuwa na moyo wa namna hii utakuwa umetimiza Ile kanuni ya kizungu "Golden Rule" iyotaka kila mmoja amtendee mwenzake kadri ambavyo anapenda atendewe.
Kuwa mkweli na mwaminifu kwa watu wote wanaokuzunguka na unaokutana nao kwenye maisha ikiwemo kutotoa ahadi ambazo huwezi kuzitimiza.
Ikitokea umeahidi kufanya jambo ukishindwa kulifanya omba msamaha pasipo kutoa visingizio visivyoeleweka.
Usiwe mtu wa kubadilika badilika kila wakati, fanya tathmini ya maamuzi yako juu ya jambo fulani kabla ya kutoa msimamo wako hadharani ili kuepuka kuonekana kigeugeu mfano ukisema nimeacha ulevi acha kweli usije kuonekana unasafiri kwenda kunywa pombe maeneo ya mbali. kitendo hiki kitakupotezea uamnifu hivyo kukupunguzia heshima.
Jambo lingine linaloweza kukujengea heshima ni kuepuka umbea.
Usiwe mtu wa kutangaza Mambo ya watu pasipo ruhusa yao kwani wataacha kukushirikisha mambo yao wakidhani kuwa utawatangaza hivyo hawatakuheshimu tena.
Tumia lugha nzuri wakati wa mazungumzo iwe kwa njia ya sauti au maandishi, epuka lugha za matusi ili wanaokusikiliza au kusoma ujumbe wako waweze kuuona ustaharabu ndani yako watakuheshimu.
Heshimu mali, mambo na kazi za watu wengine Kama vile kuepuka tabia za wizi, uporaji na kutamani wake, waume wa watu wengine hii itakupunguzia roho ya tamaa na kukufanya uheshimike.
Pia kuwa sehemu ya jamii yako kula nao, cheka nao na ushiriki shughuli zote za kijamii zinazokuhusu iwapo una muda wa kufanya hivyo.