Familia iliyoondolewa kwenye makazi Upanga-Dar yadai kuna matumizi ya nguvu yametumika, waomba mamlaka ziingilie

informer 06

Member
May 11, 2024
50
26
Kwa siku ya jana August 20, 2024 kulibuka taharuki katika eneo la Upanga karibia na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo familia moja ilidaiwa kuondolewa kwenye makazi chini ya uangalizi wa maafisa wa Jeshi la Polisi.
IMG_5727.jpeg

Baada ya maafisa wa Jeshi la Polisi kumaliza kusimamia zoezi la kuondolewa kwa vitu kwenye makazi hayo kuliibuka utata ambao ulipelekea mabishano baina ya watu waliopewa jukumu la kubomoa nyumba pamoja na familia upande wa familia iliyoondolewa, wanafamilia hao walidai kuwa waliendesha zoe hilo kinyume

Ambapo familia iliyoondolewa inadai baadhi ya vitu vikidaiwa kuibiwa wakati wa zoezi la kuondoa vitu ndani ya nyumba kabla ya kubomoa.

Sababu ya kubomolewa kwa nyumba hiyo inadaiwa kuwa ni mgogoro uliopo baina ya familia hiyo na upande wa familia ya Mzee Tambaza.
IMG_5739.jpeg

Ambapo upande wa familia ilivyokuwa inakaa kwenye nyumba kupitia Wakili wao pamoja na Msemaji wa familia, wanadai hakuna utaratibu wa kimahakama unaotoa idhini ya nyumba hiyo kubomolewa.

Lakini upande wa wabomoaji walipotafutwa na wanahabari baadhi ya walioonekana eneo la tukio walikuwa wakikimbia na kukataa kuongea na vyombo vya habari, hata hivyo baadhi ambao hakuwa tayari kunukuliwa walidai kuwa eneo hilo Mahakama imetoa kibali familia hiyo iondoke.

Kumekuwepo na taarifa kuwa familia hiyo ilitaka kupewa na hela upande wa wabomoaji zaidi ya milioni 100 ili kuwataka kuondoka eneo lile lakini wanadai kuwa walikataa kwa sababu wao wanaamini eneo hilo ni lao.

Aidha Diwani wa Upanga, anadai kuwa nyaraka alizonazo mezani kwake zinaonesha wabomoaji ndio wamiliki wa eneo hilo.
IMG_5725.jpeg

Kufuatia hali hiyo familia hiyo imetoa wito kwa mamlaka za juu kumulika suala hilo wakidai kuwa kuna viashiria vya matumizi ya nguvu pamoja na rushwa katika kufanikisha zoezi la kuwaondoa.


View: https://youtu.be/KxoZCIAf8x0?si=hwFFR4b5g9n2cYjW
 
Hizi stori za uongo uongo kila inapotokea bomoa bomoa zitaisha lini? Yaani Mtu mwizi hachagui jinsi ya kutafuta pesa ya bure. Akiguswa tuuu utaskia nilikua na kitu xyz kimepotea. Umaskini ni kansa
 
Haya majambo sio mazur kabisa na yanasikitisha.ila watoto wa mama kizimakazi nasemaje" mwenzako akinyolewa zako tia maji
 
Nyumba upanga imechoooka,si mngechukua m 100 tu mtafute kwingine.
Wajane wa5 wamejazana hapohapo,usikute na watoto wao.
Na hao wajukuu wa Tambaza kuna aliyepanda kidau labda m500.
Wanataka wauze wagawane.
Haya hiyo bomoabomoa km ndio wabomoaji hao si mtawaua.
kwanza Watamaliza sa ngapi? Mseme wanaharibu nyumba na hao walevi wa gongo.
hamna kubomoa hapo.
 
Back
Top Bottom