Fahamu zaidi kuhusu chanzo na dalili za ugonjwa wa fangasi ukeni (Vaginal Candidiasis)

_pjc_

Member
Aug 25, 2019
58
31
UGONJWA WA FANGASI UKENI (VAGINAL CANDIDIASIS)

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua ni tatizo kubwa sana Duniani 75% ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili.

Fangasi ukeni ni miongoni mwa magonjwa ambayo hutesa wanawake kwa namna mbalimbali.

Husababisha miwasho, harufu mbaya, maumivu, majimaji, homa nk kiasi cha kuingilia ratiba na ufanyaji kazi wa kila siku wa mtu.

Huweza kuwakumba wanawake wa aina zote, ila wanawake wenye ujauzito huwa kwenye hatari zaidi.

Ukikosa matibabu mazuri unaweza ukahangaika nao kwa muda mrefu sana, lakini ukipata matibabu mazuri basi ndani ya muda mfupi tu unapona kabisa na kuweza kuwa vizuri.

Maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu kuu mbili nazo ni;

1) MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
Katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka pia dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS

2) MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka.

VISABABISHI
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS, maambukizi haya pia hujulikana kama YEAST INFECTIONS CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia chakula (PHARYNVISAX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke, pia fangasi hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, MFANO mabadiliko katika hali ya PH tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0-4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile.

-MATUMIZI YA MADAWA YA ANTIBIOTICS kama AMPICILLINE, CIPROFLAXINE, AMOXYLINE, DOXYCYCLINE, ERTHROMYCINE, NK
-Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambazo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri pia kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy).
-Magonjwa ya saratani ya tezi koo la Chakula (thyroid cancer).
-Wanawake wenye umri wa miaka 20-30 wapo katika hatari ya kupata
maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira na vitu wanavyotumia.
-Upungufu wa Kinga mwilin kutokana na magonjwa hatar ya saratani, kisukari, ugonjwa wa mononucleosis nk.
-Matumizi ya vidonge vya majira.
-Kujamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex).
-Matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi
-Ujauzito (husababisha kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini kuwa
-Kuvaa nguo za ndani zisizo kauka vzur na kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehemu za siri

DALILI ZA FANGASI UKENI
Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk
  • Kuwashwa sehem za siri
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana (superficial dysapareunia)
  • Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri Mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation)
  • Kupata vidonda ukeni (soreness)
  • Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje wa uke (labia minora)
  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito, uchafu huu unakua kama maziwa yaliyoganda na hauna harufu kali
  • Kutokwa na harufu kali baada ya kushiriki tendo la ndoa
  • Kuchafua chupi mara kwa mara.
MADHARA
Tatizo la fangasi lisipotibiwa mapema huleta madhara makubwa sana kama ifuatavyo
  • Huweza kusababisha kansa ya viungo vya uzazi
  • Huweza kusababisha ugumba
  • Husababisha maumivu kipindi cha kujamiana
  • Kusababisha msongo wa mawazo
  • Kupekea kuvunjika kwa mahusiano.

IMG_0525.jpg
 
Unakutana mdada mzuri na msafi kabisa lakini akivua tu unakuta ana harufu mbaya ukeni kiasi cha ku kuchafua mazingira ya kufanya tendo.

Unaona kabisa sura yake inabadilika na anakosa mood ya show.

Inatia huruma sana.
Pole sana..kama wampenda kweli mpeleke hospitali akapate tiba..ili muenjoy kwa pamoja.

#MaendeleoHayanaChama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom