SOMO LA KWANZA
MAANA YA GRAFTING NA BUDDING
Grafting na buddinging ni maneno ya kiingereza ambayo kwa lugha ya kiswahili ni 'kupandikiza'. Kwenye somo letu ni sawa na kusema 'kupandikiza mche' ikiwa na maana ya miche miwili yenye sifa bora tofauti (mmoja ukiwa na sifa ya ubora au uimara wa mizizi na mwingine ukiwa na tabia ya ubora wa vinasaba (genes) yaani wingi na ubora wa matunda). Huunganishwa pamoja kwa lengo la kusababisha ukuaji wa pamoja kama mti mmoja wenye kufaidi sifa zote za pande mbili.
TOFAUTI KATI GRAFTING NA BUDDING
Grafting na budding ni mbinu za bustani (Horticultural techniques) ambazo zinatumika kuunganisha sehemu za mimea miwili au zaidi ili zikue kama mmea mmoja.
MUDA MZURI , MAZINGIRA SAHIHI NA HATUA ZA KUFUATA ILI KUFANYA GRAFTING NA BUDDING.
Grafting (upandikizaji mche) unaweza kufanyika mahali inapooteshwa yaani kitaluni au mahali mche utakapo pandwa yaani shamban (main field).
Grafting hufanyika pale shina la mche likiwa limefikia upana wa sentimeta moja (1) kwa makadirio ni miezi sita ( 6 ) baada ya kupanda na urefu wa sentimeta kumi ( 10 ) kutoka usawa wa udongo (shina linapoanza kuchomozea (collar root ). Zoezi hili ni muhimu lifanyike sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha ili kufanikisha muunganiko mzuri wa mishipa ya kikonyo (scion) na shina mzizi / mmea mzazi (root stock).
Vikonyo kwa ajili ya ku'graft ni lazima vitoke kwenye miti teule ya aina inayohitajika mfano kama lengo ni parachichi aina ya HASS, Kwenye kuchukua vikonyo inashauriwa uchukue vyenye upana wa saizi tofauti tofauti ili kufiti katika mashina mizizi ya saizi tofauti tofauti pia.
Grafting ( sehemu ya maungio ) ikifikia urefu wa sentimeta 20-25 inaweza kupelekwa shambani kwa ajili ya kupandwa. Ilimradi tu kidonda ( sehemu ya maungio ) iwe imepona na kuungana vizuri na shina lillilopandikizwa.
Vyanzo mbalimbali vinaelezea nyanja mbalimbali za utofauti wa mbinu hizi mbili mfano kwenye nyanja za uimara, ubora, matumizi, aina n.k japokiwa mbinu hizi mbili kimsingi hutofautiana kwenye namna ya uunganishwaji wa mche au mti kama ilivyoelezwa hapo juu.
UTOFAUTI ni kama ifuatavyo
Kwenye grafting sehemu ya juu ya mmea / mche mmoja (kikonyo) hukua kwenye sehemu ya mzizi ya mmea / mche mwingine yaani, sehemu ya ahina ya mmea mmoja hupachikwa kwenye kwenye mmea mwingine.
Hivyo kwenye GRAFTING, kikonyo ni sehemu ya shina.
Kwa upande mwingine ( BUDDING).
Budding (upandikizaji mche / mti) ni mbinu ya kilimo cha bustani ambapo TAWI CHIPUKIZI (a bud) la mti mmoja ( mti pendwa / mti pendekezwa ) / (desired crop) huchomekwa au hupandikizwa kwenye mti mwingine kwa lengo la kukua kama mti mmoja.
Kwenye budding, mche chipukizi kwenye mti mkuu (bud au kikonyo) huchukuliwa kutoka kwenye mmea mmoja na kukuzwa kwenye mmea mwingine. Mti unaotumika kukuzia chipukizi (bud) ya mti mwingine huitwa mmea mzizi /mmea mzizi.
Hivyo kwenye budding, kikonyo ni mche chipukizi (a bud)..
Kwenye aina hii ya upandikizaji wa miche / miti yaani budding kikonyo ni tawi chipukizi (a bud)
tawi chipukizi (kikonyo) huchomekwa shinani kwenye gome la mmea mzizi (mmea mzazi) patanifu ili kutengeneza muunganiko thabiti wenye manufaa kati ya mmea pendwa (cultivar) na mmea mzazi
Bud (tawi chipukizi)
Ni mche mchanga au otea ambao kwa kawaida hutokea pembeni mwa shina
CULTIVAR
mmea wenye sifa pendwa
/ pendekezwa.
Ni aina ya mmea ambayo watu wameuzalisha maabara na wenye sifa fulani pendwa endelevu kwa kila kizazi kipya kwa njia za kitalaamu mfano muongozo wa tishu na udhibiti makini wa uzalishaji wa mbegu.
Rootstock ( mmea mzizi / mmea mzazi)
VIGEZO VYA KUFANYA GRAFTING NA BUDDING BORA.
1. Utengamano wa kikonyo na shina mzizi (Compatibility of scion and root stock).
Kwa kuwa grafting inahusisha uunganishwaji wa kikonyo na shina mzizi (joining of vascular tissues), mimea inayokosa mfumo wa mishipa mfano nyas, migomba, vitunguu, mahindi, mtama, mpunga (lacking vascular cambium) n.k haziwezi kufanyiwa grafting. Kwa ujumla kadiri mimea miwili inavyokua na mfanano zaidi wa asili (vinasaba / genes). Uwezekano wake wa muunganiko (grafting) unaongezeka. Grafting has a high success rate when performed with plants of the same family and genera (identical clones and intra-species crops).
2. Mpangilio wa mishipa na mgandamizo wa uunganishwaji (Cambium alignment and pressure).
Mifumo ya mishipa ya shina mzizi na kikonyo lazima iunganishwe kwa kukazwa kisawa sawa kuelekea uelekeo wa ukuaji wa kawaida (normal growth). Mpangilio sahihi na mgandamizo toshelevu inachochea mishipa kuunganikana kwa haraka, hivyo kuruhusu virutubisho na maji kusafiri kwa haraka kutoka kwenye mizizi kwenda kwenye kikonyo.
3.Kukamilika wakati wa hatua inayofaa kwa mmea.
Grafting hukamilika wakati ambapo kikonyo na shina mzizi vinauwezo wa kutengeneza tishu komavu hasa za kuponya kidonda (grafting union). Kwa kiwango kikubwa joto huathiri mmeakipindi cha mabadiliko yake. Kama hali ni ya joto sana (temperature greatly affect plant physiology), grafting njiti huweza kutokea (premature grafting may result).
4. Utunzaji sahihi wa eneo la muunganiko.
Baada ya grafting zoezi la kulea miche husika ni muhimu ili kurejea katika hali ya afya bora kwa muda. Vifungashio mbalimbali hutumika kulinda kikonyo na shina mzizi visipoteze maji. Pia kulingana na aina ya grafting, kamba hutumika kuupatia uimara zaidi sehemu ya muunganiko. Wakati mwingine ni vyema zaidi kuondoa machipukizi eneo la chini ya muunganiko (removing suckers / pruning) ili yasizuie ukuaji wa kikonyo.
FAIDA ZA KUFANYA GRAFTING
1. Uharakishwaji wa mti kupevuka (precocity)
Grafting inasaidia mche kufikia mzazi yaani utoaji wa maua na matunda pasipo kupitia ya awali ya ukuaji (kipindi kati ya kuchipua kwa mbegu mpaka ukomavu wake kabla ya uzazi). Kwa miti mingi ya matunda, kipindi hiki hudumu kwa miaka 5, 9 mpaka 15. Kufanya grafting kwa vikonyo vilivyokwisha pevuka inasaidia mche / mti kufikia uzazi ndani ya miaka miwili (2).
2. Dwarfing (kwa lugha ya kiswahili ni kibete)
Ni mchakato unahusisha mzao mpya wa mmea uliobadilishiwa sifa zake asilia za jamii yake mfano kuwa mdogo zaidi / dwarf kwa lengo la kuongeza uzalishaji na ubora wa matunda, kupunguza ajali za wavunaji wa matunda.
3. Urekebishaji
Grafting inasaidia kurekebisha hitilafu kwenye shina la mti ambayo ingezuia usambazaji wa virutubisho mfano kubanduka kwa gome la mti kwa wadudu waharibifu kama vile panya. Katika hali hii grafting huweza kurekebisha na kuunganisha tishu zilizopatwa na hitilafu na kuruhusu usambazaji wa virutubisho kuendelea.
4. Uzalishaji kasi wa mmea chotara
Grafting inasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa mmea chotara. Miche chotara huchukua miaka 10 au zaidi kutoa maua au matunda kwa mizizi yake ila grafting inapunguza muda wa maua na kufupisha kipindi kuelekea uzazi.
5. Ukinzani wa magonjwa na wadudu.
Kwenye maeneo ambayo wadudu wa udongo (soil borne disease / pest) wangezuia kumea kwa aina pendwa ya mmea muafaka huwa ni matumizi ya mmea mzizi unaostahimili magonjwa na wadudu kupitia grafting.
6. Kuubadilisha mmea (changing cultivar)
Grafting inasaidia kuubadisha mmea wa zamani kuelea mmea mpya wenye faida zaidi pasipo kuung'oa ule wa awali. Hivyo kuifanya njia hii kuwa ya haraka zaidi kuliko kupanda upya mbegu nyingine au mmea mwingine ambao hujafanyiwa grafting.
7. Uthabiti wa maumbile (Genetic consistency)
Kwenye kilimo biashara, kwenye uthabiti kwa maana ya saizi, rangi na ladha ya matunda hudumishwa kwa kikonyo chenye sifa zinazohitajika, hasa kwa mimea ya matunda yenye asili ya tabia zaidi ya moja mfano parachichi, embe n.k
SOLMO LA PILI
KILIMO HAI
KILIMO HAI ni mfumo wa kilimo cha usimamizi na uzalishaji kinachounganisha kiwango cha juu cha mwingiliano wa viumbe hai (biodiversity) pamoja na shughuli za mazingira zinazotunza maliasili, ustawi wa wanyama pamoja na kuzalisha chakula salama kwa walaji.
Ni mfumo wa kilimo unaotumia mbolea za asili kama vile mbolea ya samadi, majani, mifupa pamoja na kuweka msisitizo juu ya mbinu kama vile kupanda mazao kwa mzunguko / kubadilishana (crop rotation) na kupanda mazao mchanganyiko yenye kufaidiana (intercropping, uthibiti wa wadudu kibaiolojia na kukuza wanyama wanaowinda wadudu .
Viwango vya kilimo hai vimeundwa kuruhusu matumizi ya vitu vya asili huku ikipiga marufuku matumizi ya matumizi ya bidhaa za viwandani (synthetic substances). Mfano wa dawa asilia za kuua wadudu ni kama vile mmea wa pareto pamona sumu ipatikanayo kwenye mizizi ya baadhi mimea (rotenone).
Bidhaa za viwandani zinazoruhusiwa ni Copper, sulfate, elemental sulfur, Ivermectin.
Mbinu za kilimo hai zinathibitiwa kimataifa na kutekelezwa na mataifa mengi kwa sehemu kubwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na 'International Federation Of Agriculture Movement' (IFOAM). Shirika mwamvuli kwa mashirika ya KILIMO HAI liloundwa mwaka 1972.
Tokea mwaka 1990, soko la vyakula visivyo na kemikali limeongezeka kwa kasi kufikia dola bilioni 63 dunia nzima kwa mwaka 2012. Uhitaji huu umepelekea ongezeko la mashamba yanayoendeshwa kwa misingi ya kilimo hai kwa kiwango cha 8.9% kwa mwaka 2001-2011.
Kwa mwaka 2020, hekta milioni 75 (ekari milioni 185.325) duniani kote zilizolimwa kwa misingi ya kilimo hai, ikiwakilisha 1.6% ya mashamba yote duniani.
Mashamba yaliyo thibitishwa kufuata kanuni na misingi ya kilimo hai hekta milioni 70 ulimwenguni, ikiwa nusu ya jumla ya mashamba yote yapo Australia.
Mnamo julai, 1939 Bw. Ehrenfried Pfeiffer mwandishi wa maswala ya kilimo cha mfumo hai (bio-dynamic agriculture) alikwenda Uingereza kufuatia mwaliko wa Bw. Walter James, mwanariadha wa nne wa Northbourne - Uingereza kama mtangazaji katika shule ya majira ya kiangazi na mkutano wa Betteshanger (Betteshanger Summer School and Conference) juu ya kilimo cha mfumo hai katika shamba la Northbourne huko Kent ikiwa na moja ya madhumuni makuu ya kuwaleta pamoja watetezi na mbinu mbali mbali za kilimo hai.
Bw. Howard alihudhulia mkutano ambapo alikutana na Bw. Ehrenfried Pfeiffer. Mwaka ulifuata Bw. Northbourne alichapisha jarida lake la kilimo hai kwa kuangalia ARDHI ndipo hapo alipobuni neno 'ORGANIC FARMING'.
Mkutano wa Betteshanger umeelezwa kuwa kama kiungo kinachokosekana kati ya kilimo cha mfumo hai (bio-dynamic agriculture) na aina nyingine za kilimo hai (organic farming).
Mnamo mwaka 1940 Bw. Howard alichapisha kitabu chake alichokiita 'An Agriculture Testament' kwenye kitabu hiki alitumia neno la Northbourne 'organic farming' kazi ya Bw. Howard ilienea sana na kujulikana kama baba wa kilimo hai (Father of Organic Farming) kwa kazi yake ya kutumia ujuzi na kanuni za kisayansi katika mbinu za JADI na ASILI.
Huko marekani Bw. J.I Rodale ambae alipendezwa sana na maneno ya Bw. Howard na mifumo yake ya kilimo hai vilivyozinduliwa katika miaka ya 1940 ikiwa kama shamba la KILIMO HAI la majaribio. Taasisi ya Bw Rodale pamoja na chombo chake cha HABARI vikaanza kutetea mbinu za kilimo hai kwa umma mpana zaidi vilivyopelekea kuenea kwa kilimo hai. Kazi zaidi ikafanywa na Bi. Eve Balfour na wengine wengi duniani kote.
Kuongezeka kwa mwamko wa mazingira kwa umma kwa nyakati hizi za kisasa zimebadilisha harakati za kilimo hai kutoka kuendeshwa kwa usamabzaji (supply)-driven) na sasa kuendeshwa kwa mahitaji (demand-driven). Kuongezeka kwa bidhaa hizi pamoja na ruzuku za serikali zimevutia zaidi wakulima.
Katika ulimwengu unaoendelea (developing world), wazalishaji wengi hulima kulingana na mbinu za KITAMADUNI zinazolinganishwa na kilimo hai lakini hazijaidhinishwa (not certified) na ambazo huenda zisijumuishe MAENDELEO YA KISAYANSI katika nyanja ya kilimo hai.
CHIMBUKO LA KILIMO HAI
Kilimo kilikua kinafanywa kwa maelfu ya miaka bila kuhusisha matumizi ya kemikali za viwandani.
Mbolea za viwandani zilitengenezwa kwa mara ya kwanza katikati ya karne ya 19 . Mbolea hizi za awali zilikuwa za bei nafuu, zenye nguvu na rahisi kusafirisha kwa wingi, vivyo hivyo katika viuatilifu vya kemikali katika miaka ya 1940, kupelekea muongo huo kujulikana kama 'zama za viuatilifu' / 'THE PESTICIDES ERA'.
Mbinu hizi mpya za kilimo zikiwa na manufaa katika muda mfupi, zilikuwa na madhara makubwa ya muda mrefu mfano mgandamizo wa udongo, mmomonyoko wa udongo (SOIL EROSION) na kupungua kwa rutuba pamoja na wasiwasi wa kiafya kuhusu kemikali sumu zinazoingia katika vyakula.
Mwishoni mwa miaka ya 1800 na mapema miaka ya 1900, wanasayansi wa bailogia ya udongo (SOIL BIOLOGY) walianza kutafuta njia za kurekebisha athari hizi huku wakidumisha uzalishaji wa juu (high crop yield).
Mnamo 1921, mwanzilishi wa harakati za kilimo hai Bw. Albert Howard na mkewe Bi. Gabrielle Howard, watalaamu wa mimea walianzisha taasisi ya tasnia ya mimea kuboresha mbinu za jadi za kilimo hai nchini India. Pamoja na mambo mengine, walileta zana za kilimo zilizoboreshwa na mbinu bora za ufugaji kutoka kwenye mafunzo yao maalumu; kisha kwa kujumuisha vipengele muhimu vya mbinu za kitamaduni za Kihindi, itifaki za mzunguko wa mazao tofauti (crop rotation), mbinu za kuzuia mmomonyoko wa udongo na taratibu bora za matumizi ya mboji na samadi.
Mnamo mwaka 1924, Bw. Rudolf Steiner alitoa mfululizo wa mihadhara 8 kuhusu kilimo kwa kuzingatia ushawishi wa mwezi na sayari (non-physical beings and elemental forces). Walishikiliwa kujibu ombi la wakulima waliogundua uharibifu kwenye udongo, kuzorota kwa afya ya na ubora wa mazao kutokana na matumizi ya mbolea za kemikali.
Kwa kuchochewa na uzoefu wa mbinu hizi za jadi za kilimo Bw. Albert Howard alivyorejea nchini Uingereza mwanzoni mwa miaka 1930 alianza kutangaza mfumo wa kilimo hai.