Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,230
Ni kitu cha kushangaza lakini pia ni cha kujifunza kwa wenzetu wa marekani ambapo kuna baadhi ya taaluma zinahitaji mtu awe na degree ya kwanza ya kitu kingine ndio apate nafasi ya kupata degree ya kwanza ya taaluma hizo..yaani entry qualification is a bachelor degree.
Miongoni mwa taaluma hizo ni
(1)Sheria
(2)Udaktari na
(3)Uandishi wa habari.
Umeshajiuliza ni kwanini imekuwa hivyo hata kwa waandishi wa habari??Nikiwa na maana waandishi mnaowaona wanareport vituo vikubwa USA wana degree 2.
Hii inaondoa makosa na kuongeza ufanisi katika kazi mfano mtu aliyesoma degree ya uchumi kisha akaenda kusomea uandishi wa habari huyu atakuwa na uwezo mkubwa wa kuandika kuhusu mijadala ya kiuchumi,kuchambua uchumi,kuhoji wachumi na kutoa fafanuzi mbalimbali tofauti na ambaye hajui uchumi kabisa atabaki kusikiliza kama kasuku na misamiati ya kiuchumi itakuwa kama sindano masikioni kwake mfano ukiangalia waandishi wa habari juzi waliokwenda kumuhoji CAG wameshindwa kutumia fursa ya kuuliza kuhusu hali ya ukaguzi nchini wameishia kuuliza utaenda wapi baada ya hapa,swali ambalo hata mimi naweza kuuliza.
Hii inaenda sambamba kwa taaluma zote zikiambatanishwa na taaluma ya habari,hawa watu wanakuwa na uwezo mkubwa wakuhoji na kuchambua mambo.
Kwa upande wa sheria,ni vigumu kwa mwanasheria aliyesoma sheria tu kumuhoji mkandarasi aliyetengeneza barabara mbovu tofauti na mwandishi aliyesoma uhandisi atakovyohoji na kuthibitisha.
Ukisoma sheria bila taaluma nyingine utaishia kwenye kesi za wizi wa kuku..kesi nyingine zote zitakushinda utasikiliza ya kuambiwa tofauti na hukumu angetoa mwanasheria mwenye taaluma ya kitu kilicho mbele ya mahakama.
Kwa madaktari ni tofauti kidogo hawa hulazimika kusoma degree ya kwanza ya kitu kingine ili kuwaongezea ufanisi na kupunguza makosa ,wakiamini mtu akitoka huko atakuwa amestaarabika na kuwa sawa na kzi hiyo muhimu.