Fahamu madhara ya chuchu bandia "soother" kwa mtoto

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,094
7,226
Matumizi ya cha chuchu bandia zenye jina maarufu la ‘soother' yanaonekana yakishika kasi katika miaka ya karibuni kutoka katika fikra kwamba ni ya familia tajiri hadi kwa jamii ya kipato cha chini. Wengi wamekuwa wakihadaika na faida chache zipatikanazo kama kumzubaisha mtoto katika michezo mbalimbali na hata hivyo kumfanya aache kulia ovyo.

Kama ni mama au mlezi ambaye anamlea, hupata muda mwingi wa kufanya shughuli zake bila usumbufu wa mtoto kulialia ovyo. Licha ya hivyo wengi wanapendelea soother kwa kuwa zinawafanya watoto wapendelee chakula sana kutokana na kukinyonya kwa muda mrefu.

Wakati mwingine wanawake wengi hufurahia kumzubaisha na chuchu hiyo ili asihangaike na ziwa lake na hivyo kumfanya anyonyeshe kwa vipindi anavyovitaka.

Madhara ya hizo chuchu ‘soother' .
1.mtoto kushindwa kuzungumza kwa muda mwafaka.
Hali hii hutokana na kukosa muda wa kujifunza kuzungumza maneno kadhaa yakiwamo tata, dada, mama na minong'ono kadhaa anapokuwa mchanga. "Mtoto ana hatua zake katika ukuaji. Unapompa mtoto ‘soother' unamnyima nafasi ya yeye kuweza kuzungumza maneno ya awali.

"Maneno haya ya awali ndiyo yanayoanza kuumba matamshi ambayo mwishowe mtoto huyatamka katika kuumba maneno. Utaratibu huo humfanya aweze kuzungumza kwa wakati Mwafaka,

2.Hupunguza hamu ya kunyonya ziwa la mama.
mara nyingi watoto wachanga wanaopewa chuchu bandia katika wiki za kwanza za maisha yao huwa hawapendi kuendelea kunyonya kwa kuwa humpunguzia hamu ya ziwa. Ubongo wa mtoto unapaswa kuzoea kwanza chuchu za mama.

3.Mtoto kuumwa tumbo mara kwa mara.
wanawake wengi ambao wanafanya kazi wamekuwa wakisumbuliwa sana na tatizo la watoto wao kupata homa za mara kwa mara, lakini asilimia kubwa inatokana na chuchu bandia.Ukiangalia watoto wanaoongoza kwa kuumwa kila siku ni wale wa wafanyakazi. Mara nyingi mama zao wanawaacha na waangalizi, lakini chuchu bandia wanazopewa hazizingatii kanuni za usafi hivyo kumsababishia mtoto magonjwa ya tumbo.

4.Kuathiri mfumo wa kulala wa mtoto.
Mtoto anapoendelea kunyonya kwa muda mrefu huathirika pia kisaikolojia kwa kuiona soother kama moja ya kitu chake cha lazima. Hivyo watoto wengine hushindwa hata kulala kwa kuwa tu wamekikosa kifaa hicho.

"Kinamwathiri pia kisaikolojia. Wapo watoto leo hii hawawezi tena kulala kwa kuwa tu wamekosa kifaa hiki

5.Kuumiza fizi za mtoto.
Wengi wao wamepata michubuko mikubwa kwenye fizi. Unajua chuchu bandia ni ngumu na si laini kama chuchu ya mama."

"Tatizo lingine ni watoto wanaweza kupata mzio kutokana na vifaa hivi.".

USHAURI:

A. KUWA NA USAFI MUDA WOTE.
kuwa usafi wake ni mgumu sana hasa kwenye kitundu cha kutolea maziwa kwa wale wanatumia chuchu bandia za kunyonyea maziwa mbadala.

"Kinamama wengi hawana uelewa mzuri jinsi ya kusafisha. Kila siku utaishia hospitali mtoto akiharisha. Pale inapolazimu, mtoto apewe maziwa kwa kikombe chenye mdomo mkubwa

B. Kuacha kuiga iga "uzungu" mtaani.
ni vizuri kinamama wakashauriana na wataalamu wa afya kuhusu mambo ambayo yanafaa kwa watoto wao na siyo kusikiliza au kuiga mambo yanayofanywa na wengine mitaani.

Kwa leo ni hayo tu, unakaribishwa kwa maoni.

attachment.php
attachment.php
attachment.php
1pcs-High-Quality-Funny-Teeth-Silicone-Baby-Nipple-font-b-soother-b-font-font-b-holder.jpg
images
images
images
 
santeee nilishawah ambiwa kitu kama hiki.mtoto atachelewa kuongea. lakin pia kuumwa tumbo na fizi za mtoto zitavimba na hapa umeniongezea nyingine mkuu asante kwa kutukumbusha
 
Nilipiga marufuku mtoto wangu asitumie hii kitu nikaonekana bonge la mshamba! Ubishi wa kiume tu ndiyo ulinifanya nikomae na msimamo wangu! Asante kwa elimu hii kubwa sana
 
santeee nilishawah ambiwa kitu kama hiki.mtoto atachelewa kuongea. lakin pia kuumwa tumbo na fizi za mtoto zitavimba na hapa umeniongezea nyingine mkuu asante kwa kutukumbusha

Asante sana kwa kuwa mwerewa ... natumai utawasaidia na wenzio waweze elimika zaidi. pamoja tujenge taifa.
 
Nilipiga marufuku mtoto wangu asitumie hii kitu nikaonekana bonge la mshamba! Ubishi wa kiume tu ndiyo ulinifanya nikomae na msimamo wangu! Asante kwa elimu hii kubwa sana

Watanzania wengi ni wabishi sana... ila nashukur kwa kuwa na utambuzi wa hili jambo toka mapema ..kwani si kila ukionacho basi cha faa.. asante sana mkuu . pamoja tulijenge taifa.
 
kuumwa tumbo ndo kulifanya niache kutumia

Pole sana mkuu.. kwani mtoto kuamsha mwenge mara kwa mara sio jambo jema kabisa kwa ustawi wake kiafya na kiakili. ila nikupe big up kuubwa sana kwa kulitambua hilo janga uka amua kuchukua hatua mapema.
 
santeee nilishawah ambiwa kitu kama hiki.mtoto atachelewa kuongea. lakin pia kuumwa tumbo na fizi za mtoto zitavimba na hapa umeniongezea nyingine mkuu asante kwa kutukumbusha

Ok, shukrani sana.... natumai utawafahamisha na wengine zaidi kwani unaonekana kuw ana ufahamu flani juu ya madhara ya hii kitu. pamoja tulijenge taifa.
 
Umeona enheee.... naomba uendelee kuwa balozi mzuri wa kuokoa kizazi chetu hiki cha uzungu mwingi.

Kumnywesha kwa kijiko ni bora zaidi kwani vinaosheka kirahisi coz vipo open
Muhimu mtoto awe na vyombo vyake visiwe vya share
 
Back
Top Bottom