Fahamu kuhusu soko la hisa na Dar es salaam dse

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,655
6,007
Habari za wakati huu;
NI matumaini yangu kwamba mnaendelea vizuri na kudumu katika ujenzi wa taifa lenu.Kama ilivyo ada leo nimeona nilete mjadala kuhusu soko la HISA la Dar es Salaam.Msingi wa majada huu unatokana na ukweli kwamba uchangamfu wa Soko letu la HISA na mchango wake katika UCHUMI na Uhamasishaji wa maendeleo bado unahitajika na haujatumika ipasavyo.

"Hata hivyo kabla ya kuzama katika mjadala naomba nitoe angalizo.Kwanza kabisa Mimi sio mtaalamu wa Biashara ya hisa na masoko ya hisa na wala sina ufahamu wa kina a utendaji kzi wa masoko ya hisa na kwamba andiko hili ni matokea ya mtazamo na uelewa wangu binafsi na iwapo kutakuwa na makosa basi ninamani kwamba tutaendelea kuelimishana na kuhamasishana."

Soko la Hisa ni Nini?
Soko la hisa kama yalivyo masoko mengine ni eneo ambalo hufanyika biashara ya kuuza na kununua hisa.Hisa ni vipimo vya umiliki wa biashara au kampuni fulani.Katika soko la hisa thamani ya hisa hupanda na kushuka kwa kutegemea kiasi cha hisa zilizopo sokoni na idadi ya hisa zinazohitajika.Hivyo basi unapokuwa muwekezaji katika soko la hisa unakuwa unanunua na kuuza makampuni au biashara mbalimbali.

Pembeni kubadilikwa kwa bei kwa sababu nilizotaja hapo juu huw pia kuna kubadilika kwa bei kutokana na athari au matukio mengine ya kibiashara,kiuchumi na hata wakati mwingine kisiasa.

Nini Faida za Kumiliki Hisa katika SOKO la HISA?
Unapomiliki hisa katika soko la hisa unakuwa ni Mmiliki wa Kampuni husika kwa kiasi cha hisa unazomiliki.Kampuni inapotengeneza Faida na kutangaza Faida basi inakuwa inatoa gawio la sehemu ya Faida kwa wamiliki ambao huitwa wanahisa ambao ni watu wote ambao wanamiliki hisa za kampuni husika.

Je HISA zako zina matumizi Mengine?

Katika Muktadha wa kiuchumi hisa zina matumizi mengi.Unaweza kutumia Hisa zako kama Dhamana ya KUombea Mkopo Benki,Kwa Lugha Nyingine kama wewe una miliki HISA za NMB basi unaweza kwenda na Hisa zako NMB na NMB wakakupa MKOPA kwa UDHAMINI wa Hisa zako za NMB.Kwa Lugha nyingine unajikopesha PESA zako mwenye kisha unajigawia faina inayotokana na malipo yako ya Mkopo.

SOKO la HISA na Dar es Salaam lina Muundo Gani?
Kwa mujibu wa vyanzo tofauti,Soko la Hisa la Dar lina muundo wa aina tofauti ambao unahusisha masoko tofauti kama vile ENTERPRISE GROWTH market ambalo linalenga kampuni changa zinazoibuka na Main Market ambalo ndilo soko Kubwa.Hivyo Basi Muwekezaji anaweza kununua Hisa katika SOko Mojawapo ya hayo.Hata hivyo DSE inatoa huduma tofauti za kuhamaishsa uwekezaji katika SOKO la HISA.

JE KAMPUNI inahitaji nini ili iorodheshwe katika SOKO la HISA?

Baada ya kulitazama soko katik Mtazamo wa muwekezaji sasa tulitazame soko kama wasaka MITAJI yaani wamiliki na waanzilishi wa Kampuni.Kampuni yoyote inaweza kuorodheshwa katika soko la Hisa la Dar es Salaama kwa kuzingatia vigezo na masharti ya SOKO la HISA na Vile vya mamlaka ya Masoko ya Dhamana na MITAJI CMSA ambao pia wanaisimamia DSE.

Ili kuorodhesha Kampuni yako katika Hisa utatakiwa kuonyesha kwamba una uwezo,utayari wa kuweza kusimamia Biashara na kutengeneza Faida.Ila pia unatakiwa uoneshe kwa kina uhitaji wako wa mtaji na namna ambavyo mtaji huu utatumika.Itakupasa kuushawishi Umma wa wawekezaji kwamba Biashara yako ina tija na kwamba wakiweleza kwako watapata FAIDA nzuri na mtaji wao utakuwa salama.

Nimeeleza kwa ufupi sana ili kuchokoza mjada ili kila mmoja wetu ajdili na kuonesha uelewa wake kuhusu soko la HISA la Dar es Salaama na Iwapo anatamani kushiriki katika SOKO hili.Ili kufahamu zaidi kuhus DSE tafadhali tembelea tovuti rasmi ya DSE

Ninakutakieni Wakati mwema sana.
 
Mkuu masoko tz ile kariakoo mtandaoni iliishia wapi?
 
Haijaisha mzalendo,ni kazi in progress.I hope lengo lako siokunifanya nihisi kuna mambo yamekwama bali ni kuhamasisha mjadala maana hata hiyo project uliyotaja itapendeza zaidi kam ikiwekwa kama platform.All in all sitakulaumu iwapo ndio fikra zako maana hata mimi huwa nina fikra za namna ila huwa nina ujasiri wa kukubali kujikosoa na hat kukosolewa.

Angalizo.Nimenote huwa aina yako ya comment huwa zina mrengo uwo wa kutaka mtu ahisi hawezi au anachokiamini hakiwezekani.Epuka sana njia au mtazamo huo isipokuwa tu kama kuna ulazimamaana kuna wakati uankuwa unajitia vidole, mwenyewe na kuona raha.Wwenimpambanaji ukiona wazo zuri mtandaoni onyesh apreciation au litumie.Kuna siku utakumbuka haya mawazp ya wadau humu ujilaumu.

Jitahidi sana uwe na hoja chanya.Sisi wote ni waja
 
Waja leo waondoka leo.

Mimi natka kuwa chachu ya ufanikishaji na ufanis wa wazo lile. Although ni muumin wa context na particular na diversity.

Mm nitakula na wewe sahan moja mpaka ipatikane best ya wazo lile. Mim ndo chachu ya ufanisi wake, na"opt" kuwa changamoto itatukayo kuleta ufanisi.

Narudia, nitakul na wewe sahani moja
 
duh
 
Back
Top Bottom