Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,675
- 6,045
Habari za wakati huu;
Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea salama na jitihada zenu za kujenga uchumi binafsi na wa Taifa.
Kwa heshima na taadhima kabisa nimeona leo nilete mjadala kuhusu Mtu aliyefilisika au kwa lugha ya mtaani Kufulia na Mtu Maskini/Fukara.Lengo la kuleta mjadala huu ni ili kuhakikisha kwamba wote kwa pamoja tunaondokana kabisa na Umaskini/Ufukara
Umaskini ni hali ya kifikra zaidi kuliko ya kiuchumi.Ndio maana wapo maskini wengi ambao wanamiliki Mali nyingi kama vile mashamba,madini.Kwa mfano Taifa kama Tanzania,Congo na Nchi nyingi za Africa zinaitwa nchi maskini lakini zinamiliki utajiri mkubwa zaidi kuliko nchi nyingi ambazo zinaitwa nchi TAJIRI.Sababu kubwa ni kwamba UMASKINI/UFUKARA ni hali ya KIFIKRA na sio hali ya kiuchumi.
Maskini wengi wanatumia nguvu na akili zao nyingi kutajirisha wengine huku wao wakiendelea kutopea katika shida na matatizo.Je SIFA za maskini/fukara ni nini?
Mtu aliyefilisika/BROKE ni mtu ambaye ama ana madeni mengi au kipato chake kimepungua kwa kiasi kikubwa au hana kipato cha uhakika.Mtu aliyefilisika/kufulia huwa anakuwa katika mapambano ya kujikwamu.Utamkuta akiwa bado na mawazo chanya ya kuamini kwamba mabadiliko yatatokea na kwamba lazima yeye achukue hatua ili kuleta mabadiliko.Sifa zake ni kama hizi:

- Mtu maskini au fukara daima atalaumu wengine kwa yote anayopitia,Mfano atalaumu wazazi wake,rafiki zake,mfumo wa elimu,mfumo wa uchumi,sheria za nchi,viongozi wa nchi,viongozi wa dini,majirani na wengine wengi ila HATAJILAUMU yeye mwenyewe.
- Mtu Maskini daima hajui thamani yake wala ya alicho nacho na hupokea na kukubali na kuridhika na kile ambacho anapea au kupangiwa na wengine bila kujali maslahi yake
- Mtu Maskini huwa hana mipango,wala malengo wala matarajio yoyote katika siku,mwezi,mwaka wala maisha na wala hana utayari wa kubadilika au kubadilisha mazingira yake
- Mtu maskini huwa na wivu,choyo,kinyongo uwoga,uzembe uvivu na kiwango cha juu cha Ujinga
- Mtu Maskini huamni kwamba yeye hawezi na huwa hatazami fursa wala kuwa na matumaini.
Mtu aliyefilisika/BROKE ni mtu ambaye ama ana madeni mengi au kipato chake kimepungua kwa kiasi kikubwa au hana kipato cha uhakika.Mtu aliyefilisika/kufulia huwa anakuwa katika mapambano ya kujikwamu.Utamkuta akiwa bado na mawazo chanya ya kuamini kwamba mabadiliko yatatokea na kwamba lazima yeye achukue hatua ili kuleta mabadiliko.Sifa zake ni kama hizi:
- Huwa anakubali makosa na kuchukua wajibu wake kuijiondoa katika changamoto zinazomkabili bila kukata tamaa.
- Anafahamu thamani ya alicho nacho na daima hutafuta kupata faida maradufu kutokana na kile alicho nacho.
- Huwa ana mipango na malengo makubwa na asiyeogopa changamoto zozote zile zinazomkabili
- Hachukii wala kuwa na kinyongo na wivu na wengine bali huona kama ni changamoto pale anapojaribu kupambana kuhakikisha kwamba anainuka na kubadilisha maisha na hujaribu sana kuwatumia wengine ili aweze kubadilisha hali yake ya kiuchumi