fahamu jinsi ya kurudisha vitu vilivyofutika kwenye kompyuta simu sd card na nk

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
519
915
fahamu jinsi ya kurudisha vitu vilivyofutika kwenye kompyuta simu sd card na nk

kama ulikua unatafuta njia rahisi ya kufanya kuweza kurudisha vitu vilivyofutika kwenye simu kompyuta flash sd card basi makala hii ni yako . watumiaji wengi wa simu kompyuta flash na nk huwa wanapoteza vitu vyao akuna mtu ambaye hajawahi kupoteza vitu vyake ila inshu ni kuweza kuvirudisha tu kuna baadhi wanajua wengine hawajui watumie njia gani kuweza kurudisha vitu vyao vilivyofutika na kupotea kabisa katika vifaa vyao.

katika posti zilizopita nilishawahi kugusia software moja ya kuweza kurudisha vitu vilivyofutika kwenye kompyuta | laptop yako lakini fahamu tu software zinauwezo tofauti tofauti kama ili haikuweza kukusaidia basi hii itakua muafaka wa tatizo lako kabisa . njia hii itaweza kukusaidia kurudisha vitu vyako vilivyopotea kwenye mfumo wa simu , window na mac os pia zinafanya kazi Bila shida yoyote hile.

kwa wale watumiaji wa kompyuta unschotakiwa kufanya na kuweza kupakua program ya wondershare recovery it yaani itaweza kuchagua aina gan ya window unatumia kama mac os au window za kawaida kisha utapakua na kuinstall hiyo software kwenye kifaa chako.

programu hii itaweza kukusaidia kuweza kurudisha vitu vyako bure kabisa kwenye simu flash au hard disk uliyoifuta vitu vyako na kuvipoteza kabisa.baada ya kuweza kudownload na kuinstall. itaweza kuifungua na kuchagua ni vitu gani unataka kuvirudisha baada ya kuvipoteza.

program nyingine ambayo nzuri kwa kuweza kurudisha vitu vilivyopotea kwenye kompyuta | laptop | simu yako ni DR FONE ni moja ya programu nzuri Sana ya kutumia kuweza kurudisha vitu vyako pia ni bure hivyo unaweza kuitafuta sasa hila program hii inafanya kazi kwa simu ambazo ziko rooted kama haijawa root unaweza kuitafuta video jinsi ya kuroot simu yako sasa.

kwa kutumia program hizo mbili za wondershare recovery it na DR FONE utaweza kurudisha vitu vyako ulivyopoteza kwenye simu au kompyuta yako sasa.

VIPI UMEFANIKIWA KURUDISHA VITU VYAKO TUACHIE MAONI HAPO CHINI SASA


Karibu katika ulimwengu wa teknolojia njoo ujifunze masuala ya simu kompyuta app games maujanja matatizo na suluhisho zake kwa lugha ya kiswahili karibu utajifunza mambo mengi usiyoyajua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom