Fahamu chakula unachopaswa kula ukiwa na zaidi ya miaka 40

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,821
34,207
food

Chakula ni kirutubisho muhimu sana kwa wanadamu na maisha hayangewezekana bila lishe bora.
Hata hivyo licha ya umuhimu wa lishe kwa mwili wa mwanadamu, wataalamu mara nyingi huwa wanazingatia faida za lishe bora na kiwango cha chakula ambacho mtu anapaswa kula kwa ajili ya afya yake.
Wataalamu wametoa angalizo pia na kutoa tahadhari dhidi ya aina ya chakula ambacho watu wanapaswa kula kutokana na hali yao ya kiafya au umri.
Lakini kadri mtu anavyozeeka, kuna aina za vyakula ambavyo mtu anahitaji kula mara kwa mara.
Ukiendelea kuzeeka, unashauriwa ni aina gani ya vyakula unapaswa kula mara kwa mara ili kuboresha afya yako na kinga ya mwili.

Lishe bora ukiwa na miaka 40​

Katika mahojiano na BBC, daktari kutoka hospitali ya chuo kikuu cha Ilorin iliyopo nchini Nigeria alisema ukifika miaka ya 40,kwa kawaida ni muhimu kubadilisha lishe.
Kwa mujibu wa Dkt Sadiya Musa, anasema ni muhimu kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 kuwa muangalifu na afya yake kwa sababu kadri mtu anavyozeeka anaweza kupungua uzito pia.
Hivyo inakuwa rahisi kupata magonjwa.
Mtu mwenye umri mkubwa anahitaji lishe bora ambayo itamfanya kuwa na afya na nguvu, anasema Dkt Sadiya.
Kutokuwa makini katika lishe ukiwa na miaka hiyo , ni hatari kwa afya wakati ambao utapata magonjwa kama kisukari, presha na matatizo ya miguu kunaweza kuathiri mtu.
Dkt Sadiya anasema vyakula ambavyo mtu mwenye umri wa miaka 40 ni pamoja na:
  • Samaki
  • Mboga za majani na mizizi kama moringa,
  • Matunda
  • Kula uyoga badala ya nyama
  • Vyakula vya protini kama maharage ya soya badala ya mayai
Ni muhimu kufanya vipimo vya damu ili kusaidia kupunguza hatari za maambukizi, kwa mujibu wa daktari.
  • Kupunguza kula vyakula vinavyohifadhiwa kwenye makopo
  • Kupunguza matumizi ya limao ni hatari kwa afya
  • Kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula
  • Kupunguza kula nyama, karanga na siagi
n

Daktari amesema pia mtu akifika umri huo hapaswi kuacha kula vyakula alivyozoea ghafla badala yake anapaswa kuacha taratibu mpaka atakapoacha kabisa haswa kwa wale wenye matatizo ya kisukari na presha.

Vyakula asili​

Licha ya kwamba daktari ameshauri kula vyakula vinavyoboresha afya ,ni vyema kupunguza vyakula ambavyo ni hatari kwa afya kwa kuzingatia umri.
Ni muhimu kudhibiti matumizi ya dawa za mitishamba au dawa za hospitalini bila maelekezo ya daktari pia ni hatari kiafya, kwa mujibu wa daktari.
Pia ni muhimu kula vyakula vya asili kama vile mahindi, mtama, maboga na vinginevyo.
n

Maelezo ya picha,
Moringa

Moringa ni chakula maarufu cha asili ambacho ni muhimu.
Jizuie kula vyakula ambavyo vina kemikali.
Dkt Sadiya, anasema watu ambao hawana magonjwa ya kisasa wanawezekana kuwa na lishe bora zaidi.
Aidha daktari amesema watu wenye afya bora, ni kutokana na aina ya chakula cha asili wanachokula na wengine wanapata magonjwa kutokana na uchaguzi mbaya wa chakula. chanzo.BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom